Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Kama Waziri Mkuu kakosea, ashitakiwe.
Tuambiwe kavunja sheria ipi, apelekwe mahakamani, walioonewa waje hapa kutoa data zao, kama hawana fedha za kuendesha kesi tutawasaidia.
Sio mtu analaumu "mtindo" bila kuongelea sheria.
Mimi nilivyo m blast rais Magufuli kuingilia tafrija ya bunge, niliongelea "checks and balances" za kutoka katika katiba.
Pasco anapom critique PM, atupe msingi wa kisheria.
Kama hana msingi wa kisheria, asimlaumu PM. Ampigie simu mbunge wake sheria ibadilishwe.
Kukosea siyo lazima mtu avunje sheria.
Unaweza ukafanya jambo ambalo si kosa kisheria lakini likawa si la busara.
And just because one can, doesn't mean they should.
Kuna sehemu niliona umezungumzia tact. Hilo neno halipo kwenye msamiati wa Magufuli wala Majaliwa.
Hebu ona siku waziri mkuu alivyoenda hapo bandarini mara ya kwanza.
Hapo kwenye 0.33 mark anamwamuru IGP amkamate Bw. Masamaki...."IGP kamata huyu, ashiriki kwenye uchunguzi huu".
Hivi kweli hiyo unaona kuwa ni sawa?
Au watu tushakata tamaa kabisa na kufikia sehemu hatujali tena mambo ya tact ili mradi tunaona kuna kitu kinafanyika, hata kama hakina matokeo yoyote ya maana?
Last edited by a moderator: