Ana tatizo la kuugua ugua mara mara

Ana tatizo la kuugua ugua mara mara

Mzux

Member
Joined
Jan 19, 2013
Posts
29
Reaction score
7
Nitajitahidi kuandika ufupi kwa kwenda moja kwa moja kwenye suala ambalo kwangu linanichanganya. Nina rafiki wa kike ambaye tumefahamiana kwa takribani miaka miwili na tumekubaliana tuwe wachumba na nimeshamtambulisha kwa baadhi ya ndugu zangu akiwemo mama yangu.

Tatizo ni kwamba ni bahati kupita mwezi hajaumwa. Sasa naomba kupata uzoefu kwa yeyote ambaye ameshakumbana na hali kama hii.

Lengo langu ni kutaka kujua endapo hali kama hii itabadilika au ndo mtu anakuwa hivyo maisha yote(mgonjwa mgonjwa). Binti ndo mwenye hili tatizo(kuugua ugua mara kwa mara)
 
Tangu mwanzo hakukwambia juu ya matatizo ya afya yake? Mchukue umpeleke hospitali kuangalia tatizo ni nini, utapata pa kuanzia. Pole sana Mkuu.
 
Tangu mwanzo hakukwambia juu ya matatizo ya afya yake? Mchukue umpeleke hospitali kuangalia tatizo ni nini, utapata pa kuanzia. Pole sana Mkuu.

Kila nikimuuliza huwa anasema ni siku hizi tu na kwamba zamani hakuwa na matatizo hayo. Hivyo nimekuwa najitahidi kumvumilia nikijua huenda hali hii itaisha ila bado
 
Nitajitahidi kuandika ufupi kwa kwenda moja kwa moja kwenye suala ambalo kwangu linanichanganya. Nina rafiki wa kike ambaye tumefahamiana kwa takribani miaka miwili na tumekubaliana tuwe wachumba na nimeshamtambulisha kwa baadhi ya ndugu zangu akiwemo mama yangu. Tatizo ni kwamba ni bahati kupita mwezi hajaumwa. Sasa naomba kupata uzoefu kwa yeyote ambaye ameshakumbana na hali kama hii. Lengo langu ni kutaka kujua endapo hali kama hii itabadilika au ndo mtu anakuwa hivyo maisha yote(mgonjwa mgonjwa).
Binti ndo mwenye hili tatizo(kuugua ugua mara kwa mara)
Hua anaugua nini, na niwakati gani hasa amekua akiugua?
Maradhi ni neno pana sana mkuu, nivema uka kamilisha swali lako ili ufanye wepesi kwa wajuzi wa maradhi na tiba.
 
Jambo la kwanza unatakiwa uumuulize yeye kama yeye labda ana tatizo la kiafya la kudumu ili upate jibu ndo utajua pa kuanzia
 
Hua anaugua nini, na niwakati gani hasa amekua akiugua?
Maradhi ni neno sana mkuu, nivema uka kamilisha swali lako ili ufanye wepesi kwa wajuzi wa maradhi na tiba.

mara nyingi huwa anasema anahisi uchovu chovu. Na mara nyingi mafua na kikohozi, miguu kuvimba pamoja na kupungukiwa damu.
 
Jambo la kwanza unatakiwa uumuulize yeye kama yeye labda ana tatizo la kiafya la kudumu ili upate jibu ndo utajua pa kuanzia

nimekuwa nikiuliza hili swali mara kwa mara lakini amekuwa akisema hali hii imeanza miaka ya karibuni( mwaka jana)
 
Aisee niliwahi kugonjeka kwa mtindo huu. "Homa za mara kwa mara hazikatikii".... Wakati huo nilikuwa chuo. Baada ya hapo nilioa na hadithi ikaisha. Inawezekana hata stress huyo Dada zinamtesa. Nini kimebadilika mwaka huu mmoja kwenye kuumwa kwake?
Jitahidi usimbwage.
 
Oa tuu yaani umeipiga miaka yotee miwili leo unamuona kimeo? Oa ww huyooo
 
kitu cha msingi au uzoefu niliotaka kupata hapa ni kama kuna mtu aliyeoa au mwenye ushuhuda kutoka kwa mtu aliyeoa mtu mwenye tatizo la kuugua ugua baadaye matatizo hayo yakakoma au kuendelea maana binafsi nahisi pia kuwa huenda stress na kuishi bila kupata huduma kwa muda mrefu ikawa huenda kisababishi cha matatizo pia.
 
mkapime naye umeme,sio aende mwenyewe akuletee majibu.Muende pamoja.
mmmmmmh..
kuna mtoto mmoja alienda kupima mwenyewe akaniletea majibu, kwani kuna noma hapa??
 
mmmmmmh..
kuna mtoto mmoja alienda kupima mwenyewe akaniletea majibu, kwani kuna noma hapa??
fikiria mfano angekuwa positive angekuletea majibu kuwa kanasa?anyway mi huwa naamini ile kwenda mguu kwa mguu.
 
Back
Top Bottom