Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Wewe jamaa ni mjinga kweli kweli aise. Alafu nakumbuka wakati wa kampeni ulikua team LOWASSA so ulichokiandika hapa ni muendekezo wa wa ukanjanja wako.
By the way, kama unaona si sawa hama nchi tu sasa maana hakuna namna.
Go Magufuli go, ulipo tupo.
 
Last edited by a moderator:
kwa jinsi hii hawa maofisa wa mashirika ya umma walivokubuhu kwa wizi na ubadhirifu, acha wadhalilishwe tu maana wao wangekuwa waumini wa good governance wasingefisadi nchi.
 
"Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!."

hizi zote ni ishu za miaka mingi hawa maofisa wanazifahamu vema, nakubali mh. Majaliwa anajidhalilisha kwa kuwafuata
hawa watu kwani uhujumu uchumi wao upo wazi, angewatumia hata sms waachie ofisi.

huwezi cheka na ngedere shambani.
 
Umejitwisha hekima isiyo na chembe ya ubinadamu. Kuna watu mirija yao inakatwa wanabaki kupiga kelele tu hahahaha kufeni tuzike
 
Good governance my foot. Ukubaliane nae au uwe on the other side, does it really matter?
Kila mtu ana style yake ya kuongoza, so long anafuata sheria. Anawadhalilisha TRA, TPA na TRL kwa sababu walijidhalilisha kabla ya yeye kwenda, unategemea yeye afanye nini?
TRA & TPA ndio moyo wa nchi, asipotengeneza hilo eneo, hakuna viwanda, elimu bure, maendeleo n.k so let them be.
Tangu bajet ya 2015/16 itengwe, hakuna shughuli yoyote ya maendeleo ilofanyika, ni kampeni na uchaguzi tu. Ngoja waddle roadmap yao, wafuate roadmap yao na kufanya kazi. Of course tutacriticize kama kawaida, but let it be constructive criticism...
 
Hata mi sipendi. Sidhan ka vyombo vya habari visingekuwepo angefanya vile. Ndo mana kuna siku bunge lilitaka liwe recorded.
Watanzania ni watu wa hovyo kabisa good governance ndiyo imetufikisha nchi kufirisika , hakuna utawala bora kwa wezi na mafisadi,njia ya kwenda ofisini na kuuliza ndio mwanzo wa rushwa , Nani hajui hawa wakuu wa hayo mtaasisi ni wezi. Njia ya kutumbua jipu haina ustaharabu , ni kutumbua tu
 

Pasco anaogopa madudu aliyokuwa anafanya kupata tenda za 77 na 88 za kutangaza matangazo yote ya serikali,anahisi majaliwa/magufuli wakija pande Hizo lazima alambishwe mchanga.
 

sometime nahisi wanatoa system walio ikuta ili waweke yao in a style na upigaji uendeleee sababu wangezuia yasiwe yanatoka wanagundua magonjwa hawayapi dawa
 
Inaonyesha pasco alikuwa mnufaikaji wa good governance.
Hakuna cha kuitana pembeni, huko pembeni ndio hupigana sound alafu wanaishia kupeana hongo. Good governance my foot, fukuza wote wabadhirifu.
 
kwa nchi ilipofikia acha tu wadhalilike
 
Pasco "UTAISOMA NAMBA"kama wewe ni msafi una wasiwasi gani?
Najua wewe ni miongoni mwa wale wachache mnaokula pesa za serikali.
 
Namna ilikuwepo: kujiuzulu.

Tatizo hatuna huo utamaduni.

Sina nia ya kukupinga mkuu wangu lakini wale wote walioonesha nia ya kusimamia haki kinachowapata baada ya hapo sote tunajua,uoga na wasiwasi kibinadamu hivi vipo kwa watu wote.

Ni muhimu tuangalie athari zinazopatikana kutokana na wizi huu na heshima tunayotaka wapewe viongozi walioshindwa kuwajibika katika nafasi zao.Kupanga ni kuchagua.
 
Pasco anachokifanya ni sahihi. Pasco mmeiba mno. Hapa kuna mmoja alikuwa na tambo zote za utajiri kumbe mumewe ni kogogo wa uwizi tra. Pasco najuwa u mpambe wa mwana wa mfalme sasa mmekwisha.

Nchi haikusanyi kodi. Shilingi inaporomoka kisa ni nyie Pasco, mbona hauna huruma. Mbona hauna aibu.

Waache wafanye kazi. Ukisingiziwa nenda kapate haki mahakamani.
 
Last edited by a moderator:

The Boss umeshakiri kuwa nchi nyingine sio yetu. nchi nyengine hazihitaji hata monitoring na sheria zipo kama ishara tu kwasababu wananchi wa huko wanajitambua. pima kwenye mambo madogo tu suala la usafi kwa mtu mwenye akili timamu haihitaji hata balozi akuelekeze namna ya kufanya usafi sababu ni kwa faida yako sio kiongozi lakini tumeshindwa kabisa!!! ni watanzania wachache wanaoweza kujisimamia wao wenyewe na shughuli ikawa kama ilivyokusudiwa. hadi tusukumwe tutishiane ndo mambo yanaenda ukisema mpelekane kistaarabu utafukuza nchi nzima hii. tuna disappoint sana kwa kweli. wakoloni wasingeweza kutu manage bila viboko
 
Last edited by a moderator:
Hii ni MBWA style management hii inatumika hasa kwa watumishi wazembe ambao bila kusimamiwa hayaendi, waongowaongo, serikali ya magufuri inataka kuwaonyesha wananchi kuwa tatizo siyo ikulu bali na watu huku chini wanaokwamisha serikali kufanya mambo yake.


 
Hakuna namna kwa unapopewa uongozi ukakuta "rotten system"!
Issue ni je hizo tuhuma wanazopewa kuna ambayo imekosa validity? otherwise kwa tulipofika we all need to say..go go go PM ..mwanzo mzuri just keep on setting stage for your five years term!
 
Majaliwa piga kazi sisi tunapiga maombi usiyasikilize haya majungu ndo maana tulitaka viongoz wasio na doa ili wasiwe na aibu ya kukemea rushwa hadharani hatutaki watu wenye ndimi mbili hapa mtu anasema anaunga mkono kisha anadai ni uzalilishaji unafanywa iv kweli huyu pasco ni kilaza kweli kweli
 
Waziri Mkuu Majaliwa aendelee hivyo hivyo na hao wafanya kazi wachapww hata viboko.

Mtoa mada siajabu ni mmoja wa hao watu waliokuwa wanafaidika na uzembe uliokithiri, wizi, udanganyifu, na hata kutofanya kazi kabisa huku wanalipwa mishahara.Asiyeweza spidi ya HapaKaziTu ajiuzulu kazi ya umma na akajifanyie kazi nyumbani kama apendavyo.
 
Go go go go again Dr. Magufuli.
Jihakikishie kura 90 percent uchaguzi ujao ili wale madogo wasiibe tena kura. Acha na akina Pasco.
 
Last edited by a moderator:
Hata mi sipendi. Sidhan ka vyombo vya habari visingekuwepo angefanya vile. Ndo mana kuna siku bunge lilitaka liwe recorded.

Hii vita ni kubwa sana kuna watu kama nyie mmeongwa kuja kupunguza kasi na kulaumu tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…