Anae kielewa kipindi kipya cha salama "ngazi kwa ngazi"

Mimi nakipenda kwakweli, Salama ni creative sana kipindi japokuwa wengi hawakielewi. Mtakielewa tu kidogokidogo.
 
Mkuu inawezekana we unamuelewa Salama ndo umeunganisha na kipindi
Aisee kwa ambavyo nakiona kile kipindi dooh ...sijakisoma kwakweli
Kuwa mpole mkuu utakielewa tu polepole
 
Mkuu inawezekana we unamuelewa Salama ndo umeunganisha na kipindi
Aisee kwa ambavyo nakiona kile kipindi dooh ...sijakisoma kwakweli
Kuwa mpole mkuu utakielewa tu polepole
 
Ule ndo ubunifu coz anatupa nyimbo ambazo uwez kufikiria kma watu wameziangalia lkn nyimbo zile n kubwa sana kwenye mataifa mengine,, n ubunifu mzur badala ya kuwahoj wasanii kma ilivyokuwa kwenye mkas sasa anawahoj kidesign kiko vizur sana.... UKIONA UMESOMA KITABU UJAKIELEWA BASI UJUE UJAANDIKIWA WW..
 
Wadau najaribu kufatilia kipindi kipya cha salama jabir "ngazi kwa ngazi" dizain naona km sikielewi elewi hivi hakina mvuto ule wa ubora wa salama au ndo uzee.....!!

Kille kipind nakipenda segment ya mchongo na vituko yaliyobaki hayanuhusu..........
 
Vipindi vingine hakuna haja ya kuvielewa unaangalia tu then unaachana nacho.
 
Salama Jabir ni mbunifu wa hali ya juu sana katika kutangaza sanaa na muziki, ngazi kwa ngazi ni kipindi cha kipekee sana, kwa watu tunaojua nini maana ya Ubunifu tunaelewa kule ambapo Salama anaelekea. Kwa sababu.

1/Hajaiga popote.
(Hakuna Tv station ambayo amewahi kuwa na aina ya kipindi kama kile)

2/Uchaguzi wa nyimbo zake unazingatia ladha mbali mbali za muziki za kila mahali duniani.

3/Ndani ya Kipindi kimoja kuna "Ideas" zaidi ya Kumi zimejificha(Kwa mfano Studio setting, Presentation Style, Music Content, Interview, Song Ranking, Jokes, Modeling, Biographies, Narrations, News, Culture, Lugha ya Kiswahili)..

Kwa kifupi kabisa, kipindi kile kimelenga Kitaifa, kimataifa na Matokeo ya Muda mrefu sana.
 
Tusisahau pia ni Salama Jabir huyu huyu aliwahi kuja na vipindi hivi ambavyo vilivuma kupita maelezo.
1/Planet Bongo.
2/Mkasi.
3/Siasa za Siasa.

Na mara zote vipindi hivyo vilivyoanza kuruka hewani, watu wengi hatukuelewa mantiki nzima, lakini baada ya muda tulielewa na kuanza kuvipenda sana.

Huwa nawaheshimu sana watu vipaji vya kubuni na kuishi katika ubuni wao.
 
Hajaiga vip mkuu?? Ile sauti inayotumika mbona kaiga B. E. T awards. Fuatilia utajua, binafsi kipindi sijakielewa nadhani hakieleweki that's why hakina mdhamini hata mmoja mpaka sasa. Mkasi b4 haijaanza kilishapata udhamini, but hiki dooh maybe soon or later nitakielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…