Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni bullying, kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!, this is bullying.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. It is simple bullying!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

Paskali




My Take:
Tuna tatizo kubwa la uelewa humu, ila pia kufuatia wengi kuchoshwa na kukinaishwa na rushwa na ufisadi, wamekata tamaa na kuhamaniko na mihemuko ya kuchukuliwa hatua kali sana na ikibidi hata wanyongwe!.

Nimenote wengi humu hawakunielewa!, japo nimeanza kwa utangulizi wa kuunga mkono hatua zozote zinazochukuliwa na awamu ya 5 kupiga vita rushwa na ufisadi, siungi mkono the means kwa kutumia populistic approach ya kufanya ili watu waone unafanya!.

Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa haki wa Uingereza, wa presumed innocent until proven guilt beyond reasonable doubt by the court of competant juisdiction!, kinachofanyia ni media trial kumuonyesha mtu ni mkosaji mbele ya camera!.

Sio wengi humu wanaojua kuwa hata mhalifu anahaki!, hata mlaushwa, fisadi, mwizi, pia ana haki!. Hata muuaji aliyehukumiwa kifo kwa kunyongwa naye pia ana haki zake, ananyongwa kwa heshima yake, na kabla hajanyongwa, anaitwa daktari kumpima afya yake, akikutwa na maadhi yoyote, hanyongwi!, bali anatibiwa mpaka apone ndipo adhabu hiyo itekelezwe!.

Japo kisheria hairuhusiwi kamera za waandishi kuingizwa mahakamani, Tanzania tunaingiza kamera mahakamani!, polisi nao wanawaparade wahalifu kwa waandishi wa habari ili hali wako mikononi mwa polisi!, ni kama kuwahukumu kabla!. Kama Kova kila uchao, kwenye screen!, hilo baraza jipya likiishateuliwa, kama kila waziri nae atatembea na media team ili watu waone si itakuwa chaos?!.

Nilichokiona jana anachokifanya PM pia kinakwenda against the principles of Natural Justice
Vita dhidi ya uzembe, rushwa, ufisadi, na ukwepaji kodi yes!, means no!, haki sio tuu itendeke bali pia ionekane kutendeka!.

Paskali
Update.

Mkuu Kiranga, sio kila kitu ni sheria, vingine ni taratibu tuu na kanuni!, ndio maana kwenye ofisi za kizamani kuna vyumba vnawatenganisha ma bosi na wafanyakazi wao!, kuna chumba kinamtenganisha waziri na secretary wake, kuna ofisi ya boss, lengo ya yote hayo ni kuweka heshima na privacy!, nimefanya kazi na wazungu fulani nchini Uswiss, wenzetu wako kwenye full open government initiative, no secrets zozote ofisini, partition zote ni za kioo transparent, computers zote ziko linked kwenye network, desktop zote ni shared, ukipint chochote kuna back copy iko saved, all public communications ni shared.

Huwezi kumrepremand boss infront of his subordinates let alone infront of the media, mtu anaulizwa swali, hajapewa muda wa kujibu, linafuata na lingine na lingine!. Mimi sijasema mafisadi na wala rushwa wasishughulikiwe kikamilifu, nimesisitiza tuu, kuwepo fairness, respect, ustaarabu na sio kutegeana, kuumbuana na kuaibishana!. Wote walioangalia jinsi boss wa TRL alivyokuwa anahojiwa, kiukweli yule bosi amedhaaulika anaonekana ni li bosi lijinga ajabu!, limeshindwa kujibu simple questions kutoka kwa PM, wamekopa kwa idhini ya nani?!, baada ya tukio lile, kweli bosi kama huyu ana any respect left kwa wafanyakazi wake wa chini!, nahisi hata akipita, wananchungulia madirishani na kujisemea kimoyo moyo, angalia lijinga lile linapita!, ni huku tuu Afrika tunafanyiana mambo kama yale ile ni bullying of some kind!.

Paskali
dada Elitwege eti ni kweli hii👆
 
Pasco

Hayo ni maoni yako ni kwanini unataka uyalazimishe kwa WatanZania wote? Hayo ya utawala bora ni kulingana na tafsiri yako wewe na jinsi unavyoongoza familia nyumbani kwako usitake kutuletea kwenye nchi yetu, tumeshatoka huko, tumeshayafanya yote hayo ya kuitana faragha, kuundiana tume, kuonyana kwamba ninawajua wala rushwa msipojirekebisha mtakiona cha mtema kuni kote huko tumepita lkn matokeo yake ni kwamba makontena zaidi ya 2500 hayajalipiwa kodi, yaani yamekombolewa Bandarini bila kulipiwa sasa huu ni uhujumu Uchumi na kwa nchi nyingine adhabu yake ni sawa na Uhaini kwani unalinganishwa na uuwaji watu wote waliofia mapokezi kwa kukosa dawa hospitalini wameuliwa na hawa wezi!

Hivyo tuache na Magufuli wetu tumeshamkubali jinsi alivyo na vyovyote anavyofanya ana baraka zetu, na ndio maana ya kushinda Uchaguzi na kuwa Raisi vinginevyo basi kila mtu angejiongoza?
Habari Janeiro
 
Back
Top Bottom