Anaandika mwana Simba Yericko Nyerere

Anaandika mwana Simba Yericko Nyerere

MO ataonewa bure

Tatizo la Simba ni Bodi nzima

Kuna kundi la 51% hawa nao hawana msaada

Bodi ndiyo yahusika na sajili na kandarasi zote, hivyo lawama zitupwe kwao

Mchezaji kama Bocco hakupaswa ongezewa mkataba

Mikataba yote yatakiwa iwe na kipengele cha kuvunja endapo mchezaji hataonesha uwezo wake.

Bonus ziondolewe, ziweke baada ya ushindi wa medali

Wakipoteza mechi wakatwe mishahara
 
Hesabu ni rahisi sana:-
1. Kuliko usajili waxchezaji 6 wa kigeni wa milioni mia mbili kila mmoja sawa na bilioni moja na milioni mia mbili halafu baada ya miezi sita unawatoa kwa mkopo kwenda sijui Ihefu huko ni bora usajili wachezaji 3 wa milioni mia nne kila mmoja sawa na shilingi bilioni moja na milioni mia mbili ile ile.
2. Ni bora kuwa na wachezaji watatu wa kigeni wenye uwezo mkubwa wanaoingia kwenye first eleven moja kwa kwa moja tangu siku ya kwanza wanasajiliwa na wakakupa matokeo kuliko kuwa na rundo la wachezaji 6 wa kigeni wenye uwezo mdogo wanaokaa benchi na hata wakicheza wanakupa matokeo mabovu.

Kwenu viongozi wa Simba, bodi nzima ya Simba na mwekezaji hesabu hizo hapo juu tafakarini kuelekea super league ya Afrika na pesa za kutosha za usajili mtapewa na maandalizi muanze mapema maana mwezi wa nane sio mbali.
Usisahau kuna kuumia, kuchoka, out of form, suspensions
 
Mambo mengine siyo wanajiandikia andikia tu. Hebu wewe Yericko Nyerere hebu ukuje utueleze hapa. Hao 89% ya wachezaji wasiofaa kuitumikia Simba ni wachezaji gani? Hawa waliofikisha Simba robo fainali ya African Champions league?
Hawa walioifunga Yanga?
Hawa waliofika nusu fainali ya Azam Federation Cup?
Hawa walioiwezesha timu kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu?
Wachezaji hawa waliofanikiwa kuiingiza Simba kwenye Top Ten ya viabu bora Afrika?

Hebu jifunzeni kuwa wanamichezo aisee, mnalalamika sana hadi mnatia aibu. Simba imejipatia mafanikio makubwa sana, kama una jicho hilo unapaswa kuwa umeliona.
Punguzeni uswahili. Ipeni Club na wachezaji maua yao. Siyo msubiri miaka 20 ijayo ndiyo muanze kusema mliwahi kuwa kwenye Top 10 ya vilabu bora Afrika.

Na hizo hisa 49% wewe shabiki zinakuathiri nini?
We Mo punguza jazba. Sisi tunataka makombe na siyo mambo ya kufa kiume sijui nusu fainali asfc
 
Back
Top Bottom