Anaandika Askofu Bagonza: Nadhani Tunajichanganya? Au ni Mimi Najichanganya?!

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
ANAANDIKA ASKOFU BAGONZA

NADHANI TUNAJICHANGANYA?! Au ni Mimi Najichanganya?!

1. SAFARI YA VATICAN

Tungepatana nyumbani kwanza na wawakilishi wa Papa kabla ya kwenda kwa Papa. Tumempiga Padre wake; Tumetengeneza Wakatoliki Vijora; Tunamdhalilisha Kitima, halafu tunaenda kwa Papa. Hatari ipo ya kuambiwa, “Kama hamkumsikiliza Musa na Manabii, hamtaweza kushawishika hata mtu akifufuka”(Luka 16:31). Patana na mshtaki wako kabla ya kwenda kwa Kadhi.

2. MABEBERU:

Tumezoea kuzizodoa nchi za Ulaya kuwa ni mabeberu. Vatican iko Ulaya. Je, Hata Papa ni Beberu? Naye anataka kuchimba Uranium yetu?

3. AMANI YA NCHI

Wizara ya Mambo ya Nje inamuomba Papa aiombee nchi yetu iwe na Amani na Utulivu. Wizara ya Mambo ya Ndani inasema nchi iko salama imetulia. Hawawasiliani? Nani msemaji wa nchi?

4.MARIDHIANO

Wazee wa Chama wanataka Maridhiano. Bunge linasema nchi iko sawa. Tume iko kazini kuchunguza. Nani mkweli? Je kuna ukweli tusioujua hadi tuumulike kwa tochi ya Tume? Je tunataka maridhiano kabla ya ukweli?

5. CHADEMA na CCM

Wapo wanaosema Chadema Imekufa lakini wanaisema kila siku. Huyu ni marehemu mwenye nguvu. Makada wa CCM wanasema CCM tunatamba nayo. Ukiiangalia unaiona ni mfungwa asiye na pingu. Nani zaidi kati ya marehemu anayeishi na aliye hai lakini amekufa?

6. YALIYOTOKEA OKTOBA 29

Siku hii inatusumbua mpaka tunaenda Vatican. Bado kwenda Mecca. Kama waliokufa hawajulikani; waliowaua wanajijua. Dunia inajua makundi yote mawili. Hekima ya WAJALUO inasema, “kuchelewa kwenda kujisaidia, hakuzuii njaa kuuma”. Tukubali: Tuliua, Walikufa; tuombe radhi, tuwajibishane na kusonga mbele.

7. TUNDU LISU

Waliompiga risasi hawajapatikana lakini walioiba michango yake wamekamatwa. Yeye yuko rumande. Mahakama imeenda likizo na haki yake iko likizo. Fikiria daktari akienda kupumzika katikati ya operesheni mgonjwa?!

8. WIZARA YA MAMBO YA NJE

Hii Wizara inaonyesha tuko vitani. Kimsingi ina mawaziri 4: Kombo, Kabudi, Nyalandu na JK. Msiniulize JK ni nani maana mtamuona anatumwa katika masuala magumu nje. Waliobaki 3 na manaibu 2, wanaunda kikosi kazi cha mawaziri wa wizara. Msiniulize nani ni Boss maana Kabudi anaweza kujikuta ni Naibu Waziri. TUNAJIKANYAGA MNO.

9. Taifa likiwa katika mtifuano kama tulio nao, linakuwa kama mgonjwa. Hawezi kwenda kwa daktari akagoma kuvua nguo. Tuvue zote na madaktari watuingizie vidole kila mahali ili kubaini ugonjwa ulipo ndipo tutibiwe.

Wajaluo wakibanwa TEZI DUME husingizia wanaumwa kichwa.
Sasa Wajaluo wa TEZI JIKE hao usiseme!
 
Taifa likiwa katika mtifuano kama tulio nao, linakuwa kama mgonjwa. Hawezi kwenda kwa daktari akagoma kuvua nguo. Tuvue zote na madaktari watuingizie vidole kila mahali ili kubaini ugonjwa ulipo ndipo tutibiwe.

Wajaluo wakibanwa TEZI DUME husingizia wanaumwa kichwa.
Ha ha haa 🤣🤣
Askofu ashakuwa muhuni Sasa.
 
Amesema vema Askofu Bagonza. JK alikuwa Rais, akamfanya Samya kuwa pumzikio, alipokuwa mstaafu, akamlipa pumzikio lake umakamu, baadaye urais, huku yeye ikiwa boss wake. Baada ya mambo kuparanganyika, boss kajifanya waziri wake wa mambo ya nje, na mkufunzi wa Makombo.
 
ANAANDIKA ASKOFU BAGONZA

NADHANI TUNAJICHANGANYA?! Au ni Mimi Najichanganya?!

1. SAFARI YA VATICAN

Tungepatana nyumbani kwanza na wawakilishi wa Papa kabla ya kwenda kwa Papa. Tumempiga Padre wake; Tumetengeneza Wakatoliki Vijora; Tunamdhalilisha Kitima, halafu tunaenda kwa Papa. Hatari ipo ya kuambiwa, “Kama hamkumsikiliza Musa na Manabii, hamtaweza kushawishika hata mtu akifufuka”(Luka 16:31). Patana na mshtaki wako kabla ya kwenda kwa Kadhi.

2. MABEBERU:

Tumezoea kuzizodoa nchi za Ulaya kuwa ni mabeberu. Vatican iko Ulaya. Je, Hata Papa ni Beberu? Naye anataka kuchimba Uranium yetu?

3. AMANI YA NCHI

Wizara ya Mambo ya Nje inamuomba Papa aiombee nchi yetu iwe na Amani na Utulivu. Wizara ya Mambo ya Ndani inasema nchi iko salama imetulia. Hawawasiliani? Nani msemaji wa nchi?

4.MARIDHIANO

Wazee wa Chama wanataka Maridhiano. Bunge linasema nchi iko sawa. Tume iko kazini kuchunguza. Nani mkweli? Je kuna ukweli tusioujua hadi tuumulike kwa tochi ya Tume? Je tunataka maridhiano kabla ya ukweli?

5. CHADEMA na CCM

Wapo wanaosema Chadema Imekufa lakini wanaisema kila siku. Huyu ni marehemu mwenye nguvu. Makada wa CCM wanasema CCM tunatamba nayo. Ukiiangalia unaiona ni mfungwa asiye na pingu. Nani zaidi kati ya marehemu anayeishi na aliye hai lakini amekufa?

6. YALIYOTOKEA OKTOBA 29

Siku hii inatusumbua mpaka tunaenda Vatican. Bado kwenda Mecca. Kama waliokufa hawajulikani; waliowaua wanajijua. Dunia inajua makundi yote mawili. Hekima ya WAJALUO inasema, “kuchelewa kwenda kujisaidia, hakuzuii njaa kuuma”. Tukubali: Tuliua, Walikufa; tuombe radhi, tuwajibishane na kusonga mbele.

7. TUNDU LISU

Waliompiga risasi hawajapatikana lakini walioiba michango yake wamekamatwa. Yeye yuko rumande. Mahakama imeenda likizo na haki yake iko likizo. Fikiria daktari akienda kupumzika katikati ya operesheni mgonjwa?!

8. WIZARA YA MAMBO YA NJE

Hii Wizara inaonyesha tuko vitani. Kimsingi ina mawaziri 4: Kombo, Kabudi, Nyalandu na JK. Msiniulize JK ni nani maana mtamuona anatumwa katika masuala magumu nje. Waliobaki 3 na manaibu 2, wanaunda kikosi kazi cha mawaziri wa wizara. Msiniulize nani ni Boss maana Kabudi anaweza kujikuta ni Naibu Waziri. TUNAJIKANYAGA MNO.

9. Taifa likiwa katika mtifuano kama tulio nao, linakuwa kama mgonjwa. Hawezi kwenda kwa daktari akagoma kuvua nguo. Tuvue zote na madaktari watuingizie vidole kila mahali ili kubaini ugonjwa ulipo ndipo tutibiwe.

Wajaluo wakibanwa TEZI DUME husingizia wanaumwa kichwa.
Sasa Wajaluo wa TEZI JIKE hao usiseme!
Mwanafasihi kasema nani apinge.
Kombo mhuni
 
C&P
 
SIFA KUBWA KWA MTU KUWA ASKOFU NI KUTOKUWA NA AKILI KAMA HIVYO

SERIKALI IMEENDA KUONANA NA PAPA KWA AJENDA ZAKE NA SIYO KUWAPLEASE HAWA WAVAA MAGAUNI WA HAPA BONGO NA NJAA ZAO

SERIKALI INAZUNGUMZA NA MWENYE MMBWA HAIONGEI NA HAWA VICHAA NA MAGAUNI YAO YANAYONUKA MIKOJO
 
Kwa taarifa yako Roman wanafanya kazi kwa uraratibu wa kueleweka, sio huu upuuzi wa amri toka juu ulioko hapa. Ukeinda Roma ukapeleka taarifa yako, wanaanza chini kwa wahusika kupata ukweli. Kwa ushahidi walio nao Roma hapa nchini, hakuna namna serekali inaweza fanya lobbying ya bei rahisi. Hao ni wakristo wanajitambua kuliko maelezo.
 
Back
Top Bottom