Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

ngozi nyeusi haiendi bila kuburuzwa au kusukumwa, hayo unayotaka ndo aliyofanya JK lakini mwisho wa siku akawa amecheka na nyani
 
Kuna video clip moja ya Putin anawavamia jamaa sijui wa kiwanda gani kile kisha kamshurutisha jamaa asaini contract. Jamaa kasaini kiunyonge sana alipomaliza kusaini akaondoka na pen. Mara Putin akamuita akamwambia nirejeshee pen yangu. JK aliacha mambo yaende yanavyokwenda. Sasa ni ngumu Magu yuko UKAWA
 
huwa wanajionaga miungu watu.....ikibidi Waziri mkuu awachape Viboko
 
Hii nchi inabidi kuendeshwa hivi kibabe babe mpaka kila mtu arudi kwenye mstari. Mambo ya kuunda Tume, tunafuatilia, tuko kwenye mchakato, hii ni changamoto.....ZAMA ZAKE ZIMEPITA.

Na bado. Subirini watu watakapoanza kwenda jela sasa.
 
Mparaganyiko mkubwa
kaenda kwanza kagundua makontena 300
karudi tena kagundua mengine zaidi ya 2000

so inawezekana yakafika hata elfu 10 hajagundua bado
na hakuna namna ya kugundua hadi waziri mkuu aende mwenyewe..
ni kama system ime fail kabisa....waziri mkuu anafanya ukaguzi wa kontena
sio kujenga system mpya yasitokee haya tena

Sasa utajengaje system mpya ili yasitokee kama kwanza hujachunguza mbinu iliyokua inatumika? Hukuona waziri mkuu kaagiza system ya billing isitumike na baada ya wiki watafute wataalamu wa kufufua technologia waliyoikacha?
 
wanabodi,

kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na waziri mkuu, wetu, mhe. Majaliwa, kasim majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha tra kilichomngoa kamishna mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini, na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huki akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo kaatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata tra siku hiyo alikwenda na nondo za makomtena, alipomuuliza bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda trl na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 tib za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, mkuugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya waziri mkuu, wetu, mhe. Majaliwa, kasim majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, leo nimemuona magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na waziri mkuu, wetu, mhe. Majaliwa, kasim majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, sio sawa, sio haki, sio good governance!, ni udhalilishaji na kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.
Pasco


we pumba kabisa unakanyaga mafuta kama mashine ya kusaga huku huko rivasiii...............ANDIKA VIZURI NIKUNUNULIE KAKOKA BWANA MDOGO.
 
Yupo sahihi kabisa,na huwezi kwenda mahali kukagua wakati huna data kamili, kama tume zilishaundwa sana na kama faragha watu walishakaa sana inatosha kwa kweli, Wacha tu waisome namba wenyewe ndicho tulichokuwa tunakililia.
 
Pasco ana hasira; maana PPR yake ina kila dalili za kuto-shine katika Awamu hii ya Mh. Magufuli. The Boss ana hasira; maana watu wake, Rished Bade na Harry Kitillya wametuhumiwa kwa ufisadi.
 
Tunashukuru brother Pasco kwa mtazamo wako.

Ila kwangu mimi naona alicho kifanya waziri mkuu ni sahihi kabisa.
Kwanza, ametufanya kujua angalau kwa kiasi fulani uwezo wa viongozi wetu kwenye hayo mashirika ya serikali. Kiongozi unaulizwa kuhusu taarifa muhimu zinazo husu shirika lako, una babaika kama vile ume anza kazi jana. Alipofanya kwa TRA, haya mashirika mengine yote yalitakiwa yakae mkao wa kula. Kama kuna taarifa mbaya uzijue, na mipango na njia za utatuzi wake pia uuweke wazi na nzuri pia uzijue na uweze kuziuza.

Pili, PM anatembea na taarifa/ripoti akiwa anajua tabia zetu za uongo zilizo kithiri, ndio maana ana amua kutuumbua hadharani. Nimependa pia hiyo style yake ya kutembea na hizo taarifa, maana inatupa mwanga na sisi wananchi wapenda mabadiliko. Hizihizi taarifa zake ndio zitatupa nafasi ya kuhoji siku tutakapo ona hakuna chochote kilicho fanyiwa kazi na hata kupelekea kushinikiza aondolewe/ajiuzulu kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.

Watanzania tumekua tukilalamikia mambo mengi mabaya ambayo yanafanyika hapa kwetu na hata kufananisha hatua ambazo zinachukuliwa na nchi za wenzetu katika kukomesha mabaya hayo. Ikiwemo kuua/kunyonga kama wanavyo fanya China. Hebu na sisi tuwape nafasi hawa viongozi wetu wafanye kwa staili ambayo wataona wao inafaa katika kuondoa uozo ulio kithiri. Makosa katika utekelezaji yapo, kwani wao sio Malaika na wafanye mambo ambayo yatampendeza kila mtu kwa wakati mmoja. Ila kuna kukosea kuzuri...
 
hahahaaa...ulitaka iundwe kamati?? skuizi hamna kamati ukivuruga unakula za uso live live...viva magufuli
 
Mkuu Pasco,

Kwa misingi ya utawala bora ni kuwa kila mtu awajibike kwa ufanisi katika nafasi yake. Kilichoonekana jana kutoka kwa Meneja wa Bandari na Mkurugenzi wa TRL ni kuwa uwajibikaji wao (accountability) ina walakini. Iweje PM aje na taarifa (siri sirini) akuulize kitu kilicho chini ya utendaji wako (mf. huyo Mkurugenzi wa TRL kukopa fedha kwa malengo ya uendelezaji wa shirika, wao wakaamua kulipana mishahara!!!) then ukose majibu ya msingi!!!

Ndiyo inaweza kutafsiriwa kama ni udhalilishaji lakini kwa tabia za watendaji wa ki-Tanzania zilizopo sasa ngoja Mwalimu wa Nidhamu amsaidie Mwalimu Mkuu kufanya ukaguzi wa kucha na nywele. Atakapoteuliwa mwalimu wa uraia (utawala bora) basi akute kuna usafi na aanzie hapo kufuatilia misingi ya utawala bora. Kwa sasa ngoja wasafishe mazingira. Na wasipokuwa makini wataaibika sana. Namuona na Eng. Felchesim (sijui kama niko sahihi 100% katika kuliandika jina la huyu bwana) Mramba wa Tanesco naye ajiandae. Ataaibika.
 
Kwa wale mnaokumbuka vizuri utawala uliopita ulifanya juhudi kumfinya magufuri asionekane kwenye macho ya wengi kama mtu makini,huyu mzee sasa analipiza kisasi,ni raisi mpinzani wa ccm kutoka ccm,ccm washukuru bado si mwenyekiti,anaitumia tiss kupata taarifa ili kuumbua watu lakin anasahau tiss ina wanafiki na kuna muda iligawanyika,tiss kuna wapiga dili ambao wana uchungu na kukosa utawala uliopita,WATANZANIA MNAPENDA KUSHABIKIA UJINGA BILA KUFIKIRI NDO MAANA ZIARA YA MUHIMBILI HAINA TIJA ZAIDI YA KUFUNIKA UDHAIFU WA MATAMKO HEWA KWA VITANDA,NAMUUNGA MKONO MAGUFURI ILA HAPA KAZI TU BILA SERA NI UPUUZI,HAKUNA MWONGOZO NDO MAANA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WANAFANYA KAZI KUMFURAHSHA MKUU BADALA YA WANANCHI,KWAMWE HATUTOPATA LONG TERM SOLUTIONS KWA UTENDAJI HUU BALI ITAKUWA KILA MTU ANAFANYA YAKE SIKU IPITE
 
Huo ustaarabu ndo umetufikisha apa naweza Elewa container 2000 jamani bado mnataka awe mstaarabu jamani watz tumelogwa.
Akifanya kazi yako kwa weledi hawezi kuja
 
kama ingewezekana majaliwa uwe unawazaba na vibao hao wezi wametuibia mno mpaka mama zetu wanajifungulia chini hakuna muda wa kukaa nao mezan wakat detail zinaonyesha waz wameiba
 
Wahanga wa majipu wamejaa kwenye hii thread!!!

Hii style ndio nzuri! Aendelee tu kuwastukiza
 
Uwezo wa wafanyakazi wa serikali in ICT ni mdogo sana. Lazima tunaibiwa sana kwa jina la ICT. Lazima tunauziwa programs ambazo ni substandard, mara nyingi kwa kutokujua ni program gani tunataka. Na kwa jinsi tulivyozoea ujanja ujanja na udanganyifu, lazima ICT inatumika sana kuwezesha ukwepaji wa kodi. Kabla ya kuendelea kushangilia ICT kwenye mifumo ya ukusanyaji mapato ya serikali, forensic auditing inahitajika kwa mifumo ambayo inatumika tayari.

Cha kushangaza, eneo ambalo hajafika au sijasikia kama amefika pale bandarini ni la kupokea mafuta. Kuna ujinga mkubwa sana uliofanyika kwa miaka mingi wa ku-temper na vifaa vya kupimia shehena ya mafuta inayoingia nchini "flow meters". Bila "flow meters" inayofanya kazi na ambayo haijachakachuliwa, serikali haiwezi kujua kiwango sahihi cha kodi inachostahili.


Sasa mkuu kama ambaye unampa Tender ya kukuuzia Program ndiye yule yule ambaye anapitisha makontena yake hapo bandarini kila wiki unategemea nini?? Alafu unaletewa IT Manager ambaye hata haujashiriki kwenye hatua yeyote ya utengenezaji wa hiyo program, kazi yako ni kuirun tu basi.. Hujui weaknesses zake, na ndio hapo tunakopigwa..

Hata huko kwenye mafuta, jamaa wa weights and measures anayekula hiyo Tender kila mwaka ni muhindi mmoja ambaye nae pia ana ubia na waingizaji wa mafuta nchini.. Hii nchi imeoza kila mahali, na hizi Tender za kupeana peana kwa kujuana ndiyo kumetufikisha hapa..
 
Mkuu Pasco nakubaliana na maoni yako lakini yote kwa yote protocol ziwekwe kando hawa maCEO walijahau sana muda wa kuwakimbiza mchaka mchaka ndio umewadia hakuna cha nini wala nini kama PM ana nondo za ofisi yako wewe huna unataka upakwe poda taifa limeachwa nyuma sana kwasababu ya visheria,kanuni na taratibu mbovu zilizopitwa na wakati.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom