kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Bila shaka yoyote hata Lissu mwenye hana Raha kwa Sasa maana haamini ni kwanini hajakamatwa na kuwekwa ndani mpaka Sasa hata baada ya kusema Yale aliyokuwa akiyasema kuhusu serikali wakati ikiwa nje ya nchi.
Hakuna ubishi kuwa aliposema anarudi na siku ya kurudi Tanzania alisindikizwa na vyombo vingi vya habari vya nje ili kuandika na kuripoti kile kitakachompata Lissu atakapotua Airport Tanzania.
Rais JPM amedhihirisha kuwa amedhamiria kuijenga upya Tanzania na hana sababu nyingine moyoni mwake. Ameonyesha kuwa hana nia mbaya zaidi ya kupambana na ubadhilifu, rushwa na njama za wawekezaji wabaya.
Mpaka Sasa kalamu za vyombo vingi vya habari vilivyotaka kuandika habari za lissu kurejea zimekauka wimo kwa kukosa Cha maana cha kuandika. Bahati mbaya mheshimiwa Lissu mpaka Sasa sijamsikia bado akisema kile atakachowafanyia watanzania punde atakapofika ikulu Kama atashinda uchaguzi, badala yake mpaka sasa muda mwingi anautumia kueleza alivyopigwa Dodoma.
Anasahau kuwa habari ya kupigwa kwake ziliandikwa Sana na kutangazwa Sana wakati yeye yuko nje ya nchi kwa matibabu, hivyo watu wanazifahamu sana hivyo hakuna haja ya kuwapotezea watu muda kuizungumzia Tena kirefu majukwaani zaidi ya kushukuru kwa dk moja tu Kisha atueleze namna atakavyofanya kwenye madini, utalii, kilimo, ufugaji, uvuvi, utawala bora, usalama, makazi..kwa kifupi wakati tukisubiri kampeni zianze rasmi.
Uzuri na ubaya wa Rais wao wanaufahamu Sana hata wao, hivyo asipoteze muda kuwasimulia watu ambao walikuwepo Tanzania kwa miaka yote 5 ya awamu ya tano, maana wao wanafahamu Sana kuliko yeye ambae hakuwepo nchini kwa miaka 3.
Anachotakiwa Lissu Ni atumie muda kidogo alionao kuwaambia wananchi ataifanyia Nini Tanzania akifika Ikulu.
Ukomavu huu wa serikali ya JPM umeishangaza dunia kusema ukweli, hasa wale waliotarajia mshikemshike pale Airport.