Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Anachofanya Waziri Mkuu sio sawa, sio haki, sio Good Governance! Ni udhalilishaji na kuaibishana!

Pasco Leo Sijui Umekunywa Nini? Kwa Hiyo Ulitaka Mh Waziri Wetu Mkuu Mpendwa Ndugu Kassim Majaliwa Aache Kurudisha Heshima Mahala Pa Kazi, Tunahitaji Viongozi Kama Hawa Kuleta Nidhamu Mahala Pa Kazi

Naona kanywa supu ya maharage huyu pasco. Kiongozi unafanya ufisadi halafu unataka good governance ipi? Ufisadi na wizi no good governance?
 
Mkuu Pasco Labda tungeanzia hapa "What is Good Governance?"
Wewe peke yako ndiye umeweza kujenga hoja dhidi ya hoja ya Pasco. Maana kuna watu wamemrukia Pasco bila hata ya kujua nini kinaongelewa. Hakuna mtu anayependa kulea uovu lakini lazima kuwe na mfumo endelevu na unaojitegemea unaoweza kupambana na uovu bila ya kuwepo kwa uonevu!!
 
Watanzania wa ajabu!! Mtu unaibia na kajitokeza Mtu anakusaidia kumkamata mwizi baadae unaanza kumtuhumu namna alivyomkamata sio!! Kwataarifa yako staili iliyobaki ya kuwakamata ni hiyo hiyo--zingine zote zilifail. Kama huna cha kuandika kwa kimya acha johnpombemagufuli na Majaliwa wapige kazi na sisi tuliowengi tunawaunga mkono
 
Last edited by a moderator:
Naipenda hii kasi ya magufuli lakini naona kwenye management kidogo something is lacking. sio kazi ya majaliwa kukagua makontena. Fix the system ifanye kazi yenyewe hata ukiwa umelala nyumban!!!
Huwezi fix system kwa mwezi mmoja,especially system iliyojengwa for 50 years,so kipindi hiki ambacho system mpya itakuwa inajengwa,wacha njia za muda mfupi zenge kuleta results zitumike.Theory ya hili ni sawa na theory ya uchumi tu,kukiwa na mdororo wa kiunchumi Solution ni kujenga msingi imara wa kuimarisha uchumi kwa muda mrefu,lakini hilo sio jambo la overnight,so wakati unajenga msingi huo imara ndipo utakuta kuna njia za muda mfupi lakini very effective ktk kuuokoa uchumi zinatumika mfano kutoa `Economic Stimulus'
 
kwani kwenye jamii yetu hakuna jinsi ya kushghulika na wabakaji?? Hii tabia ya majaaliwa mnayoipogeza ni dalili kwamba nchi inaendeshwa kiporini porini!!

Nchi hii ilishakuwa ya "kiporini porini" kwahiyo inabidi iendeshwe hivyo hivyo kiporini porini!

Cha msingi Majaliwa aongeze spidi kutoka hii 60 aliyoanza nayo mpaka 120. Halafu Magafuli akanyagie spidi 180 kabisa.
 
Sasa mkurugenzi mzima hajui nani akiwaruhusu wakope benki!?
Mkurugenzi ajui sababu za Ku kupindisha pesa za miradi kulipa mishahara!!?
What type of mkurugenzi is that?
 
Pasco, nitakushangaa sana kama utakuwa na mawazo ya namna hiyo. Watu waliopewa kazi ya UMMA na kuaminiwa na serikali wanafanya mambo ya ajabu namna hiyo, waheshimiwa kwa lipi. Mimi nilitamani sana wangeshikiriwa na polisi na kuwekwa ndani wakati tuhuma dhidi yao zinafanyiwa kazi. Jiheshimu hueshimiwe inabidi hiwe hivyo
 
waambie hao Mwalimu Nyerere aliyeamulu wapigwe mboka 24 kwani alikuwa hajui kuwepo kwa haki za binadamu? watu wanafilisi uchumi wa Nchi halafu mnataka waonewe huruma badala ya kuonea huruma wagonjwa waliopo mahospitalini wanaopata shida kutokana na vitendo vya ufisadi vya wachache.
 
wanabodi,

kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na waziri mkuu, wetu, mhe. Majaliwa, kassim majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha tra kilichomng'oa kamishna mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa rais!.

Hata tra siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda trl na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 tib za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya waziri mkuu, wetu, mhe. Majaliwa, kasim majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, leo nimemuona magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na waziri mkuu, wetu, mhe. Majaliwa, kasim majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, sio sawa, sio haki, sio good governance!, ni udhalilishaji na kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

Pasco
hahaa msemaji wa mstaafu polen sana njoon na kirma yenu hapakazi pasco polen kama nondo limewashukia lakini amkujiandaa.mapema tangu anachaguliwa wengine.waliomba kustaafu mapema na leo wala awaguswi.mlijua.mzee.wa.mtwara anakujakamata.nchi.nn..
 
Wanabodi,

Kwanza naomba kukiri, kuwa ninaunga mkono kwa asilimia 100% juhudi za serikali awamu ya 5 kupambana na rushwa, ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi, ili mtindo unaotumiwa na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa, sio!.

Baada ya kukisikia kisanga cha TRA kilichomng'oa Kamishna Mkuu na maofisa kadhaa kufuatia sakata la makontena, leo amerudi tena bandarini na nimekishuhudia kitu anachokifanya, japo anashangiliwa na umati wa watu, lakini anachokifanya ni kuviziana, kutishana, kudhalilishana na kunakwenda kinyume cha utawala bora, yaani good governance!.

Waziri Mkuu anafanya ziara za kushtukiza mahali, huku akiwa na karatasi lenye tuhuma specific, lakini amelificha!, anakwenda kumuuliza mhusika wa pale kuhusu utendaji wa mfumo fulani, anaelezwa kuwa mfumo uko perfect, kisha analiibua hilo karatasi lenye tuhuma na kuanza kumsomea mhusika mbele ya kadamnasi ya watu, abcd!, mhusika anashindwa kujibu, atasimamishwa kazi, na kama yuko juu ya mamlaka yake, atamchongea kwa Rais!.

Hata TRA siku hiyo alikwenda na nondo za makontena, alipomuuliza Bade, akamjibu details ziko kwa maofisa wangu, ndipo akaibua nondo lake na kumsomea kwenye kadamnasi ili aonekane mjinga!, huku ni kuaibishana, kudhalilishana na kinyume cha good governance!.

Baada ya kutoka bandaini, akaenda TRL na kumuuliza mkurugenzi mkuu, mlikopa bilioni 3 TIB za kufanyia nini?!, kwa nini hamkufanya kile mlichokopea?, akaambiwa tumelipia mishahara, nani aliwapa idhini ya kukopa?!, Mkurugenzi hana jibu na naamini kesho atatangazwa hana kazi!.

Top management angekaa nao ofisini na kuulizana kistaarabu ndio good governance!. Mimi hata home, wife alikuwa na tabia ya kuwafokea ma tx home, mbele ya watoto, nikamkataza!, nikamsisitiza if things are not right, muite pembeni ndipo umseme, sio kumdhalilisha mbele ya watoto!.

Anachofanya Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa ni kuviziana, kudhalilishana na kuabishana bila sababu za msingi!, hili la kuitana na kuanza kuhojiana mbele ya waandishi ili watu wamuone alivyo mkali, ni tabia za ma populist leaders!, Leo nimemuona Magufuli akiongea na wafanyabiashara yuko very humble even cracking some jokes!.

Kama kuna watu wako karibu na Waziri Mkuu, wetu, Mhe. Majaliwa, Kasim Majaliwa, wamwambie anavyofanya sio vizuri, Sio Sawa, Sio Haki, Sio Good Governance!, Ni Udhalilishaji na Kuaibishana tuu!. Akumbushwe kuna kitu kinatwa 'karma' kisije kumshukia!.
Au wewe unaonaje?!, toa maoni yako ni sawa au sio sawa!.

Pasco

Huna jema ww wasipofanya kazi oooh hawafanyi kazi,wakifanya kazi sio good governance sasa unatakaje popoma?
 
tunatofautuana wajameni.......yaan mwizi aulizwe kiheshima????
mimi nlitegemea majaliwa cassim awacharaze kabisa bakora hadharani


huo unaoitwa utawala wa sheria ndio chanzo cha kulea mafisadi
 
Mbona hamuwaonei huruma vibaka mnawachoma moto hata wale walioiba kuku tu. Au suti walizovaa ndiyo zinazowafanya waonekane bora zaidi kuliko vibaka. Hao hawastahili staha, Mh Waziri Mkuu Big-Up Mungu atakulinda endeleza Mapambano wametutesa sana hao.
 
Hii nchi ina wakurugenzi na maboss zaidi ya 5000 wa serikali. Anachofanya ni kuonyesha mfano ili wengine washike adabu...
 
Pasco,
Kikatiba uko sawa kwa vile una uhuru wa kutoa maoni.
Nionavyo mimi,utawala bora ni kutopiga dili na vyote vifananvyo na hivyo. Sasa hawa jamaa kama wanaruhusu upigaji wa dili unataka turudi kule kule enzi za kuunda tume!? Ulitaka waunde tume,waitwe waulizwe watu walipane posho? No thank you...enough is enough. Mh waziri mkuu yuko sawa na bado kawaheshimu sana, kama huyo mzee wa TRL kweli unamtetea huyo? Mkurugenzi unakopa peas ya kitu kingine mnalipana mishahara! Hivi ni kweli TRL ingepata usimamizi mzuri ingeshindwa kujiendesha? Tukubari kuwa hapa hakuna usimamizi ndo maana wamekosa mishahara mpaka wakope billioni tatu za kulipana?
 
Wanyooshwe tu ikiwezekana wachapwe hata viboko hadharani sita wakiwa wanaingia kazini na sita wakiwa wanatoka wakawaoneshe wake zao,nchi iligeuzwa pagara la uswahilini,mimi kama mpinzani nilikuwa nalilia serikali ya aina hii toka nimepata akili,WACHA WAISOME NAMBA
 
Hawa sio viongozi nadhani hawajui wanataka kuifanyia nchi hii yaani majaliwa anauliza makontena 2431 ya January to December 2014 kwenye serikali waliyokuwemo kwa kweli nimeamini hawana plan yakutuvusha haya mambo yakupachikwa kwenye uongozi tabu tupu

mungu ainusuru nchi hii na binadamu aliowajazamo. hivi ni nini maana ya ukweli na uwazi? kama hayo makaratasi ya majaliwa yana uongo mbona ndiyo ingekuwa nafasi nzuri ya watuhumiwa kuyapinga na kumtia aibu pm?. lakini kwa kuwa yana ukweli wahusika wanashindwa kujitetea.hata kama alikuwa serikalini hapo hapakuwa sehemu yake ya utendaji. tuwe wastaarabu tuone nchi itafika wapi kwa style hii kama tulivyovumilia miaka 10 iliyopita.
 
Nina imani mtoa post ni VICTIM wa hizo ziara za kushutukiza za MP na sisi wananchi Tunampa GO AHAED sidhani kama ww utasikika ...
pole sana mkuu na siku si nyingi ataenda sehem nyngne na NONDO lingne ..najua itakuuma na utapost tenAa
Hapa kazi tu!!!
 
Kuna watu wanaakili z kuvukia Barabara ! Nahic huwezi kosa kwenye hilo kundi # pasco, tena kama huna cha kuandika usiwe unajaza watu upumbavu n utumbo wako
 
An apple a day, sends a doctor away.

Fanya kazi yako BARABARA hutamuona Majaliwa ofisini kwako. DSSD Mwananyamala, NSSF, CMA, na TANESCO wanaomba kutembelewa na PM.

Tena hawa CMA ndio nina usongo nao kweli kweli. Back then Kikwete alitembelea pale, the day yuko hapo anawasifia jinsi ambavyo wanaendesha kesi chap chap, mimi nilikuwa nina kesi yangu ina miezi 5, by the time hukumu imetolewa, mwajiri wangu ameshauza assets na hayupo nchini.
Pasco, cool down brother....there is no civilized way of slaughtering a pig.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom