Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 5,146
- 15,927
Nianze kwa na declaration of interest, ili kama kuna eneo nitakua 'biased' basi wajumbe mniuie radhi. Mimi ni Mtanzania muumuni wa dini ya kikristo. Nimekua mkristo kwa maisha yangu yote. Lakini pia ni muumini mkubwa wa haki, demokrasia na falsafa ya 'secular state'.
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa nchi yetu ya Tanzania ina tatizo la 'mfumo kristo', tatizo ambalo mizizi yake mirefu ilianzia kwenye utawala wa mkoloni ikiwa ni pamoja na mfumo wa elimu waa wamishonari (vitangulizi vya ukoloni).
Hata rais mstaafu wa awamu ya tatu hayati Ben Mkapa alikiri kwenye kitabu chake cha 'My Life My Purpose' juu ya tatizo hili na jinsi lilivyochangia kuwadidimiza ndugu zetu waislam, kama inavyoonekana kwenye ukurasa niliouambatanisha hapo chini.
Kutokana na mfumo huu, kumekua na tofauti kubwa ya namna viongozi wa nchi ambao ni wakristo wanavyotendewa ukilinganisha na wenzao ambao ni waislam.
Mfano mdogo tu ni hiki tunachokiona kwenye awamu hii ya mheshimiwa rais Magufuli, mara kwa mara amekua akiyageuza madhabahu ya makanisa kuwa 'platform' ya kufanyia siasa kwa kisingizio cha 'kumtanguliza Mungu mbele', kama hiyo haitoshi kila akienda kwenye ibada basi kurugenzi ya mawasiliano ikulu inaifanya hiyo kuwa habari rasmi ya kitaifa. Yaani ibada ambayo ni jambo la kibinafsi la Magufuli linageuzwa kuwa tukio rasmi la 'Rais Magufuli'.
Angalau basi jambo hili lingekua linafanyika kwenye siku chache maalumu kama vile krismas au pasaka, lakini hii imekua routine ya kawaida kabisa ya kiongozi wa nchi ambayo inapaswa kuwa haina dini bali ina wananchi wenye dini zao mbalimbali.
Hebu tujiulize na tuwe wakweli, kama rais Magufuli angekua muislam na angekua anayafanya haya misikitini kila ijumaa hali ingekuaje? Bila shaka mabaraza yote ya maaskofu yakiongozwa na TEC yangekua yamemkalia kooni na kumkosoa vikali, angeitwa kila aina ya majina kama vile 'mujahedeen' na kadhalika. Angekumbushwa na kila mtu kuwa nchi hii haina dini.
Lakini kwakua ni mkristo basi woote kwa unafiki mkubwa wako kimya, kwasababu mfumo umewafundisha kuwa hii ndio hali ya kawaida.
Pia tujiulize, salamu za kidini zina ulazima gani kwenye shughuli za kiserikali? Sikumbuki kuwahi kumsikia Mzee Mkapa akisalimia watu 'Bwana Yesu asifiwe', au 'As-salaam aleikum', au 'Bwana apewe sifa'. Sio kwamba alikua hamjui Mungu, lahasha! Mzee Ben alilelewa na kusomeshwa na waseminari kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la 12, na aliendelea kuwa muumini madhubuti wa kanisa katoliki kwa maisha yake yote. Kama hiyo haitoshi, baba yake mzazi alikua katekista! Lakini kama kiongozi wa nchi alielewa maana ya 'secular state'. Mambo yake binafsi ya kanisani aliyaacha kanisani, alipokuja mbele ya watanzania alikuja kama kiongozi wa watanzania wote.
Ni haki ya kikatiba ya rais Magufuli kuabudu na kufuata dini anayoitaka, lakini sio sawa kuyafanya mambo yake binfsi ya kidini kuwa mambo ya kitaifa na kiserikali. Hata watumishi wa umma wanazuiwa kufanya hivyo, lakini kutokana na mfano mbaya anaounesha mheshimiwa rais ndio maana haishangazi kuwaona askari wa jeshi la polisi huko Mbalizi Mbeya wakipiga maombi kituoni tena wakati wa saa za kazi wakiwa ndani ya uniform.
John 8:32
"And you will know the truth, and the truth will set you free"
Message sent and delivered