Anachoona kanji na tunacho ona mashabiki ni vitu tofauti kabisa

Mleta mada yuko sahihi kabisa. Wewe ndio huzielewi hizo odds. Ukiwa na odds kubwa kuliko mpinzani bila kujali uko nyumbani au ugenini maana yake una nafasi ndogo ya kushinda kuliko mpinzani.

Kuwa nyumbani inapunguza odds na sio kuwa kunaongeza odds. Ukiona uko nyumbani na bado kanji amekupa odds kubwa maana yake ameona uwezekano wa kushinda uko mbali zaidi.Zingatia; timu yenye odds ndogo ndio yenye uwezekano mkubwa wa kushinda kwa mujibu wa kanji na anakuwa ameangalia vitu vingi.

Timu bora kama man city anapewa odds ndogo dhidi ya wapinzani wake hata akiwa ugenini , na akiwa nyumbani anapewa odds ndogo zaidi kuliko wapinzani wake ,maana yake uwezekano wake wa kushinda ni mkubwa zaidi.

Note: Mwenye odds kubwa anaweza kutoa kipigo kitakatifu kwa mpinzani mwenye odds ndogo
 
hapo kubeti ni kutupia Goals under 3.5 😂 kwa game ya Yanga.

Kwa game ya simba ni Goals over 3.5 maana Ahly lazma afe kwa goli 3 au 4 huku akirudisha moja kwa mbinde sana au atoke kapa.
 
Note: Mamelody watadhihirisha hili katika game yao na yanga. Wapaka piko lazma wachakae sana
 
kabisa tuko sawa
 
Mkuu mbona wewe ndo umechanganya files... Ukipewa odds kubwa maana yake sio favorite wa kushinda and vice versa.
Mfano. City 1.32.united 2.80 hapo mbabe ni City.
 

Mkuu mbona wewe ndo umechanganya files... Ukipewa odds kubwa maana yake sio favorite wa kushinda and vice versa.
Mfano. City 1.32.united 2.80 hapo mbabe ni City.
Kuna jambo bado hamlielewi kuhusu hizo odds na jinsi kanji anavyofanya biashara. Kuna mchangiaji hapo juu amegusia wakati mwingine kanji anaingiza watu kingi na hili linafanyika zaidi pale uwezekano wa yeyote kushinda unapokuwa unakaribiana sana na odds zinakaribiana, kwa hiyo kanji anaweza kuswitch favorite ili kuvutia watu upande ambao sio. Odds zile ambazo tofauti zake ni kubwa ndiyo zinakuwa na clear favorite.
 
Prediction zangu:

Yanga x Mamelodi [away/draw double chance]

Simba x Al Ahly [Draw]
 
Kwenye kubet hakuna ulijualo aisee
 
Karibu kwenye chama uone odds zinavyochanganya.
Hapana siyo starehe yangu hiyo ila mara chache sana nabeti nikipata hisia kali au nikiwa na taarifa za ndani na odds ziwe nzuri. Ile mechi ya Yanga walipotolewa Mapinduzi nilikuwa nina uhakika kabisa Yanga anapigwa halafu ile timu iliyocheza nayo ilipewa odds za kama 9 hivi, daaah. Dakika ya mwisho nikasita ila nilitaka kuweka kama milioni hivi. Nilijilaumu sana kwa nini sikubeti siku ile.
 
Unanikumbusha mwaka 2020 kama sikosei kulikuwa na mechi ya Aston Villa v Liverpool.

Liverpool alikuwa na odds 8 au 9 kwa sababu mhindi alijua liver hawezi kushinda ile mechi kwa vile kikosi cha wakubwa kilienda sijui Qatar kwa hiyo asilimia kubwa wakapangwa watoto.

Lakini watu kwa kujua kabisa tukajitoa mhanga kumdhamini liver. Kanji alivyoona idadi ya wanaomdhamini liver inaongezeka, akashusha sana odds hadi kufika 4 kama sikosei ili kubalansi mahesabu ya kuwalipa wabetiji endapo kweli liver atashinda.

Lakini mwisho wa matokeo Aston Villa akashinda, tukawa tukawa tumeliwa.
 
Hizo technicalities zote nazifahamu kuhusu soko kuchangia kubadilika kwa odds.. Ceteris paribus your previous statement on odds was wrong.
 
Wewe ndio huelewi na angalia huko juu ulivyocomment 'simba kuwa nyumbani ndio imechangia kupewa odds kubwa' wakati kiuhalisia ukiwa nyumbani odds zinatakiwa zipungue.

Matokeo kuwa against the odds huwezi kusema ni mtego wa kanji sababu hakuna uhakika kuwa timu zenye uwezo unaokaribiana timu favorite inapewa odds kubwa na always inashinda, na pia wewe ungekuwa bilionea maana tayari ushaujua mtego...utajitetea hutaki ubilionea kupitia kubet!

Ukweli ni kuwa mpaka odds zinapangwa kampuni za betting zinaangalia vitu vingi yaani wanafanya uchambuzi kwa undani sana, kama vile first eleven, majeruhi, mahali mechi inapochezwa, performance ya karibuni, head to head, n.k . Hivyo timu inapewa odds ndogo au kubwa kwa kucombine factors mbalimbali na sio kwamba ni mtego ingawa matokeo yanaweza kuwa kinyume na ilivyotarajiwa.
 
Kwa odds hizi yanga anapasuka simba anatoboa.
 
Unajua issue ya demand and suply invyo athili price ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…