Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Mkuu Pasco you are really smart na mwandishi mzuri sana!!! unajaribu kucheza na akili zetu kwa kutufanya WTZ hatuna kumbukumbu eeennhhh! your dead wrong. Tulikuwa tunaambiwa na uongozi uliyopita kuwa una orodha ya wauza unga,wakwepa kodi mpaka orodha ya majangili na tukawa tunalaumu kuwa mbona hatuoni kuchukuliwa hatua yoyote na wala orodha haiwekwi hadharani? nadhani wote ni mashahidi ilifika sehemu Serikali iliambiwa "live" legelege aaaahhh "what an insult" kwa kweli sikuelewi ndiyo maana nimekwambia your very smart labda ulitaka kutupima kumbukumbu zetu basi hatujasahau tupo vitani na elewa "VITA HAINA MACHO"
 
Samiah anapaswa kusafiri safari zote ambazo JPM haendi
tutakosa hata mikutano ya muhimu kwa kuendekeza kuchukia safari...
na mwisho tutazidi kuwa taifa la kienyeji..kama one big village
mara amri ya kufanya usafi mara hivi mara vile...as if hakuna nchi zingine tunazoweza jifunza

Bossman ushaandaa fagio lako?
 
hakitaweza kitaongeza tatizo
watu watafanya kazi kwa fear na kutojiamini
bureaucracy itazidi sababu kila mtu atataka kuwa safe side..
kujipendekeza na kuwa infomer ndo kutageuka dili...
na hata ku pretend kufanya kazi kuliko kufanya kazi kutaongezeka..
na culture ya kukaa kimya na kutohoji maamuzi na amri kutoka juu itaongezeka

Wewe ni mbeba maboksi au mganga wa kienyeji!?

Unasema watu wata pretend?...kwenye hizi kazi zetu kuna kitu tunaita target. Na wala target haina usanii wa kusema nita-pretend.

Kwa mfano ikitokea serikali imeweka lengo la makusanyo kutoka bandarini pekee yawe trillion 7 kwa mwaka wa fedha 2016/2017....basi na iwe hivyo...lengo lifikiwe ili huduma itolewe kwa Watanzania...sasa hapo kuna ku-pretend sijui unafanya kazi au hufanyi?

Sisi tuna-deal na results tu. Kama ikitokea hiyo figure (trilion7) haijafikiwa kutokana sijui na rushwa au bandari kukosa ufanisi...basi tunaingia site kwa kushtukiza na kuanza timua timua. Mbona watanyooka tu.

Ndio maana tunasema chuki zako hizo hazisaidii kitu. Zaidi yakuonekana na wewe ulikuwa sehemu ya wale waliokuwa wakifaidi mfumo mbovu.
 
Wewe ni mbeba maboksi au mganga wa kienyeji!?

Unasema watu wata pretend?...hizi kazi zetu kuna kitu tunaita target. Wala target haina usanii wa kusema nita pretend.

Kwa mfano ikitokea serikali inataka makusanyo kutoka bandarini pekee yawe trillion 7 kwa mwaka wa fedha 2016/2017....na iwe hivyo...sasa hapo kuna kuna ku-pretend sijui unafanya kazi au hufanyi? Sisi tuna-deal na results tu. Kama hiyo figure haijafikiwa kutokana na rushwa au bandari kukosa ufanisi...basi tunaingia site kwa kushtukiza na kuanza timua timua. Mbona watanyooka tu.

Ndio maana tunasema chuki zako hizo hazisaidii kitu. Zaidi yakuonekana na wewe ulikuwa sehemu ya wale waliokuwa wakifaidi mfumo mbovu.

Hamida Malembeka kwani wewe ni kinuka mkojo, mla vumbi, au dada poa?

USA baby
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco

Pasco vipi mkuu nawe ni muhanga nini?? Au nduguyo kabanwa???
PM anataka watu wawe na Data sahihi, ndio maana wapo kwenye hizo ofisi ni maproo. Wacha awachangamshe hakuna kurudi nyuma, hapa kazi tuu!!
 
Last edited by a moderator:
watumishivkama hao ndo hatuwataki kabisa; eti kadharirishwa? mbona yeye alikula billion zote hizo bila hata aibu? na bado kwanza alitakiwa afungwe jela kwa kuhujimu uchumi, unakopa 3bil halafu unazilipa mishahara, sasa wewe pasco ndugu yetu unauhakika gani kama kwel hzo 3bil. zote zililipa mishahara; ndo hizo zinaenda kujenda majumba 73 ya afisa 1 wa tra.
 
watumishivkama hao ndo hatuwataki kabisa; eti kadharirishwa? mbona yeye alikula billion zote hizo bila hata aibu? na bado kwanza alitakiwa afungwe jela kwa kuhujimu uchumi, unakopa 3bil halafu unazilipa mishahara, sasa wewe pasco ndugu yetu unauhakika gani kama kwel hzo 3bil. zote zililipa mishahara; ndo hizo zinaenda kujenda majumba 73 ya afisa 1 wa tra. Hivyo ni wakati wao wa kudhalilika kwa yale waliyowafanyia watz. acha wadharirike tu maana wakati wazitumia kununua mavx ya familia zao waliona fahari lkn MUNGU kawaumbua acha wapate mshahara wao wala huna haja ya kuwahurumia otherwise na wewe ni miongoni mwao.
 
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?

Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.

Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?

mkuu umenifanya nicheke... maana siamini kama uliwaza kabla hujaandika.. kwani wote waliokuwa wakipita kwenye kampeni kutaka uongozi ni wangapi hawakuwahi kuwa kwenye system?? kumbe lowasa angeweza na angekuwa sahihi ila si magufuli na majaliwa
 
mkuu umenifanya nicheke... maana siamini kama uliwaza kabla hujaandika.. kwani wote waliokuwa wakipita kwenye kampeni kutaka uongozi ni wangapi hawakuwahi kuwa kwenye system?? kumbe lowasa angeweza na angekuwa sahihi ila si magufuli na majaliwa

Umewahi kuniona nimesema Lowassa angekuwa sahihi kuliko Magufuli?
 
Fanyani kazi kwa uaminifu na kwa weledi muone kama mtababaika hata akikishtukiza Magufuli mwenyewe. Tatizo mna makando kando yenu ndo maana hamjiamini muda wote mna wasiwasi tu
 
Mkuu Pasco mimi nakubaliana na wewe 100%.

Sina kitufe cha like lakini na zaidi ya like nilitaka kuongeza pesa mbili zangu.

Baaadhi ya hawa watu anaowadhalilisha hadharani mbele ya vyombo vya habari pengine siku za usoni atawahitaji kufanya nao kazi kwa ukaribu sana. Hii dhalila anayoifanya sasa haiashirii mwanzo mzuri.

Magufuli na Majaliwa wamekwisha tuonesha kuwa hawataki mchezo na wana dhamira ya kusafisha serikali. Lakini kuanzia sasa na kuendelea watumie diplomasia kutekeleza azma yao kama ulivyoainisha (mfano - kuwaita watuhumiwa ofisini kwake na huwachamba faragha).
 
Last edited by a moderator:
wangeepuka yote hayo kama wangefanya kazi yao vizuri
 
hakuna ustaarabu hapa kipindi wanavyoiba hizo kontena 2000 hawakuuona ustaarabu
 
Mwaka huu mtaelewa tu, iteni vyovyote,sijui kudhalilishwa,sijui bad governance sie hatujui. Mtanyooshwa sana mwaka huu, tena hiyo mibosi ndo mizuri hiyo, daaaaaadek mtahama nchi mwaka huu
 
Wengine tulihoji kuhusu hilo suala la bunge.

Tukaambiwa eti rais naye ni sehemu ya bunge na ndo maana hulivunja na kulifungua.

