Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Ni vigumu kuwa billionaire katika ulimwengu wa tatu bila kukwepa kulipa kodi. It is next to impossible. Haiwezekani mfanyabiashara kuanza na mtaji wa million moja na kutengeneza faida muda wote hadi kufikia level ya billionaire. HAIWEZEKANI. Haiwezekani mfanyabiashara 'mtakatifu' akawa billionaire. Hata kama atatengeneza super normal profit kiasi gani, haiwezekani kuwa billionaire.

Msingi wa ubillionaire ni kufanya biashara haramu, kutapeli, kupunja wateja kupita kiasi, ku monopolize soko, na zaidi ya yote KUKWEPA KULIPA KODI STAHIKI. Rostam Aziz ni billionaire kwa sababu alikuwa ameingia ubia na Ikulu...nani ni nani ni nani kwa sababu ya kukwepa kulipa kodi stahiki, kuuza unga, kutapeli, kupunja wateja, etc.

Leo Magufuli unaanza kuwabana, kuwachunguza wafanyabiashara? Kweli? Unataka wawe watakatifu? Si utawaua? Kwa mwendo huo utatengeneza hata billionaire mmoja katika ufalme wako kweli? Sio tutarajie wengi kupukutika? Yetu macho.
Ondoa neno haiwezekani, all things are possible to him that believe... Ni saa ya waaminio... Husikii magufuli akirudia msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Tazama tukiwa mabilionare bila rushwa. Kwanza mabilionare wengi hawaisaidii Tanzania kama hawalipi kodi, "aliye mwaminifu kwenye jambo dogo na kwa kubwa ni hivyo hivyo" kama hakulipa akiwa na milioni moja hatalipa akiwa na bilioni 100, ni bora kuwa na wafanyabiashara wadogo wengi wanaolipa kodi kuliko mabilionare wachache wasiolipa kodi... Simple truth. JPM is not interested of you becoming a billionaire but you paying taxes
 
Kaka viongozi na watumishi wengi walikuwa wamezoea kuwa Tanzania ni shamba la Bibi, sasa watakipata na hata kama ni mzazi wangu amekamatwa. Itakuwa fundisho kwenye familia, ukitaka kufumania hutatoa taarifa, ukitoa taarifa haukamati hata mtoto
 
Anavyofanya sawa sawa. Waache Headmaster (Magufuli) na Academic Master (Majaliwa) wetu wachape kazi.

Tena Bado Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Nendeni na huko. Majengo yote yale waliyojenga lazima Kuna Mafisadi wa majengo hatari.

Fanyeni kazi bila kumuangalia mtu usoni, iwe barabarani, ofisini au korokoroni.

Go Magufuli, Go Majaliwa. Tumbueni MAJIPU.

We are behind you, and we pray for you.

Acheni unafiki, au walioaibishwa ni ndugu zako? Walipojenga na kutumia fedha za kifisadi hawakuzionea haya. Wamefaidi sasa na heshima tuwalindie! No way, heshima wanajilindia wenyewe, wangetoka mapema kabla ya hatari. Waandishi wa Habari ni chombo cha dola pia, ndio maana, waziri anakuepo, chombo cha dolla na waandishi wa Habari bila siri. Asipoenda na waandishi wa Habari raisi atahakikishaje utendaji wake, atahakikishaje hajapewa rushwa kwa mlango wa nyuma, wananchi tutahakikishaje uwazi. Wezi wa barabarani mnawaanika hata utupu, mafumanizi mnayaanika lakini hawa wanaosababisha mauaji makubwa zaidi kuliko wote unataka tuwatunzie heshima! fikiri vizuri. Waziri hawezi ingia mahali tusimphotoe wakati anafanya kazi ya umma. Utakuta anamuuliza ofisa, je kuna upotevu wa makontena, anajibu hakuna, akitoa list anaulizwa unayajua haya anasema yah nayajua. Sasa kama anamzunguka boss wake macho makavu hivyo, anaaibishwa au anajiabisha mwenyewe!? Mimi sioni kosa kabisa hapa, msimlaumu, furahini... Ni tz ya JPM, tulipomchagua tulichagua job skills zake, imani yake, ujasiri wake na utashi wake, so tulia he is under Dr president JPM
 
mwendo wa kumagufulfly hata wangechapwa na viboko mbele za watu tumechoka na mafisad tumechoka sana...tulikuwa tumekata tamaa ila Mungu c ccm ametukumbuka wanyonge wa TZ.
 
Hahahaha! Naona ndicho anachotaka Pasco tuvune mabua kwa kuitana chemba kuulizana eti uliiba? Kisha tuundiane tume itakayotumia mabilioni hahahaha.

hakuna kuunda tume hapa kazi tu kila fisadi apate haki yake
 
Kwa uelewa na mtazamo wangu kw ujumla ninaona akina majaliwa wanafanya kazi nzuri tu kuudhihirishia umma kuwa kumekuwa na ufisadi wa kiwango kisichosemekana.mtu wa kawaida ambaye hata kupata sh.10000 kwa wiki kwake ni ndoto kimawazo lazima atatofautiana na mtu mwenye kipato au aliyeajiriwa.Kwa kifupi jamii nyoingi huwa wanadhani umasikini wa watanzania ni asili yetu lakini unapomshuhudisha kuwa tatzo la umasikini wako limechangiwa na fulani,basi hekima na subira na huruma ya huyu masikini inapotea.Kwa kifupi watanzania karibu wote wanafurahi sana kwa sababu wanahusianisha hali ya umasikni walio nao na tuhuma za ufisadi zinazobainishwa na rais na waziri.
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

Pasco

My Take:
Tuna tatizo kubwa la uelewa humu, ila pia kufuatia wengi kuchoshwa na kukinaishwa na rushwa na ufisadi, wamekata tamaa na kuhamaniko na mihemuko ya kuchukuliwa hatua kali sana na ikibidi hata wanyongwe!.

Nimenote wengi humu hawakunielewa!, japo nimeanza kwa utangulizi wa kuunga mkono hatua zozote zinazochukuliwa na awamu ya 5 kupiga vita rushwa na ufisadi, siungi mkono the means kwa kutumia populistic approach ya kufanya ili watu waone unafanya!.

Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa haki wa Uingereza, wa presumed innocent until proven guilt beyond reasonable doubt by the court of competant juisdiction!, kinachofanyia ni media trial kumuonyesha mtu ni mkosaji mbele ya camera!.

Sio wengi humu wanaojua kuwa hata mhalifu anahaki!, hata mlaushwa, fisadi, mwizi, pia ana haki!. Hata muuaji aliyehukumiwa kifo kwa kunyongwa naye pia ana haki zake, ananyongwa kwa heshima yake, na kabla hajanyongwa, anaitwa daktari kumpima afya yake, akikutwa na maadhi yoyote, hanyongwi!, bali anatibiwa mpaka apone ndipo adhabu hiyo itekelezwe!.

Japo kisheria hairuhusiwi kamera za waandishi kuingizwa mahakamani, Tanzania tunaingiza kamera mahakamani!, polisi nao wanawaparade wahalifu
kwa waandishi wa habari ili hali wako mikononi mwa polisi!, ni kama kuwahukumu kabla!. Kama Kova kila uchao, kwenye screen!, hilo baraza jipya likiishateuliwa, kama kila waziri nae atatembea na media team ili watu waone si itakuwa chaos?!.

Nilichokiona jana anachokifanya PM pia kinakwenda against the principles of Natural Justice
Vita dhidi ya uzembe, rushwa, ufisadi, na ukwepaji kodi yes!, means no!, haki sio tuu itendeke bali pia ionekane kutendeka!.

Pasco
Update.

Mkuu Kiranga, sio kila kitu ni sheria, vingine ni taratibu tuu na kanuni!, ndio maana kwenye ofisi za kizamani kuna vyumba vnawatenganisha ma bosi na wafanyakazi wao!, kuna chumba kinamtenganisha waziri na secretary wake, kuna ofisi ya boss, lengo ya yote hayo ni kuweka heshima na privacy!, nimefanya kazi na wazungu fulani nchini Uswiss, wenzetu wako kwenye full open government initiative, no secrets zozote ofisini, partition zote ni za kioo transparent, computers zote ziko linked kwenye network, desktop zote ni shared, ukipint chochote kuna back copy iko saved, all public communications ni shared.

Huwezi kumrepremand boss infront of his subordinates let alone infront of the media, mtu anaulizwa swali, hajapewa muda wa kujibu, linafuata na lingine na lingine!. Mimi sijasema mafisadi na wala rushwa wasishughulikiwe kikamilifu, nimesisitiza tuu, kuwepo fairness, respect, ustaarabu na sio kutegeana, kuumbuana na kuaibishana!. Wote walioangalia jinsi boss wa TRL alivyokuwa anahojiwa, kiukweli yule bosi amedhaaulika anaonekana ni li bosi lijinga ajabu!, limeshindwa kujibu simple questions kutoka kwa PM, wamekopa kwa idhini ya nani?!, baada ya tukio lile, kweli bosi kama huyu ana any respect left kwa wafanyakazi wake wa chini!, nahisi hata akipita, wananchungulia madirishani na kujisemea kimoyo moyo, angalia lijinga lile linapita!, ni huku tuu Afrika tunafanyiana mambo kama yale ile ni bullying of some kind!.

Pasco

Haki zingine upuuzi
 
Ulitaka afanyeje? Au wewe pia umeguswa?
 
Nchi haiwezi kuendeshwa kama unavyomuendesha mkeo, mkeo ulimpata baada ya kumpenda, kwa hiyo wewe na yeye mnapendana sana, katika elimu ya uongozi, weledi na uaminifu wa matumizi ya Mali ulizokabidhiwa ni muhimu kuliko sympathy (mapenzi), usichanganye vitu "you grown up".
 
Hamna good govenance wala nn. Kwa nchi kama zetu hizi hivi ndivyo inapaswa viongozi wafanye sio tunaigaiga tu mambo toka nje. Wenzetu wamepitia stage kama nne au tano katika history. Sasa cc tunaburuzwa tu na tunakubali kila mfumo unaowekwa hapana acha Kassim Majaliwa afanye mambo yake.
 
majaliwa anafanya kwa kukomoa.
Wacha inafiki wewe mtoto.
Angekuwa anaitwa Warioba au Joseph usingesema haya.

Wacha Waziri afanye kazi yake.
Na wewe endelea kuuza hizo leso kwenye traffic lights hapo tazara.
 
Pasco naamini uko sawa kabisa ila,kama kiongozi wa sehemu husika na huna jibu kuhusu utendaji wa sehemu yako maana yake hufanyi kazi sawia ni mtu wakutegemea ripoti na katika uongozi kwa bara letu hili ambapo tunaamini uongo ni moja ya sehemu ya uwajibikaji bora ni hatari sana kwa kiongozi kutegemea ripoti ya kuletewa,hata mimi nikienda kwa mjumbe wa nyumba 10 nikamuuliza mtaani kwako kuna wageni wangapi kwa mwezi huu na asijue ni mzembe wa hali ya juu!
 
Wacha inafiki wewe mtoto.
Angekuwa anaitwa Warioba au Joseph usingesema haya.

Wacha Waziri afanye kazi yake.
Na wewe endelea kuuza hizo leso kwenye traffic lights hapo tazara.
Yani ww unawaza kdini tu..
 
Wacha inafiki wewe mtoto.
Angekuwa anaitwa Warioba au Joseph usingesema haya.

Wacha Waziri afanye kazi yake.
Na wewe endelea kuuza hizo leso kwenye traffic lights hapo tazara.
Ipo siku utajua kuwa Kassim Majaliwa si muislam kama unavyodhani.
 
Back
Top Bottom