Mie ni Mkristo Mkatoliki siyo wa kuzaliwa tu bila wa imani. Naipenda sana dini yangu, na ninaamini ni sahihi kuliko zote, na nina hakika na wenzangu wengine wa imani tofauti ndivyo wanavyoamini kuhusu dini zao.
Kama muumini wa mafundisho ya dini yangu, bila ya kujali tofauti yoyote ile, ninaamini kila mwanadamu ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Nikitaka kumwona Mungu natakiwa kumwangalia aliye karibu yangu bila ya kujali huyo aliyepo karibu yangu ni muislam, mhindu au awaye yeyote.
Kutomtendea haki mwanadamu yeyote hata kama ni wa dini gani ni dhambi. Kuwa mnafiki ni dhambi mbaya zaidi.
Kuna mambo ya msingi ambayo mleta hoja ameyasema, na ninayakubali kwa asilimia kubwa. Kwa ujumla, mambo mengi yaliyopo nchini mwetu na katika mataifa mengi yameegemea kwenye desturi za Kikristo. Waislam wamekuwa na subira sana katika hilo. Lakini sisi tumekuwa sensitive sana kwa mambo madogo yakifanywa na kiongozi muislam.
Nakumbuka wakati wa Kikwete, akiteua viongozi 6, waislam wakawa 4 na wakristo 2, lazima minong'ono, miguno na hata lawama zitoke kuwa anawapendelea waislam. Lakini leo Rais mkristo, hata akiteua viongozi 8, muislam akawa 1, waislam wanavuta subira.
Leo, Rais Magufuli anaenda kutoa ujumbe kwaajili ya Taifa akiwa ndani ya kanisa, mbele madhabahuni. Waislam wanavuta subira. Jambo hilo siyo mara 1 au mara 2.
Kuna mambo makubwa tunatakiwa kujifunza:
1) Taifa huwa salama na mshikamano kunapokuwepo na subira ambayo ni sehemu ya hekima
2) Viongozi wanatakiwa wawe na hekima ya kujitahidi kutoamsha hisia za udini, ukabila, uchama na ukanda. Kauli nyingi za Rais Magufuli (kama zile za wa Mwanza wasivunjiwe nyumba, wapinzani watavunja madaraja, huu ni wakati wa kujenga maeneo mengine, wenzetu wa kaskazini wasubiri, n.k.) ni za kupalilia chuki na utengano
3) Ukipenda kuvumiliwa ujitahidi kuvumilia
4) Makuzi, malezi vina mchango mkubwa sana wa kumtengeneza mtu. Ndivyo vitu huchangia mtu kuwa wa namna gani hapo mbeleni. Viongozi waislam inaonekana wanakuwa na utu sana, wanathamini zaidi ustawi wa watu. Sijui jambo hili ni kwa bahati mbaya au linatokana na malezi wanayoyapata kwenye dini na jamii zao!
Ukiwaangalia viongozi wetu kwa kipimo cha uvumilivu, kama utataka kuwa mkweli wa nafsi yako, ni viongozi waislam ndiyo wanaoongoza kwa uvumilivu. Walinganishe Mwalimu, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli.
Uvumilivu ni utayari wa kusamehe. Mafundisho ya kikristo, tunafundishwa sana juu ya upendo, msamaha na kusaidiana LAKINI kwenye uhalisia kuna mashaka makubwa kama tunayaishi.
Wakati wa Kikwete, nyaraka za Kanisa na matamko ya Kanisa havikuwa haba, japo kiuhalisia hakukuwa na uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu kama awamu hii au awamu ya Mkapa. Unajiuliza, je, viongozi wetu wa dini huwa wana mahaba makubwa ya dini kuliko mahaba ya upendo wa kweli kama Mungu alivyoagiza?
Ni nje ya mada midogo - lakini inatafakarisha!
Sent using
Jamii Forums mobile app