Na kwamba eti ile tafrija iliandaliwa na ofisi ya rais na si bunge.

Hii awamu ya tano imeingia na staili ya aina yake kweli.

Tanzania hatuna neno linalotenganisha Parliament na National Assembly to my knowledge . Vyote tunavichanganya na kuviita "bunge". National Assembly = Bunge, wabunge na Spika. Parliament = National Assembly + President. Sie tunaita yote "bunge".

Magufuli alikuwa na inauguration yake. Watu wamempigia gwaride and all. Wabunge (bunge as in National Assembly) wamekuwa na shughuli yao. Iliyopata funds kutoka kwa public na private sources. Magufuli anabanwa na "checks and balances" kuingilia hiyo shughuli ifanyweje.Labda atumie njia ya kushauriana na Spika.

Kuna yule Mama Beatrice Shelukindo alikuwa anafanya parties zake mwenyewe kutafriji wabunge, alichofanya Magufuli si tofauti sana na kumkataza Beatrice Shelukindo asifanye party ila atumie fedha kusaidia hospitali.
 
Mkuu Pasco Nasubiri upropose njia ya kistaarabu ya kupambana na uharamia...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Majaliwa piga kazi. Eti details ziko kwa maofisa wangu. Ndo matokeo ya kuwemo ofisin ukipanga madili tu. Hufuatilii huko chini wanaenda je endaje

Kuweni serious na kazi

Mnakaa ofisin mna chat tu kwenu WhatsApp na Facebook huku chini mnasubiri mletewe taarifa tu

Majaliwa amsha hao
 
I think its more of cultural thing than a principle issue which Pasco is troubled with. A working culture that has made the Public Service a joke 'shamba la bibi'...yaani mtu unaharibu kazi unajua, unadanganya ila kwakuwa ni kulindana au kuficha uozo basi uitwe pembeni uambiwe kwa upole. Hivi ndo vitu tunapaswa kuviondoa Serikalini. Taratibu za kazi zipo na kama hazifuatwi katika kuwasimamisha/ kwafukuza hao watu kazi hapo sawa ila ama zinafuatwa...wacha walale nao mbele tu hii nchi imeendeshwa kijinga sana kwa miongo kadhaa! Mtaisoma namba...
 
Ngabu iko very clear hawana 'blue print' ya nini wafanye
kubadili hii nchi iondokane na kero
so wanashiriki ku expose kero na kukaripia on tv
lakini 'what to do to change things permanently' ndio hawajui...
'the blue print' ya ku replace hii failed system hawana

Mkuu The Boss na Nyani Ngabu, heshima kwenu.

Hamuoni kuwa mnamlalia Magufuli kwa uonevu kweli?

Msukuma wa watu hata mwezi hajamaliza ofisini mnamshutumu kuwa hana mkakati wa long-term. Tusitegemee miujiza toka kwake jamani. I mean, even if the guy is a born-again Christian BUT he doesn't walk on water, nor turn water into wine.

Tumpe muda jamani, isipokuwa huu udhalilishaji hadharani apunguze.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu The Boss na Nyani Ngabu, heshima kwenu.

Hamuoni kuwa mnamlalia Magufuli kwa uonevu kweli?

Msukuma wa watu hata mwezi hajamaliza ofisini mnamshutumu kuwa hana mkakati wa long-term. Tusitegemee miujiza toka kwake jamani. I mean, even if the guy is a born-again Christian BUT he doesn't walk on water, nor turn water into wine.

Tumpe muda jamani, isipokuwa huu udhalilishaji hadharani apunguze.

Well, I am entitled to my opinion.

Pia, mimi nimekuwa mstari wa mbele kuwakumbusha watu humu kukanyaga breki zao kwa sababu mtu hata mwezi hajamaliza lakini wengine tayari wanamwona kama ndo kama kiongozi bora kabis kupata kutokea Tanzania!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom