Anachokifanya Rais Magufuli kingefanywa na Rais muislam basi angekosolewa vikali

Anachokifanya Rais Magufuli kingefanywa na Rais muislam basi angekosolewa vikali

Status
Not open for further replies.
Mie ni Mkristo Mkatoliki siyo wa kuzaliwa tu bila wa imani. Naipenda sana dini yangu, na ninaamini ni sahihi kuliko zote, na nina hakika na wenzangu wengine wa imani tofauti ndivyo wanavyoamini kuhusu dini zao.

Kama muumini wa mafundisho ya dini yangu, bila ya kujali tofauti yoyote ile, ninaamini kila mwanadamu ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Nikitaka kumwona Mungu natakiwa kumwangalia aliye karibu yangu bila ya kujali huyo aliyepo karibu yangu ni muislam, mhindu au awaye yeyote.

Kutomtendea haki mwanadamu yeyote hata kama ni wa dini gani ni dhambi. Kuwa mnafiki ni dhambi mbaya zaidi.

Kuna mambo ya msingi ambayo mleta hoja ameyasema, na ninayakubali kwa asilimia kubwa. Kwa ujumla, mambo mengi yaliyopo nchini mwetu na katika mataifa mengi yameegemea kwenye desturi za Kikristo. Waislam wamekuwa na subira sana katika hilo. Lakini sisi tumekuwa sensitive sana kwa mambo madogo yakifanywa na kiongozi muislam.

Nakumbuka wakati wa Kikwete, akiteua viongozi 6, waislam wakawa 4 na wakristo 2, lazima minong'ono, miguno na hata lawama zitoke kuwa anawapendelea waislam. Lakini leo Rais mkristo, hata akiteua viongozi 8, muislam akawa 1, waislam wanavuta subira.

Leo, Rais Magufuli anaenda kutoa ujumbe kwaajili ya Taifa akiwa ndani ya kanisa, mbele madhabahuni. Waislam wanavuta subira. Jambo hilo siyo mara 1 au mara 2.

Kuna mambo makubwa tunatakiwa kujifunza:

1) Taifa huwa salama na mshikamano kunapokuwepo na subira ambayo ni sehemu ya hekima

2) Viongozi wanatakiwa wawe na hekima ya kujitahidi kutoamsha hisia za udini, ukabila, uchama na ukanda. Kauli nyingi za Rais Magufuli (kama zile za wa Mwanza wasivunjiwe nyumba, wapinzani watavunja madaraja, huu ni wakati wa kujenga maeneo mengine, wenzetu wa kaskazini wasubiri, n.k.) ni za kupalilia chuki na utengano

3) Ukipenda kuvumiliwa ujitahidi kuvumilia

4) Makuzi, malezi vina mchango mkubwa sana wa kumtengeneza mtu. Ndivyo vitu huchangia mtu kuwa wa namna gani hapo mbeleni. Viongozi waislam inaonekana wanakuwa na utu sana, wanathamini zaidi ustawi wa watu. Sijui jambo hili ni kwa bahati mbaya au linatokana na malezi wanayoyapata kwenye dini na jamii zao!

Ukiwaangalia viongozi wetu kwa kipimo cha uvumilivu, kama utataka kuwa mkweli wa nafsi yako, ni viongozi waislam ndiyo wanaoongoza kwa uvumilivu. Walinganishe Mwalimu, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli.

Uvumilivu ni utayari wa kusamehe. Mafundisho ya kikristo, tunafundishwa sana juu ya upendo, msamaha na kusaidiana LAKINI kwenye uhalisia kuna mashaka makubwa kama tunayaishi.

Wakati wa Kikwete, nyaraka za Kanisa na matamko ya Kanisa havikuwa haba, japo kiuhalisia hakukuwa na uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu kama awamu hii au awamu ya Mkapa. Unajiuliza, je, viongozi wetu wa dini huwa wana mahaba makubwa ya dini kuliko mahaba ya upendo wa kweli kama Mungu alivyoagiza?

Ni nje ya mada midogo - lakini inatafakarisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenena mkuu
 
Hapa kama ni kumlaumu ni Kurugenzi ya mawasiliano ikulu kwani sidhani kila anachofanya Rias au kila anapokuwepo rais ni yeye moja kwa moja anawataka wampe covarage.
Kwa upande mwingine, sio aibu kuwa muumini wa dini iwayo yote maadam mtu hajavunja sheria.
Tunakuwa watu wa ajabu sana pale ambapo mtu ameingia kanisani kuomwomba Mungu alimuumba halafu mtu mwingine aone ni kero.
Mara ngapi nyakati za ijumaa au nyakati za Idd El Fitir TV zinaonesha swala au maidha ya Kiislamu na hatupati kero?

Kumheshimu mtu anaekwenda kumwomba Mungu aliemuumba ni jambo kubwa sana na hata wimbo wa taifa una mstari unasema "Mungu Ibariki Afrika.... Mungu Ibariki Tanzania"

Nampongeza Rais kwa kumtegemea Mungu na kumwomba Mungu na imani yake kwa Mungu na ujasiri wake kumtegemea Mungu, Tanzania tumevushwa kwenye janga la Covid19 na majanga mengi.

Naendelea kuamini, Rais hajakosea kwenda kanisani, na kwa mtu kuona picha/taarifa anakereka kwa Rais kwenda kanisani kwa kuwa ni Mkisto na hakuwa anahubiri injili ili watu wageuzwe kuwa wakristo, basi ninazidi kushangaa

Vipindi vya Ijumaa na Jumapili vilikuwa vikirushwa redioni tangu enzi za Nyerere. Lakini Kamwe hukuwahi kuona Nyerere analigeuza Kanisa madhabahu ya kutolea miongozo ya kiserikali kama alivyofanya Magufuli kipindi cha Korona. Kipindi hicho alitoa hotuba mbili za muelekeo wa Korona nchini kanisani!.

Pili imekuwa tabia siku hizi akienda kusali jumapili kurugenzi ya habari inatoa press release kuwa Magufuli leo kasalia kanisa fulani, Mbona Nyerere alikuwa hakosi misa ya asubuhi pale St Peters na pia Jumapili alikuwa akifanya Ibada lakini hukuwahi kuona mambo yake binafsi ya imani yanegeuka kuwa ni ishu ya kitaifa?
 
Kwanza, "Wewe ni mujahidin"
Pili umejawa na Chuki,

Tatu, Kikwete na Mwinyi wote walikuwa waislamu.
Nne, Magufuli alishasema hapangiwi, sasa kama unatka rais wa kupangiwa, subiri ucvhaguzi oktoba uchague huyo umtakaye, kuna waislamu wengi tu wanagombea.

Tano, Swala za msikiti haziruhusu kuzungumza tu, maana huwa ni za muda mfupi mfupi.

Si kweli kwamba kuna mfumo kristo, hizo ni hadithi zako, na inferiority complex yako, hakuna sensa iliyofanyika kutaka kujua idadi ya waislamu na wakristo walioajiriwa kwenye ofisi za umma.
Mbona hujagusia Bharesa kuajiri waislamu tu karibu kila idara kwenye makampuni yake?
Hayo ni mawazo yako, sio lazima yawe na uhalisia wowote.
 
Mie ni Mkristo Mkatoliki siyo wa kuzaliwa tu bila wa imani. Naipenda sana dini yangu, na ninaamini ni sahihi kuliko zote, na nina hakika na wenzangu wengine wa imani tofauti ndivyo wanavyoamini kuhusu dini zao.

Kama muumini wa mafundisho ya dini yangu, bila ya kujali tofauti yoyote ile, ninaamini kila mwanadamu ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu. Nikitaka kumwona Mungu natakiwa kumwangalia aliye karibu yangu bila ya kujali huyo aliyepo karibu yangu ni muislam, mhindu au awaye yeyote.

Kutomtendea haki mwanadamu yeyote hata kama ni wa dini gani ni dhambi. Kuwa mnafiki ni dhambi mbaya zaidi.

Kuna mambo ya msingi ambayo mleta hoja ameyasema, na ninayakubali kwa asilimia kubwa. Kwa ujumla, mambo mengi yaliyopo nchini mwetu na katika mataifa mengi yameegemea kwenye desturi za Kikristo. Waislam wamekuwa na subira sana katika hilo. Lakini sisi tumekuwa sensitive sana kwa mambo madogo yakifanywa na kiongozi muislam.

Nakumbuka wakati wa Kikwete, akiteua viongozi 6, waislam wakawa 4 na wakristo 2, lazima minong'ono, miguno na hata lawama zitoke kuwa anawapendelea waislam. Lakini leo Rais mkristo, hata akiteua viongozi 8, muislam akawa 1, waislam wanavuta subira.

Leo, Rais Magufuli anaenda kutoa ujumbe kwaajili ya Taifa akiwa ndani ya kanisa, mbele madhabahuni. Waislam wanavuta subira. Jambo hilo siyo mara 1 au mara 2.

Kuna mambo makubwa tunatakiwa kujifunza:

1) Taifa huwa salama na mshikamano kunapokuwepo na subira ambayo ni sehemu ya hekima

2) Viongozi wanatakiwa wawe na hekima ya kujitahidi kutoamsha hisia za udini, ukabila, uchama na ukanda. Kauli nyingi za Rais Magufuli (kama zile za wa Mwanza wasivunjiwe nyumba, wapinzani watavunja madaraja, huu ni wakati wa kujenga maeneo mengine, wenzetu wa kaskazini wasubiri, n.k.) ni za kupalilia chuki na utengano

3) Ukipenda kuvumiliwa ujitahidi kuvumilia

4) Makuzi, malezi vina mchango mkubwa sana wa kumtengeneza mtu. Ndivyo vitu huchangia mtu kuwa wa namna gani hapo mbeleni. Viongozi waislam inaonekana wanakuwa na utu sana, wanathamini zaidi ustawi wa watu. Sijui jambo hili ni kwa bahati mbaya au linatokana na malezi wanayoyapata kwenye dini na jamii zao!

Ukiwaangalia viongozi wetu kwa kipimo cha uvumilivu, kama utataka kuwa mkweli wa nafsi yako, ni viongozi waislam ndiyo wanaoongoza kwa uvumilivu. Walinganishe Mwalimu, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli.

Uvumilivu ni utayari wa kusamehe. Mafundisho ya kikristo, tunafundishwa sana juu ya upendo, msamaha na kusaidiana LAKINI kwenye uhalisia kuna mashaka makubwa kama tunayaishi.

Wakati wa Kikwete, nyaraka za Kanisa na matamko ya Kanisa havikuwa haba, japo kiuhalisia hakukuwa na uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu kama awamu hii au awamu ya Mkapa. Unajiuliza, je, viongozi wetu wa dini huwa wana mahaba makubwa ya dini kuliko mahaba ya upendo wa kweli kama Mungu alivyoagiza?

Ni nje ya mada midogo - lakini inatafakarisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli mtupu 100%.
Umemaliza kila kitu.
 
Mada nyingine za uchochezi. Ungejua kwamba rais huyu yupo karibu sana na waislam wala usingepoteza muda wako kuandika haya uliyoyaandika.

Yapo mengi ambayo kiutu uzima mtu unatakiwa uyasahau kadri siku za kuishi zinavyosogea. Yapo mengi ya marais waliotangulia ambayo kiubinadamu tumeshayasahau kwani maisha yakienda huwa hayarudi nyuma.

JPM anapoongea makanisani huwa hafanyi fitina kwa wale wa dini nyingine, anasisitizia umoja na upendo. Chunga sana mleta mada kwani mawazo yako sio mema kwa taifa hili.
 
Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa nchi yetu ya Tanzania ina tatizo la 'mfumo kristo', tatizo ambalo mizizi yake mirefu ilianzia kwenye utawala wa mkoloni ikiwa ni pamoja na mfumo wa elimu waa wamishonar

Tatizo lipo pia kwa watoto wanaotoka katika familia masikini, wanaishia kusoma katika shule na vyuo vikuu duni vya kata. Hili linawaathiri wote bila kujali walizaliwa katika dini gani.

Inatakiwa elimu bora kwa wote bila kujali dini, umasikini wa familia au eneo la Tanzania anapotoka mtoto wa kiTanzania.

Suluhisho ni shule zote za serikali yaani Government schools alizozisema Mkapa katika kitabu chake ziimarishe utoaji elimu bora na kuhakikisha pia mafunzo bora na sahihi kwa waalimu.

Tunaona shule za msingi za serikali zote vibao vimeandikwa Ofisi ya Rais TAMISEMI shule ya msingi Msolwa n.k hivyo kuondoa tofauti ya viwango vya elimu katika shule za serikali na zile za binafsi/ private basi serikali iwekeze pesa nyingi ktk shule zake zote zilizotapakaa nchi nzima ili kuondoa nakisi hii ya elimu baina ya watoto wa viongozi na watoto wa masikini.
 
wewe ndio upo biased unakitu unachoamini kichwani mwako ndio unaona sahihi hikohiko , kuwa free minded mambo haya hayatakufikirisha mfano umemquotes mhe. mkapa kwenye kitabu chake ila mm nilivyosoma hiyo quotation nimeelewa alikuwa anaongelea mfumo wa elimu enzi za ukoloni..

serikali za kikoloni waliwaachia missionary wahusike kwenye swala la kutoa elimu kwa kuwaruhusu wajenge mashule hivyo ulisababisha wakristo wanufaike zaidi ya waisilamu ambao wao walitegemea zaidi shule za serikari na zilikuwa chache sana.

lkn haina maana mfumo wetu wa elimu sasa pia unapendelea wakristo zaidi HAPANA

watu disaini yk ni hatari imagine wewe umebahatika kusoma labda ikatokea kuaminiwa utoe mawaidha na waumini wenzako msikitini ambao wengi hawana elimu km yako ukaanza kufanya quotation km uliyoifanya hapa na ukawaaminisha wenzio kuwa mfumo wetu wa elimu unapendelea wakristu tu, utawapandikiza chuki waumini wenzio zidi ya serikali na wakristo isiyo na sababu mwishowe ni machafuko..

nikushauri tu ukiona km wakristo wanamashule mengi ujue waliivest na wanainvest kwa kuchangishana makanisani na misaada michache kutoka nchi waisani na wewe washawishi waumini wenzako na nchi wahisani ili mjenge mashule na vyuo vingi ili mjiinue kielemu na baada ya muda utakuwa sawa na wenzenu au hata kuwapita.

Hujamuelewa rudia kusoma neno kwa neno
 
Mada nyingine za uchochezi. Ungejua kwamba rais huyu yupo karibu sana na waislam wala usingepoteza muda wako kuandika haya uliyoyaandika.

Yapo mengi ambayo kiutu uzima mtu unatakiwa uyasahau kadri siku za kuishi zinavyosogea. Yapo mengi ya marais waliotangulia ambayo kiubinadamu tumeshayasahau kwani maisha yakienda huwa hayarudi nyuma.

JPM anapoongea makanisani huwa hafanyi fitina kwa wale wa dini nyingine, anasisitizia umoja na upendo. Chunga sana mleta mada kwani mawazo yako sio mema kwa taifa hili.
Kwahiyo siku tukiwa na rais muislam na yeye pia akaamua kwa nia njema kabisa kutumia misikiti kusisitiza amani na upendo kwa nchi yetu, huku taarifa hizi zikiambatana na press release za ikulu, basi kusiwe na malalamiko ya aina yoyote.
 
Ulicho kisema ni kweli haya mambo yaliyo jaa uovu ndani yake yanayo fanywa na jiwe yangekuwa yanafanywa na raisi muislam angekuwa anakashifiwa na kutukanwa na matusi ya kila aina kila siku angekuwa anajadiliwa makanisani.
Kinacho tokea hawamu hii kimenifanya nianze kuhisi wenda hata kashifa zilizo kuwa zinatokea kipindi cha kikwete zilikuwa zinatengenezwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumu hujumu kwa sababu ya dini yake.
Nchi hii imejaa udini,unafiki,majungu, yaan kila aina ya takataka.
Mara nyingi tulimsema vibaya Kikwete, lakini nikitafakari leo hii, ukimwondoa Mwalimu, nina hakika Kikwete was the best President.

Ningetamani Mnyika amwombe Kikwete msamaha wa wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipindi vya Ijumaa na Jumapili vilikuwa vikirushwa redioni tangu enzi za Nyerere. Lakini Kamwe hukuwahi kuona Nyerere analigeuza Kanisa madhabahu ya kutolea miongozo ya kiserikali kama alivyofanya Magufuli kipindi cha Korona. Kipindi hicho alitoa hotuba mbili za muelekeo wa Korona nchini kanisani!.

Pili imekuwa tabia siku hizi akienda kusali jumapili kurugenzi ya habari inatoa press release kuwa Magufuli leo kasalia kanisa fulani, Mbona Nyerere alikuwa hakosi misa ya asubuhi pale St Peters na pia Jumapili alikuwa akifanya Ibada lakini hukuwahi kuona mambo yake binafsi ya imani yanegeuka kuwa ni ishu ya kitaifa?
Haswaa.
Tulimjua Nyerere kama mwanasiasa tu, japokuwa alikuwa mkatoliki ambaye karibu kila siku alfajiri alihudhuria kanisani na hatukuwahi kutaarifiwa hilo kiserikali au kitaifa.

Maajabu yapo kwa huyu rais wa sasa. Ni vituko vitupu.
 
Jiwe is guilty ya mambo mengi ya dhulma nchi hii, anajiegemeza kwenye dini ili kupata sympathy ya watu.

Anatafuta sana uungwaji mkono wa makanisa ambayo miaka mitatu iliyopita yalimnyooshea kidole kutokana na style ya uongozi wake usioheshimu haki za binadamu.

Hajali sana hisia za waislamu kwa sababu anajua kuwa maadamu ana Masheikh walio kwenye payrol yake basi atawatuliza kwa vizawadi viwili vitatu kisha atatoboa.

Lakini pia kwa kuwa alipitia seminari ili kuwa padri vikamshinda anaamini njia peke ya kusahihisha guilty yake ya kufeli huko basi ni kufanya upendeleo kwa watu wa imani yake au kutumia madaraka kujifanya loyal zaidi kwa dini yake

Tofauti na Mkapa ni kuwa Mkapa pia alipitia kwenye umisionari lakini tofauti na Jiwe,ni kuwa Mkapa kazaliwa kwenye jamii yenye waislamu wengi mikoa ya kusini huko, kwa hiyo kacheza utotoni na waislamu, ndiyo maana hata ukubwani alikuwa na sense ya fairness kwa waislamu. Kwa mfano kipindi Mkapa alipokuwa raisi, aliwahi kuvunja bodi ya Parole iliyokuwa na wakiristo watupu akaweka na waislamu, na ndiyo maana kwenye kitabu chake anakubali kuwa kweli kulikuwa na imbalalnce ya kielimu kati ya waislamu na wasio waislamu kipindi cha uhuru na kwenye utumishi wa umma wakati huo. Jiwe yeye kakulia mikoa yenye waislamu wachache kwa hiyo kwake Uislam ni kitu alien, kakutana na waislamu ukubwani huko mashuleni!

Pia kitu kingine ni kuwa, Jiwe aliingia madarakani akiwa na chuki kali dhidi ya waislamu, ndiyo maana kitu cha kwanza alichofanya ni kufanya teuzi na kuwapiga chini sana waislamu katika teuzi zake. Alipogundua kuwa hili lingemletea matatizo ndo akaona awakumbatie baadhi ya masheikh wamfanyie kazi ya kutuliza joto la waislamu.

Katika viongozi wadini, Jiwe hafai kabisa!
 
Mtoa hoja nadhani kuna jambo kubwa kubwa sana una-miss na iko haja kuweka record sawa.

Nianze na ku-declare interest, mimi ni Mkristo pia, ili muktadha wa mjadala uwe sawia.

Kusudi la Injili ya Kristo ni kuwahubiri wanadamu wote upendo wa Mungu ili wawe Wakristo. Ndio maana ujio wa Ukristo kupitia wamishenari, walihubiri Ukristo kwa watu wote na walioamini walikuwa converted kutoka kwenye dini zao ili wawa Wakristo bila kuja dhehebu.

Matthew 28: 19-20
Therefore go and make disciples of all nations, baptizing them in the name of the Father and of the Son and of the Holy Spirit, and teaching them to obey everything I have commanded you

Mara nyingi Rais Magufuli ameonekana makanisani, sio kanisa lake la Katoliki bali hata makanisa mengine. Sijawahi kumsikia akihubiri injili ya kuwataka Watanzania wawe converted kuwa Wakristo.

Mara nyingi amekuwa akitutaka/akituasa Watanzania tumtangulize Mungu katika mambo yetu, tumwombee yeye, tuitakie nchi amani; mambo haya ni sawa kabisa kwa mtu yeyote nobble.

John Magufuli ambae pia ni Rais, kwa msingi wa imani ya Kikristo alitakiwa ahubiri injili na kuwataka watu wote wabatizwe kama Biblia ilivyoandika (rejea Matthew 28); angesimama kuhubiri upendo wa Kristo madhabahuni na kuwataka Watanzania wawe converted kuwa Wakristo, nadhani kesho yake mitandao ya kijamii na media za ughaibuni zingeponda sana kwanini Rais anahubiri Ukristo madhabahuni huku pia ni sehemu ya wajibu wake.

Itoshe kusema, tumepata Rais ambae anampenda Mungu bila kujali mapungufu machache ambayo anaweza kuwa nayo kama mwanadamu yeyote yule. Kwa yeye kwenda kusali mbele za Mungu makanisani ni ishara ya unyenyekevu kwa Mungu; Yesu alisema, mwenye afya hamwitaji Daktari, sisi wengi twaenda kanisani si kwa kuwa tu wakamilifu, bali tunahitaji injili inayohubiriwa madhabahuni itungeuze mioyo yetu tumjue Mungu zaidi na kuwatendea wema jirani zetu sawia na maandiko yanvyo tuangiza.

Tumwombeeni John Magufuli kwa kuwa ni mwanadamu, tumwombeeni John Magufuli kwa kuwa ni Rais, Mkuu wa Nchi na Amri Jeshi Mkuu.

...Therefore I [a]exhort first of all that supplications, prayers, intercessions, and giving of thanks be made for all men, for kings and all who are in [b]authority, that we may lead a quiet and peaceable life in all godliness and [c]reverence

...I urge, then, first of all, that petitions, prayers, intercession and thanksgiving be made for all people— for kings and all those in authority, that we may live peaceful and quiet lives in all godliness and holiness.

1Timothy 2:1,2
Contradiction Kubwa

Utawala wa Rais Magufuli - utekaji watu, upotezaji watu, mauaji ya watu, mashambulio ya risasi ya watu wanamkosoa. Watu kutengnezewa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ili wateseke mahabusu, n.k.

Rais Magufuli - ni mcha Mungu

Na tabia mbili zisizoendana kamwe!!!

Tusisahau pia kuwa kumtaja taja Mungu kila wakati haimaanishi mtu ni mcha Mungu. Marais kama Sadam Hussein, Gadafi, Hosni Mubaraka, neno Mungu lilikuwa halipungua kwenye vinywa mwao. Msisikilize maneno yao, tazameni matendo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye secular state angeweka dini pembeni ila jiwe tunamjua anataka alazimishe anachokiamini basi wote wafate hichohicho. Same for dini same for uchama, jamaa ana quality zote za kiongozi mbaya. Yeye anahisi atatumia brute force kwenye kila kitu, watakaoleta za kuleta anajua atatumia nguvu kuwanyamazisha. Stupid way of thinking anaweza leta damage ambayo kuja kuifix Tanzania itacost watu maisha
Kuna siku Jiwe aliwahi kuwaambia watu wawe wakristo?
 
Vipindi vya Ijumaa na Jumapili vilikuwa vikirushwa redioni tangu enzi za Nyerere. Lakini Kamwe hukuwahi kuona Nyerere analigeuza Kanisa madhabahu ya kutolea miongozo ya kiserikali kama alivyofanya Magufuli kipindi cha Korona. Kipindi hicho alitoa hotuba mbili za muelekeo wa Korona nchini kanisani!.

Pili imekuwa tabia siku hizi akienda kusali jumapili kurugenzi ya habari inatoa press release kuwa Magufuli leo kasalia kanisa fulani, Mbona Nyerere alikuwa hakosi misa ya asubuhi pale St Peters na pia Jumapili alikuwa akifanya Ibada lakini hukuwahi kuona mambo yake binafsi ya imani yanegeuka kuwa ni ishu ya kitaifa?
Enzi ya Nyerere hapakuwa na social media ili kuwa na live streams au kutoa habari zilizotokea muda mfupi uliopita.

Sio kukuza udini kwa taarifa kutoka Rais kanisani kama ambavyo hata JK akiwa Rais kuna picha zipo hata mpaka sasa kwenye website ya IKULU, rais yuko msikitini au kwenye sala ya Eid. Na haikuwa kosa hata magazeti ya kesho yake ku-chapa front page.

Mbona EL alifanya fund raising makanisani na misikitini na haikuwa nongwa. Wakati huo tukiaminishwa ana changizo la upendo kwa watu kutoka kwa rafiki zake. Baada ya kukosa Urais, hata changizo la Covid19 hakuonekana. Mbona hamkulalamika EL anachangia kanisani na misikitini.

Acheni uchochozi na chokochoko.

Rais akienda kusali na hafanya ibada kama platform ya kuomba umoja ya kitaifa, kumtegemea Mungu na kushukuru Mungu kwa kazi za serikali ambazo baadhi ya washirika kanisani na hata wasio washirika wanafaidika kama uwepo wa barabara, huduma za kijamii kama maji, huduma za afya, mikopo kwa wanafunzi vyuo vikuu, elimu bila malipo; anapoyasemea haya ni sehemu ya kumshukuru Mungu kwa yanayofanyika.

Itakuwa kosa na lawama kama anaomba kura mbele ya madhabahu na TV/Kurugenzi Ikulu akaifanya kuwa agenda.
 
Contradiction Kubwa

Utawala wa Rais Magufuli - utekaji watu, upotezaji watu, mauaji ya watu, mashambulio ya risasi ya watu wanamkosoa. Watu kutengnezewa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ili wateseke mahabusu, n.k.

Rais Magufuli - ni mcha Mungu

Na tabia mbili zisizoendana kamwe!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Uko sahihi kiongozi!

Magufuli anaitumia dini kisiasa ili kupata sympathy ya umma na uungwaji mkono wa makanisa kwa sababu they are very powerful nchini.

Hajali sana hisia za waislamu kwa sababu anajua namna gani ya kudili nao kupitia vibaraka kama Sheikh Alhadi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom