Anachokifanya Rais Magufuli kingefanywa na Rais muislam basi angekosolewa vikali

Status
Not open for further replies.
Haya kila la heri, na kushauri tu lakini,sema na huo moyo wako.
Haki huinua taifa ndugu, sina lengo la kumchochea mtu, pia sidhani kama kuna mtanzania anaweza kuchochewa kupitia mitandao ya kijamii, Mange Kimambi analijua hilo.

Lakini pale kunapokua na jambo ambalo halina afya kwa nchi ni vema wananchi walijadili.
 
Ndugu yangu, kwani mleta mada kuzungumzia jambo la kujenga mshikamano wa kitaifa unaona amekosea nini?
Kwa hiyo wewe mathalani ukiona waislamu wananyanyapaliwa utakaa kimya kwa sababu wewe siyo muislamu?
Au unataka muislamu akiona mkristo ananyanyapaliwa akae kimya kwa sababu yeye siyo mkiristo?

Wewe ndugu yangu, Taifa hili ni Taifa letu sote, tupo ndani ya boti moja iktoboka mahali usianze kusema wewe haikuhusu kwa sababu haikutoboka pale ulipokaa wewe!
 
Mie ni mkristo (RC) lakini naona aibu na hasira sana mtu anaejitanabahi kuwa ni Mkristo halafu anashadadia mambo ya UDINI tena kwa kuponda imani za watu wengine ie uislamu! Sio malezi yetu wakristo kufanya haya, tuache ujinga tena ninyi ni wakristo majina na sio watu wa imani kamili ya ki-kristo.
 
Haki huinua taifa ndugu, sina lengo la kumchochea mtu, pia sidhani kama kuna mtanzania anaweza kuchochewa kupitia mitandao ya kijamii, Mange Kimambi analijua hilo.

Lakini pale kunapokua na jambo ambalo halina afya kwa nchi ni vema wananchi walijadili.

Ndio maana nimekuambia "all the best" labda nikukumbushe pale mwanzo nilisema JF si ya mazezeta.
 
Matthew 28: 19-20
Therefore go and make disciples of all nations, baptizing them in the name of the Father and of the Son and of the Holy Spirit, and teaching them to obey everything I have commanded you
Haya maneno ameyasema Matayo au Yesu ?

Nataka nifahamu hili, kisha tujenge hoja kutokea hapa.
 
Mie ni mkristo (RC) lakini naona aibu na hasira sana mtu anaejitanabahi kuwa ni Mkristo halafu anashadadia mambo ya UDINI tena kwa kuponda imani za watu wengine ie uislamu! Sio malezi yetu wakristo kufanya haya, tuache ujinga tena ninyi ni wakristo majina na sio watu wa imani kamili ya ki-kristo.

Ungejua Ukristo ulipochipukia kule kwa Ibrahimu Isihaka na Yakobo. Ukajua maelekezo/mafundisho yake si dhani kama ugali andika hivi. Na ashukuriwe Mungu, Emanueli aliye kuja akaishi nasi kati yetu hapa dunia, Yesu akafanya moderation. Vinginevyo sijui.
 
Hii mada ulitakiwa uweke angalizo la wenye akili tu na walio neutral kimawazo kuwa ndo wahusika kuchangia. Bahati mbaya wamekuja wafia dini na wajinga wajinga ambao hawajui lolote kuhusu utengamano wa kitaifa.

Mimi mkristo, zile barua za wazi kutoka TEC na wakristo wengine kipindi cha Kikwete ziko wapi leo. Ule ukosoaji kipindi kile uko wapi? Mbona sikuwahi ona matangazo kuwa Kikwete kaenda kuswali Ijumaa.
Yani Magufuli anaenda kusali nayo inakuwa headline kwenye media, kurugenzi ya ikulu nayo inasema. Hawa watu wanaolazimisha tuwaone wacha Mungu sijawahi waamini.
Mimi ni shabiki mzuri sana wa secularism. Imagine Kikwete angekuwa anavaa kanzu kama watu wa Pwani si yangetolewa matamko ya kupinga.
Kumbuka kanzu za mara kwa mara alizokuwa anavaa Ramadhani Dau zilivyowapa watu kiwewe ingawa alikuwa anavaa Ijumaa tu.
 
Wengine "Asalamu Aleikum" zikianza kuwa nyingi katika korido za maofisi huanza kukasirika kuwa ofisi hii imejaza wajahidina, fitna huanzia hapo.
 
Nianze kwa na declaration of interest, ili kama kuna eneo nitakua 'biased' basi wajumbe mniuie radhi. Mimi ni Mtanzania muumuni wa dini ya kikristo. Nimekua mkristo kwa maisha yangu yote. Lakini pia ni muumini mkubwa wa haki, demokrasia na falsafa ya 'secular state'.

Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa nchi yetu ya Tanzania ina tatizo la 'mfumo kristo', tatizo ambalo mizizi yake mirefu ilianzia kwenye utawala wa mkoloni ikiwa ni pamoja na mfumo wa elimu waa wamishonari (vitangulizi vya ukoloni).

Hata rais mstaafu wa awamu ya tatu hayati Ben Mkapa alikiri kwenye kitabu chake cha 'My Life My Purpose' juu ya tatizo hili na jinsi lilivyochangia kuwadidimiza ndugu zetu waislam, kama inavyoonekana kwenye ukurasa niliouambatanisha hapo chini.

View attachment 1537659

Kutokana na mfumo huu, kumekua na tofauti kubwa ya namna viongozi wa nchi ambao ni wakristo wanavyotendewa ukilinganisha na wenzao ambao ni waislam.

Mfano mdogo tu ni hiki tunachokiona kwenye awamu hii ya mheshimiwa rais Magufuli, mara kwa mara amekua akiyageuza madhabahu ya makanisa kuwa 'platform' ya kufanyia siasa kwa kisingizio cha 'kumtanguliza Mungu mbele', kama hiyo haitoshi kila akienda kwenye ibada basi kurugenzi ya mawasiliano ikulu inaifanya hiyo kuwa habari rasmi ya kitaifa. Yaani ibada ambayo ni jambo la kibinafsi la Magufuli linageuzwa kuwa tukio rasmi la 'Rais Magufuli'.

Angalau basi jambo hili lingekua linafanyika kwenye siku chache maalumu kama vile krismas au pasaka, lakini hii imekua routine ya kawaida kabisa ya kiongozi wa nchi ambayo inapaswa kuwa haina dini bali ina wananchi wenye dini zao mbalimbali.

Hebu tujiulize na tuwe wakweli, kama rais Magufuli angekua muislam na angekua anayafanya haya misikitini kila ijumaa hali ingekuaje? Bila shaka mabaraza yote ya maaskofu yakiongozwa na TEC yangekua yamemkalia kooni na kumkosoa vikali, angeitwa kila aina ya majina kama vile 'mujahedeen' na kadhalika. Angekumbushwa na kila mtu kuwa nchi hii haina dini.

Lakini kwakua ni mkristo basi woote kwa unafiki mkubwa wako kimya, kwasababu mfumo umewafundisha kuwa hii ndio hali ya kawaida.

Pia tujiulize, salamu za kidini zina ulazima gani kwenye shughuli za kiserikali? Sikumbuki kuwahi kumsikia Mzee Mkapa akisalimia watu 'Bwana Yesu asifiwe', au 'As-salaam aleikum', au 'Bwana apewe sifa'. Sio kwamba alikua hamjui Mungu, lahasha! Mzee Ben alilelewa na kusomeshwa na waseminari kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la 12, na aliendelea kuwa muumini madhubuti wa kanisa katoliki kwa maisha yake yote. Kama hiyo haitoshi, baba yake mzazi alikua katekista! Lakini kama kiongozi wa nchi alielewa maana ya 'secular state'. Mambo yake binafsi ya kanisani aliyaacha kanisani, alipokuja mbele ya watanzania alikuja kama kiongozi wa watanzania wote.

