ANAANDIKA MKE WANGU KWA HABARI YA MAGONJWA YAKE

Pelly

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
287
Reaction score
370
Naomba msaada na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya kuhusu historia yangu ya kiafya.

Kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya. Sehemu kubwa ya maisha yangu nimekuwa nikiumwa mara kwa mara; leo tatizo hili, kesho lingine. Mwaka 2018 nilifanyiwa upasuaji na kuondolewa figo ya kushoto kutokana na adrenal tumor.

Mwaka 2020 nilianza kupata ganzi na hali ya moto miguuni, pamoja na ganzi kwenye paji la uso na maeneo yanayozunguka kiuno. Nilikuwa na maumivu ninapokaa na ninaposimama. Nilifanyiwa NCS (Nerve Conduction Study) na nikaelezwa kuwa kuna tatizo kwenye sensory na motor nerves. Nilipewa dawa ambazo nimeendelea kutumia hadi sasa, lakini sijaona mabadiliko makubwa. Dalili huja na kuondoka; wakati mwingine zinaweza kukaa kwa saa kadhaa bila kusumbua sana, lakini wakati mwingine huwa kali.

Baadaye nilianza kupata misuli kukaza na muscle spasms, ambazo mpaka sasa zinanisumbua. Kwa sasa nimekuwa nikihisi kukaza zaidi upande wa kulia kuanzia kwenye nyonga kushuka chini, pamoja na mgongoni.

Pia nimekuwa na historia ya matatizo ya tumbo kwa miaka mingi. Niliwahi kuambiwa nina michubuko tumboni na gesi nyingi. Kuna vipindi hali huwa nzuri, lakini wakati mwingine dalili hurudi. Baadaye nilianza kupata maumivu ya muda mrefu kwenye tumbo la chini. Baada ya vipimo niliambiwa nina endometriosis, cysts ndogo, pamoja na abnormal cells kwenye cervix.

Nilifanyiwa biopsy ya cervix, na niliambiwa majibu hayakuonyesha cancer.

Pia nimekuwa nikiambiwa mara kwa mara nina UTI/infection ninapokwenda kupima, lakini nilipofanyiwa urine culture Mloganzila, hawakupata findings za infection. Nimerudia tena kipimo na bado nasubiri majibu.

Kuanzia mwezi wa Mei nilianza kupata au kuongezeka kwa matatizo mengine kama maumivu ya kichwa karibu kila siku, kizunguzungu, maumivu ya miguu yote miwili, maumivu na kukaza kwa joints na misuli, shingo na bega kukaza na kuuma, moto na ganzi miguuni, pamoja na ganzi usoni.

Nilienda kwa daktari wa mifupa kutokana na maumivu hayo na nikaelekezwa kuanza clinic ya rheumatoid. Nilipewa prednisone kwa mwezi mmoja pamoja na tidinazine. Baada ya kutumia dawa hizo nilianza kupata ladha ya sukari mdomoni, na nilipopima nikaambiwa kuna sukari kwenye mkojo.

Hata hivyo, mpaka sasa bado sijakaa sawa. Bado nina maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kuishiwa nguvu mara kwa mara, maumivu ya tumbo, maumivu upande wa kulia yanayozunguka kiuno na kushuka mguuni, muscle spasms, maumivu ya mgongo, shingo na bega, moto na ganzi miguuni, pamoja na ganzi usoni. Wakati mwingine nakojoa mara kwa mara mkojo usioisha...au wakati mwingine hautoki...kuishiwa nguvu muda mwingi...kupepesuka japo nakula ...hamu ya kula kuongezeka ghafla na njaa pia ambayo sikuwaga nayo

Pia nimeanza kupata njaa isiyoisha na kula sana kuliko kawaida, hali ambayo ni mpya kwangu, pamoja na macho kuwa mazito.

Kwa sasa nimefika hatua ambayo naumwa mara nyingi na sijui ni tatizo gani hasa linalosababisha hali hii au kama matatizo haya yana uhusiano.

Kuhusu tatizo la cervix, daktari amesema atanifanyia LEEP ili kuondoa cells zote zenye tatizo.

Naomba wataalamu wa afya wenye uzoefu wanisaidie kuelewa historia hii kwa ujumla na kama kuna uwezekano wa matatizo haya kuwa yana uhusiano au ni matatizo tofauti yanayotokea kwa wakati mmoja.

Nimekuwa nikihangaika na hali hii kwa muda mrefu, nimezunguka hospitali na kutumia dawa mbalimbali lakini bado sijapata nafuu ya kueleweka. Hali hii sasa imenichosha sana kimwili na hata kihisia, mpaka kuna wakati nalia kwa sababu sijui nianzie wapi kupata tiba sahihi.

Naomba msaada wa wataalamu, hasa mtu ambaye anaweza kuangalia history yangu yote kwa pamoja, badala ya kuangalia kila dalili peke yake.

Asanteni.
 
Pole sana ndugu yetu,hata sasa Mungu amekupigania na utapona usikate tamaa.Natumai watakuja wataaluma wa afya,watashauri vyema.Keep your faith up.
 
Mkuu nakushauri tenga kiasi cha pesa ikibidi hata kuuza asset kama unazo maana afya ndio mtaji wa kwanza, nenda hospitali kubwa Asia au Ulaya, naamini utapata msaada mkubwa zaidi kama umeshazunguka hapa miaka na matatizo yanaongezeka
Nimeshuhudia watu kadhaa waliongaika bongo miaka ila baada ya kwenda kutibiwa nje mara nyingi unakuta ni jambo linalotibika kirahisi
Wenzetu wana vifaa na wataalamu wa hali ya juu kuliko sisi, ndio maana hata wanasiasa wako huwa hawatibiwi hapa
 
Siku ambayo nilikuwa mgonjwa sana hadi kuhuzunika moyoni nilimuuliza Mungu kwanini haya yananipata ? Kwani sikujua sababu na wala sikujua nani mbaya wangu,

Nilipata majibu kwake.
1. Nikajua ni kwanini naumwa.
2. Mbaya wangu ni nani,
3. Nani si mbaya kwangu,
4. Na mwisho nikajifunza kumpenda yeye zaidi na kulijua kusudi la maisha yangu.
 
Habari!
Pole kwa kuumwa.
Umejieleza vyema, ingawa kuna mambo yanahitaji ufatiliaji wa kuongea na mtoa huduma ya afya moja kwa moja pamoja na ukaguzi wa mwili/examination.

Mfano: 1: Kuna umuhimu wa kujua endomentriosis, je seli husika zilipatikana kwenye maeneo gani? Kwani inaweza kuwa sababu ya maumivu mbalimbali unayoyapata.

2: Baada ya operation uliweza kuwa na ufatiliaji wa vichocheo vya mwili/homoni na madini mwilini?

3: Ulishawahi kuonana na daktari bingwa wa masuala ya homoni/endocrinologist?

4: Kama kuna vipimo vyovyote ulivyofanya wakati wa matibabu yako ni muhimu kuwasilisha kwa mtoa huduma ya afya ili kujua aanzie wapi pia kutokana na vielelezo husika badala ya kuanza upya.

5: Aina ya uvimbe uliopatikana kwenye tezi/adrenal gland na kama vipimo vilifanyika kufatilia hili.
 
Sikua ambayo nilikuwa mgonjwa sana hadi kuhuzunika moyoni nilimuuliza Mungu kwanini haya yananipata ? Kwani sikujua sababu na wala sikujua nani mbaya wangu,

Nilipata majibu kwake.
1. Nikajua ni kwanini naumwa.
2. Mbaya wangu ni nani,
3. Nani si mbaya kwangu,
4. Na mwisho nikajifunza kumpenda yeye zaidi na kulijua kusudi la maisha yangu.
Asanteni sana nyote, huyo ni mke wangu na ijumaa watamfanyia hiyo kitu nimesahau jina pale ocean road hospital, ila wenyewe wanasema ni kukwangua uvimbe ulionekana tumboni then maumivu ya tumbo yatapona, unajua tatizo hospital huwezi kwenda na vipimo toka kwingine so inabidi uanze moja ndiyo shida, mara nyingi akionekana shida regency akienda mloganzila wakipima wanakuta negative.
 
Mkuu nakushauri tenga kiasi cha pesa ikibidi hata kuuza asset kama unazo maana afya ndio mtaji wa kwanza, nenda hospitali kubwa Asia au Ulaya, naamini utapata msaada mkubwa zaidi kama umeshazunguka hapa miaka na matatizo yanaongezeka
Nimeshuhudia watu kadhaa waliongaika bongo miaka ila baada ya kwenda kutibiwa nje mara nyingi unakuta ni jambo linalotibika kirahisi
Wenzetu wana vifaa na wataalamu wa hali ya juu kuliko sisi, ndio maana hata wanasiasa wako huwa hawatibiwi hapa
Labda tuanze kupitisha daftali au kadi, mbona harusi wanachanga budget hadi ya M60+?
 
Ukiona hosp wameshindwa geukia upande wa pili sisi ni wa Afriaca.
 
Sema watu wamekuwa wabaya sana..
Pole sana kwa mkeo na ww pia kwa kuuguza..
Vipi mkeo ameshabahatika kupata watoto?
Kama bado inawezekana ikawa hormonal imbalance inapelekea kupata matatizo mbali mbali...

Wawili wote wa kike mmoja 13yrs old na wa pili 5yrs old 21 Dec 26 anafikisha 6yrs,labda useme hilo gap, asante
 
Back
Top Bottom