Anaandika Zuhura Yunus wa BBC

Anaandika Zuhura Yunus wa BBC

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
NAWAZA kwa nini baadhi ya nchi za AFRIKA zinaona tabu kufanya LOCKDOWN au hata PARTIAL LOCKDOWN katika kupambana na janga la COVID-19?

NAWAZA inakuwaje baadhi ya nchi nyingine za kimagharibi na hata za Afrika Mashariki na Kati zimefanikiwa vipi kukabiliana na janga hili hata wasiwe na kifo hata kimoja.

NAWAZA iwapo mabasi ya masafa marefu, yaani mikoani yanaweza kuzuiwa ili kupunguza kasi ya kusambaza virusi vya korona.

NAWAZA kama safari za ndege za kuingia nchi za Afrika pamoja na safari zozote mipakani zisitishwe kwa muda mpaka nchi ziweze kudhibiti kusambaa kwa virusi vya korona.

NAWAZA kuhusu nchi zenye kutumia usafiri wa maji kusitisha safari hizo kwa muda.

NAWAZA kwani nikiswali nyumbani bila ya kwenda msikitini/kanisani dua yangu haitopokelewa?

NAWAZA hivi Mungu mwingi wa Rehema ataniadhibu au kunipa madhambi kwa sababu sijaenda kufanya maombi kwenye nyumba ya ibada na badala yake nikasali nyumbani?
NAWAZA ili watu wasikose rizki, hatuwezi kuwa wabunifu na kutumia bodaboda kununua vitu na kutuachia nje ya nyumba.

NAWAZA Hawawezi watu wakapanga foleni na kuingia mmoja mmoja madukani kuepusha kusambaa kwa virusi vya korona.
NAWAZA mama lishe, wauza vitafunio asubuhi kama vitumbua n.k, hawawezi kwenda kwenye maeneo yao kwa muda maalum na kwa zamu na kuondoka haraka baada tu ya kumaliza kuuza vyakula hivyo.

NAWAZA nchi za Afrika haziwezi kusitisha kudai bili za maji au angalau kupunguza gharama za kulipia.

NAWAZA wauza bidhaa masokoni hawawezi kukaa mita mbili baina ya muuzaji na muuzaji.

NAWAZA serikali hazina mifuko maalum ya maafa na dharura kuweza kugawa chakula kwa familia ambazo hazitoweza kumudu chakula wakati wa PARTIAL LOCKDOWN.

NAWAZA pesa za makusanyo ya kodi haziwezi kutumika kugawa kwa kila familia simu moja ya mkononi angalau wanafunzi waweze kudurusu kwa njia ya kidijitali.
NAWAZA mabadiliko na ubunifu muhimu hasa kununua vitu mtandaoni na kwa njia za simu.

NAWAZA kuna ubaya gani kujua takwimu za watu wote waliopimwa, walioathirika na kufa kutokana na virusi ili niweze kujikinga zaidi.

NAWAZA Mwana Mfalme na Waziri Mkuu wa Uingereza walijitangaza walipoathirika ila kuna usiri mkubwa miongoni mwa viongozi.
 
Keshakuwa brainwashed huyo mama, anaona Muingereza ndio kipimo cha kila kitu kwa kuwa tu wanamuwezesha kwenda chooni, mbona hasemi kuna za Ulaya kama Swedeni, Island hazijafanya lockdown, Wananchi walikuwa wanajiachia tu zaidi hata Bongo, Bars zote, migahawa, masoko, parks zipo wazi na maambukizi na waliokufa Sweden ni wachache kuliko huko kwa mataahira Uingereza walikofunga kila kitu na kubomoa Uchumi lkn bado wamekufa kwa wingi zaidi, ...
 
Heri yake yeye aliyeweza kuwaza vyema tena kwa sauti, kuliko wale waliogoma kuwaza na kutwa kushauri watu wajifukize na kupiga nyungu.
 
Mpaka sauti toka nyikani (chattle) itakapoamua!

Sent using Jamii Forums mobile app
wanaowazia yote hayo ni watu wakipato fulani au wenye hali ya juu kidogo katika jamii zetu, wananchi wenggi tunategemea kupata kiasi ndo tutumie hta hyo mifuko ya hifadhi za kijamii haina kitu ilipaswa sasa kutumika ili kwezesha hta hyo partial lockdown ila acha tueendlee kuwaza kwani wote tunawaza kma tukiweka lockdown kama tutaweza jikimu au kufa kwa njaa kabisa
 
Keshakuwa brainwashed huyo mama, anaona Muingereza ndio kipimo cha kila kitu kwa kuwa tu wanamuwezesha kwenda chooni, mbona hasemi kuna za Ulaya kama Swedeni, Island hazijafanya lockdown, Wananchi walikuwa wanajiachia tu zaidi hata Bongo, Bars zote, migahawa, masoko, parks zipo wazi na maambukizi na waliokufa Sweden ni wachache kuliko huko kwa mataahira Uingereza walikofunga kila kitu na kubomoa Uchumi lkn bado wamekufa kama wadudu, ...
Upumbavu ni ugonjwa mbaya pengine kuliko corona
 
wanaowazia yote hayo ni watu wakipato fulani au wenye hali ya juu kidogo katika jamii zetu, wananchi wenggi tunategemea kupata kiasi ndo tutumie hta hyo mifuko ya hifadhi za kijamii haina kitu ilipaswa sasa kutumika ili kwezesha hta hyo partial lockdown ila acha tueendlee kuwaza kwani wote tunawaza kma tukiweka lockdown kama tutaweza jikimu au kufa kwa njaa kabisa
Ungesema hivi: mbona tushaweka hiyo partial lockdown? Mfano shule na vyuo vishafungwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Keshakuwa brainwashed huyo mama, anaona Muingereza ndio kipimo cha kila kitu kwa kuwa tu wanamuwezesha kwenda chooni, mbona hasemi kuna za Ulaya kama Swedeni, Island hazijafanya lockdown, Wananchi walikuwa wanajiachia tu zaidi hata Bongo, Bars zote, migahawa, masoko, parks zipo wazi na maambukizi na waliokufa Sweden ni wachache kuliko huko kwa mataahira Uingereza walikofunga kila kitu na kubomoa Uchumi lkn bado wamekufa kama wadudu, ...
We umeona nchi za ulaya tu mbona katolea mifano na nchi za Kiafrica, acheni upumbavu na ujuaji wa Kijinga,

Mwisho wa Usiku huu ugonjwa unaweza kuja kuisha Kote huko ukabaki hapa kwetu tu, sijui hata watalii mtawapata wapi
 
Weka kielelezo hapa kinachoonyesha kwamba hali ni mbaya zaidi kwetu TZ kulinganisha na nchi za Kiafrika zilizoweka lockdown.
 
Huyo asitake kuleta sifa hapa

Atafute ndoa kwanza aache ile tabia yake
 
Weka kielelezo hapa kinachoonyesha kwamba hali ni mbaya zaidi kwetu TZ kulinganisha na nchi za Kiafrika zilizoweka lockdown.
Bahati nzuri wabunge wa ccm ndio wanaongoza kwa ukimwi, presha, vusukari, makansa, .... Lazima hii covid iwatafune ni suala la muda ... Subiri uone

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom