Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Nafikiri taasisi ya Urais ni kubwa kuliko nyingine linapokuja suala la uongozi kwenye nchi inayofuata mfumo wa kirais...
Tuna mifano kadhaa ya Marais/Watendaji wengine wakuu ambao wameshindwa kwenye uongozi wao kwa kuchekea chekea wahalifu...sioni kwanini kuwepo tena na donge pale anapoingia mtu asiyemung'unya mambo anapotumia rungu kutokomeza ubadhirifu.
 
Pasco wewe ni mjinga sana wambie waliokutuma Hatudanganyiki Mambo yawe wazi acha upopoma kabisa...
 
Wahalifu wengi hujificha nyuma ya good governance. Nidhamu ya utumishi irejee kwanza, good governance baadaye. Mwizi anadhalilika?
 
Yaani unataka Waziri Mkuu aige utawala WAko na mkeo nyumbani❔
 
Yupo sawa, akisema awaite pembeni watamlaghai na kuomba asamehewe na km ni kugogo mazingira ya rushwa yatazidi kujengwa.
 
Hivi Pasco sio wewe uliye mshauri Rais Magufuli afute utawala wa kisheria aongoze kwa Presidential decrees ??

Nadhani hapa anazungumziwa Kassim Majaliwa ambaye si Rais wa Tanzania.

Leave Makofuli alone!!
 
Last edited by a moderator:
Bossman, talking of success stories...man...!
Huwezi kuongelea success stories overnight. Hilo halipo na haliwezi kuwepo, success stories have sad stories behind them, lazima kuumia na pengine kutoa damu ili kuimba 'nyimbo za haleluya'.
Tatizo wengi wetu tunapenda "easy and quick fix", PM aende bandari, atoe list ya wahujumu uchumi na wezi, wafungwe na maisha yaendelee tena tupate hizo "success stories". Hilo halipo na haliwezi tokea. Hata uchina, marekani, ujerumani nk walipitia huku mnakoita "kudhalilishana" hadi leo mnawaona superpowers. Soma history za Hitler & co. Utagundua mengi kabla ya kuimba "stories of success"
I applaud PM's approach, iwe ya kidikteta ama ya kudhalilisha, na anatuma ujumbe kwa jamii yenye virusi vya wizi, ubadhirifu, hujuma, uvivu na uzembe...that it's no longer a rollercoaster...
 
Tuwape nafasi viongozi wetu wafanye kazi na zaidi tuwaunge mkono, inchi ilishaharibika hii.
 
Pasco,

Acha Majaliwa na Dr.Magufuli wafanye hivyo hayo mambo ya good governance!Mkapa na Sumaye, Jk na Pinda wameyafanya sana hayakuwa na impact yeyote.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kuleana tena, nchi hii ni ya watanzania wote na haiwezekani wachache kuendelea kuiibia nchi kwa manufaaa yao binafsi. Binafsi nafarijika kuona Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa akifanya kazi yake kwa uhuru. Zamani "business as usual" sasa basi.
 
Hacha umandazi wewe kipindi wanapiga hizo dili walikuwa awalidhalilishi taifa??kuna watu wamekufa kwa kukosa dawa hospitalini eti nchi haina hela ya kununua dawa kumbe hela zote zipo kwa hao wapiga dili.ndio muda wao kudhalilishwa dunia ijue wezi walio lighalimu taifa hill.
 
Ni mparaganyiko kwa kweda mbele.Ila watu tukisema tunaonekana kana kwamba hatumpendi Magufuli wakati suala si kumpenda wala kumchukia.
Huu sio muda wa kupendwa na mijitu minafki kama nyie, mpende msipende haituhusu tunataka hivihivi, mgekuwa watu wenye kujielewa na kujitambua mgepinga majizi kuwa malaika ktk li chama lenu
 
Ukweli ni kwamba hata yeye PM akishtukizwa sasa ivi na kuhojiwa mambo ya huko Tamisemi alikokuwa hatakuwa na majibu sahihi. Kuwa mkuu haimaanishi umekariri data zote za ofisini. Pia ktk ofisi kuna vitengo tofauti kwaiyo ni vema akiwa anahoji awaite wahusika kutoka kila kitengo badala ya kumuandama boss tu maana mambo mengne hufanyika kwa niaba ya.
 
Huu sio muda wa kupendwa na mijitu minafki kama nyie, mpende msipende haituhusu tunataka hivihivi, mgekuwa watu wenye kujielewa na kujitambua mgepinga majizi kuwa malaika ktk li chama lenu

Umejamba mara ngapi leo?
 

Mwambie hajielewi huyo. Sina shaka huyo jamaaa anaslahi binafsi na hao wezi. Hatutarudi nyuma, tumechoka!
 
Nimeusikiliza kwa makini mziki huu wa Magufuli na Majaliwa na nimegundua kuwa Pinda asingeuweza hata kidogo. Huu mziki ni original tena ni wa asili ya kitanzania. Hebu angalia namba ya makontena yanayopita bandari moja tu ya Dar. Bila kulipiwa kodi, sasa kwa nchi nzima mambo ya TRA yakoje?
 

Mwaka huu wewe FISADI UTAKOMA NA BADO RUDISHA PESA ZETU. MWIZI WEWE.
 
Pasco ana Tania jamani
Hayuko seriously, msomeni kwa makini!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…