Ni haki ya kikatiba ya rais Magufuli kuabudu na kufuata dini anayoitaka, lakini sio sawa kuyafanya mambo yake binfsi ya kidini kuwa mambo ya kitaifa na kiserikali. Hata watumishi wa umma wanazuiwa kufanya hivyo, lakini kutokana na mfano mbaya anaounesha mheshimiwa rais ndio maana haishangazi kuwaona askari wa jeshi la polisi huko Mbalizi Mbeya wakipiga maombi kituoni tena wakati wa saa za kazi wakiwa ndani ya uniform.

John 8:32
"And you will know the truth, and the truth will set you free"
Message sent and delivered
Magufuli, kama mfalme Daudi amependa kuwa bawabu katika nyumba ya Bwana kuliko kushinda kwenye hema ya uovu.. Hilo ni jambo jema.. Wacha autumie urais wake katika kumtumikia Mungu.. Akifika mbinguni, atapata thawabu kwa hilo.
Screenshot_20200815-113758.png
 
Magufuli, kama mfalme Daudi amependa kuwa bawabu katika nyumba ya Bwana kuliko kushinda kwenye hema ya uovu.. Hilo ni jambo jema.. Wacha autumie urais wake katika kumtumikia Mungu.. Akifika mbinguni, atapata thawabu kwa hilo.
View attachment 1537844
Ni vema, lakini siku tukiwa na rais muislam na yeye pia akaamua kuwa bawaba kwenye nyumba ya Allah basi tusione nyaraka na kelele zozote toka makanisani.
 
Hivi si atakutana na Ma sheikh hivi karibuni ? Unonaje ukipeleka maoni yako kwa hao ili wamwambie live...

Kwa maoni yangu mwenye busara ni yule tu aliyesema (Serikali yetu haina Dini).., haya mambo ya kutumia Dini kwenye uongozi mwisho wa siku ni kutumia Dini vibaya na tukija kwenye IMANI mtu anaweza kufanya lolote kwa kisingizio cha IMANI
 
Nianze kwa na declaration of interest, ili kama kuna eneo nitakua 'biased' basi wajumbe mniuie radhi. Mimi ni Mtanzania muumuni wa dini ya kikristo. Nimekua mkristo kwa maisha yangu yote. Lakini pia ni muumini mkubwa wa haki, demokrasia na falsafa ya 'secular state'.

Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa nchi yetu ya Tanzania ina tatizo la 'mfumo kristo', tatizo ambalo mizizi yake mirefu ilianzia kwenye utawala wa mkoloni ikiwa ni pamoja na mfumo wa elimu waa wamishonari (vitangulizi vya ukoloni).

Hata rais mstaafu wa awamu ya tatu hayati Ben Mkapa alikiri kwenye kitabu chake cha 'My Life My Purpose' juu ya tatizo hili na jinsi lilivyochangia kuwadidimiza ndugu zetu waislam, kama inavyoonekana kwenye ukurasa niliouambatanisha hapo chini.

View attachment 1537659

Kutokana na mfumo huu, kumekua na tofauti kubwa ya namna viongozi wa nchi ambao ni wakristo wanavyotendewa ukilinganisha na wenzao ambao ni waislam.

Mfano mdogo tu ni hiki tunachokiona kwenye awamu hii ya mheshimiwa rais Magufuli, mara kwa mara amekua akiyageuza madhabahu ya makanisa kuwa 'platform' ya kufanyia siasa kwa kisingizio cha 'kumtanguliza Mungu mbele', kama hiyo haitoshi kila akienda kwenye ibada basi kurugenzi ya mawasiliano ikulu inaifanya hiyo kuwa habari rasmi ya kitaifa. Yaani ibada ambayo ni jambo la kibinafsi la Magufuli linageuzwa kuwa tukio rasmi la 'Rais Magufuli'.

Angalau basi jambo hili lingekua linafanyika kwenye siku chache maalumu kama vile krismas au pasaka, lakini hii imekua routine ya kawaida kabisa ya kiongozi wa nchi ambayo inapaswa kuwa haina dini bali ina wananchi wenye dini zao mbalimbali.

Hebu tujiulize na tuwe wakweli, kama rais Magufuli angekua muislam na angekua anayafanya haya misikitini kila ijumaa hali ingekuaje? Bila shaka mabaraza yote ya maaskofu yakiongozwa na TEC yangekua yamemkalia kooni na kumkosoa vikali, angeitwa kila aina ya majina kama vile 'mujahedeen' na kadhalika. Angekumbushwa na kila mtu kuwa nchi hii haina dini.

Lakini kwakua ni mkristo basi woote kwa unafiki mkubwa wako kimya, kwasababu mfumo umewafundisha kuwa hii ndio hali ya kawaida.

Pia tujiulize, salamu za kidini zina ulazima gani kwenye shughuli za kiserikali? Sikumbuki kuwahi kumsikia Mzee Mkapa akisalimia watu 'Bwana Yesu asifiwe', au 'As-salaam aleikum', au 'Bwana apewe sifa'. Sio kwamba alikua hamjui Mungu, lahasha! Mzee Ben alilelewa na kusomeshwa na waseminari kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la 12, na aliendelea kuwa muumini madhubuti wa kanisa katoliki kwa maisha yake yote. Kama hiyo haitoshi, baba yake mzazi alikua katekista! Lakini kama kiongozi wa nchi alielewa maana ya 'secular state'. Mambo yake binafsi ya kanisani aliyaacha kanisani, alipokuja mbele ya watanzania alikuja kama kiongozi wa watanzania wote.

Ni haki ya kikatiba ya rais Magufuli kuabudu na kufuata dini anayoitaka, lakini sio sawa kuyafanya mambo yake binfsi ya kidini kuwa mambo ya kitaifa na kiserikali. Hata watumishi wa umma wanazuiwa kufanya hivyo, lakini kutokana na mfano mbaya anaounesha mheshimiwa rais ndio maana haishangazi kuwaona askari wa jeshi la polisi huko Mbalizi Mbeya wakipiga maombi kituoni tena wakati wa saa za kazi wakiwa ndani ya uniform.

John 8:32
"And you will know the truth, and the truth will set you free"
Message sent and delivered
Nafikiri watu wengi tu hawakubaliani na tabia ya rais kugeuza mimbari za kanisa kuwa majukwaa ya kisiasa. Ni makosa yake kama yalivyo makosa mengi mengine anayotenda kila wakati.
 
Zipo sababu za msingi kwa nini watoto wa kiislamu walikuwa wachache shuleni wakati wa utawala wa kikoloni. Kwanza wakoloni wa kizungu walitaka kila muafrika adharau vitu vyote visivyotokana na wazungu na kuheshimu vitu vyotrvvinavyotokana na wazungu. Hivyo walibeza adharani dini za asili na uislam. Waislam wengi walichukizwa na tabia hiyo mbaya ya ubaguzi, kudhalilishwa, kudhihakiwa, kufedheheshwa na kudharauliwa. Hivyo hawakuwa tayari kupeleka watoto wao shule ili wasitiwe najisi, wasirubuniwe na kulishwa haramu na kubadilishwa dini. Tulipopata uhuru serikali ya awamu ya kwanza chini ya mwalimu Nyerere aliona jamii ya waislam wakiwa nyuma kuelimu na hawana mwamko wa kupeleka watoto wao shule kwasababu ya hofu ya watoto wao kubadilishwa dini. Ndipo akaamua kutaifisha shule za misheni na kuzifanya za serikali. Pia hakavhukua hatua ya kupandisha alama za ufaulu kwa mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Mbeya mikoa ambayo ilikuwa na watoto wengi katika shule za serikali na kushusha alama za ufaulu katika mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi Mtwara n.k mikoa iliyokuwa nyuma kielimu ili watoto wa kislamu wapate elimu. Serikali za awamu zilizofuatia ziliendelea kufanya hivyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom