Mleta mada yuko sahihi kabisa. Wewe ndio huzielewi hizo odds. Ukiwa na odds kubwa kuliko mpinzani bila kujali uko nyumbani au ugenini maana yake una nafasi ndogo ya kushinda kuliko mpinzani.Msome mleta mada utaona ninachosema. Mfano anasema Mamelodi ana "odds" kubwa kwa maana hiyo Yanga ndiyo "favorites", hilo linaleta mantiki kwako? Anasema Simba ana "odds" kubwa licha ya kuwa nyumbani, hivi kuwa nyumbani si ni moja ya sababu zilizomuongezea odds Simba?
Anasema kinachosemwa mtaani na anachosema Kanji ni tofauti wakati hizo "odds" alizoleta za Kanji zinaendana na kinachosemwa mtaani.
Sijui watu wanawezaje kubeti kwa usahihi huku wakiwa na kasoro katika uelewa wa jambo muhimu kama "odds".
Kuwa nyumbani inapunguza odds na sio kuwa kunaongeza odds. Ukiona uko nyumbani na bado kanji amekupa odds kubwa maana yake ameona uwezekano wa kushinda uko mbali zaidi.Zingatia; timu yenye odds ndogo ndio yenye uwezekano mkubwa wa kushinda kwa mujibu wa kanji na anakuwa ameangalia vitu vingi.
Timu bora kama man city anapewa odds ndogo dhidi ya wapinzani wake hata akiwa ugenini , na akiwa nyumbani anapewa odds ndogo zaidi kuliko wapinzani wake ,maana yake uwezekano wake wa kushinda ni mkubwa zaidi.
Note: Mwenye odds kubwa anaweza kutoa kipigo kitakatifu kwa mpinzani mwenye odds ndogo