Samiah anapaswa kusafiri safari zote ambazo JPM haendi
tutakosa hata mikutano ya muhimu kwa kuendekeza kuchukia safari...
na mwisho tutazidi kuwa taifa la kienyeji..kama one big village
mara amri ya kufanya usafi mara hivi mara vile...as if hakuna nchi zingine tunazoweza jifunza
hakitaweza kitaongeza tatizo
watu watafanya kazi kwa fear na kutojiamini
bureaucracy itazidi sababu kila mtu atataka kuwa safe side..
kujipendekeza na kuwa infomer ndo kutageuka dili...
na hata ku pretend kufanya kazi kuliko kufanya kazi kutaongezeka..
na culture ya kukaa kimya na kutohoji maamuzi na amri kutoka juu itaongezeka
Wewe ni mbeba maboksi au mganga wa kienyeji!?
Unasema watu wata pretend?...hizi kazi zetu kuna kitu tunaita target. Wala target haina usanii wa kusema nita pretend.
Kwa mfano ikitokea serikali inataka makusanyo kutoka bandarini pekee yawe trillion 7 kwa mwaka wa fedha 2016/2017....na iwe hivyo...sasa hapo kuna kuna ku-pretend sijui unafanya kazi au hufanyi? Sisi tuna-deal na results tu. Kama hiyo figure haijafikiwa kutokana na rushwa au bandari kukosa ufanisi...basi tunaingia site kwa kushtukiza na kuanza timua timua. Mbona watanyooka tu.
Ndio maana tunasema chuki zako hizo hazisaidii kitu. Zaidi yakuonekana na wewe ulikuwa sehemu ya wale waliokuwa wakifaidi mfumo mbovu.
Wanabodi,
Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, sio!.
Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomngoa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.
Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.
Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.
Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.
Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.
Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.
Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco
Halafu, hao wote si walikuwa kwenye serikali iliyopita?
Manake wanachofanya sasa ni kama kuivua nguo hiyo serikali.
Ina maana walikuwa wanatumikia serikali iliyokuwa imefeli?
mkuu umenifanya nicheke... maana siamini kama uliwaza kabla hujaandika.. kwani wote waliokuwa wakipita kwenye kampeni kutaka uongozi ni wangapi hawakuwahi kuwa kwenye system?? kumbe lowasa angeweza na angekuwa sahihi ila si magufuli na majaliwa
Wengine tulihoji kuhusu hilo suala la bunge.
Tukaambiwa eti rais naye ni sehemu ya bunge na ndo maana hulivunja na kulifungua.
Na kwamba eti ile tafrija iliandaliwa na ofisi ya rais na si bunge.
Hii awamu ya tano imeingia na staili ya aina yake kweli.
Ngabu iko very clear hawana 'blue print' ya nini wafanye
kubadili hii nchi iondokane na kero
so wanashiriki ku expose kero na kukaripia on tv
lakini 'what to do to change things permanently' ndio hawajui...
'the blue print' ya ku replace hii failed system hawana
Mkuu The Boss na Nyani Ngabu, heshima kwenu.
Hamuoni kuwa mnamlalia Magufuli kwa uonevu kweli?
Msukuma wa watu hata mwezi hajamaliza ofisini mnamshutumu kuwa hana mkakati wa long-term. Tusitegemee miujiza toka kwake jamani. I mean, even if the guy is a born-again Christian BUT he doesn't walk on water, nor turn water into wine.
Tumpe muda jamani, isipokuwa huu udhalilishaji hadharani apunguze.