Anaedhani Tundu Lissu ataachiwa kwa mititi ya ndani na nje ya nchi hamtakii mema Lissu, Achunguzwe

Anaedhani Tundu Lissu ataachiwa kwa mititi ya ndani na nje ya nchi hamtakii mema Lissu, Achunguzwe

Huo uchunguzi wa kimataifa unasema mataifa yapi? Kama ni kutoka ulaya hapana, hawa ni watu wanaochochea migogoro duniani ili kuuza silaha zao na kupora rasilimali. Kama Wanashindwa kuwasuluhisha wazungu wenzao wasiuane huko Ukraine na Urusi wataweza kwetu? Hawa wazungu waliondoka kwetu shingo upande, sio wema. Hata wewe nakusihi, ugomvi wako na mkeo usiite watu wa nje wakusuluhisheni, wataondoka na mkeo.

..Tunaweza kukaa kama ndugu na tukaamua kutafuta msuluhishi anayekubalika.

..Kwa mfano, kuna Maraisi Wastaafu wa nchi za Kiafrika kama Afrika Kusini, Ghana, Botswana, Malawi, au nchi yoyote yenye mifumo imara ya Kidemokrasia.

..Kwa hapa tulipofikia, kama kweli tuna nia njema, basi tunapaswa kuleta mtu anayeheshimika awe MSULUHISHI.
 
Kuna askari walikufa pia, nani aliwaua?

Wanaoishutumu serikali kwa kuzima vurugu zile kwa aina ile wamegawanyika katika makundi yafuatayo:
1. Watu waliokasirika kwanini serikali haikuangushwa ili wao wakamate dola. kama ingeanguka maneno yangekuwa machache sana na vigelegele vingi, hata waliokufa wangesema wamekufa kishujaa.
2. Watu waliotoa pesa zao kugharamia mapinduzi yaliyoshindwa.
3. Watu waliokuwa wakitarajia kupewa vyeo baada ya serikali kuangushwa. Vyeo vimeota mbawa.
4. Wafanyabiashara ambao walitarajia kurudishiwa biashara zao haramu walizopoteza.
5. Baadhi ya Wagombea wa CCM waliokosa uteuzi wa kugombea
6. Watu ambao waumini wao walishiriki vurugu kwa maagizo yao na wakapelekewa moto.
7. Wafuasi oyaoya wa upinzani, wengi wao wavuta ndumu wanaodhani kuwa chadema ikifika ikulu itawajaza noti mifukoni mwao.

Wakati wa uchaguzi polisi wengi huwa wanalinda uchaguzi, na askari jeshi wengi huwa wanalinda mipaka. Hivyo, hakukuwa na polisi wa ziada ya kuongoza maandamano ya chadema nchi nzima hata kama yangekuwa ya amani. Hii ikasababisha hao askari wachache waliopatikana kukabiliana na vurugu za nchi nzima watumie nguvu kubwa sana kuihami nchi na miundombinu dhidi ya wafanyavurugu nchi nzima, twanga tu. Hata wewe kama utavamiwa na vibaka wengi utatumia nguvu kubwa kuliko kama ungevamiwa na kibaka mmoja tu.
Mimi najiuliza kama wale wafanya vurugu tu na hawakuwa na silaha za moto na jeshi la polisi lilikuwa limeshajipanga kabla ya siku ya tukio, lakini ikatumika nguvu kubwa kiasi kile ili kutuliza tu vurugu je vp kama wangekuwa na silaha za moto hali ingekuaje? Kama wale wafanya vurugu tu jeshi lime panic na kutumia nguvu kubwa iliyosababisha vifo vya watu wengi wasiohusika na hizo vurugu, sasa kama wafanya vurugu nao wangekuwa na silaha hali ingekuaje?
 
..Tunaweza kukaa kama ndugu na tukaamua kutafuta msuluhishi anayekubalika.

..Kwa mfano, kuna Maraisi Wastaafu wa nchi za Kiafrika kama Afrika Kusini, Ghana, Botswana, Malawi, au nchi yoyote yenye mifumo imara ya Kidemokrasia.

..Kwa hapa tulipofikia, kama kweli tuna nia njema, basi tunapaswa kuleta mtu anayeheshimika awe MSULUHISHI.
Afrika Kusini hakuna issue zaidi ya kuwafukuza waafrika wenzao na kuwaacha wazungu na wahindi.
 
Nikiri kwamba mara hii natumia MOYO badala ya UBONGO kuandika uzi huu.

Mashinikizo ya ndani na nje ya nchi hayawezi kuifanya Tanzania ipindisje au iachane na Katiba yake, sheria, mila, taratibu na utamaduni wake wa kuliendesha taifa letu. Hakuna mtiti wa nje wala wa ndani unaoweza kumuondolea Lissu makosa yake kwa mujibu wa sheria zetu. Ila sisi wenyewe tunaweza kumuondolea na kumsamehe makosa yoyote mwananchi wetu kwakutumia Katiba na sheria zetu.

Tufanye kila kitu Lissu awe huru mitaani kwa kutumia njia zetu wenyewe za kitanzania ili Taifa lijikite kwenye mambo mengine muhimu pia.

Hakuna ubishi kuwa Tanzania ilichomwa moto hata leo hii magofu bado yapo, na hakuna sheria Tanzania inampa mtu excuse ya kuchoma mali ya umma na mali za wenzake wasiokuwa na hatia.

Hakuna ubishi Tanzania hatuna sheria inayoruhusu mtu mmoja au kikundi kuzuia uchaguzi Mkuu unaotupa viongozi wakuu wa nchi usifanyike. Kufanya hivyo ni sawa na kuvunja Katiba na uhaini baridi. Uhaini baridi kwakuwa muda wa viongozi kukaa madaraki kwa mujibu wa Katiba ni miaka 5. Hivyo kuzuia uchaguzi usifanyike ni kumaanisha ama nchi iongozwe na watu waliomaliza muda wako Kikatiba au nchi ibaki bila kuwa na viongozi.

Hata hivyo, kama utatafakari vizuri ukiwa umetulia utabaini kuwa Lissu ameshinikizwa tu na baadhi ya wanaCCM, wafanyabiashara na makundi ya kidini kutamka na kutenda alichokitenda kwa kushawishiwa na kuaminishwa kuwa anaweza kuwa Rais kwa msaada wao. Walimshinikiza na kumsaidia Lissu ampore Mbowe chadema kwa nguvu ili chadema waitumie kama farasi wa vita/mwamvuli/jukwaa tu kwenye mpango wao.

Watu waliomsukumiza Mh. Lissu kwenye sekeseke hili wenyewe wako huru mitaani wanadunda; na ndiyo wanaohanikiza kelele za Tundu Lissu aachiwe huru; they feel guilty kumuona Lissu waliyemsababishia shida yuko gerezani. Waliosukumiza Lissu ndiyo hao wanaohangaika na vyombo vya habari vya nje, EU, Jumuiya ya madola na hata ICC kuomba msaada Lissu atoke na nchi inyimwe misaada ili wananchi wa kawaida wakose huduma kama chanjo na dawa za misaada. Hawajali nini kitatokea kama nchi itanyimwa misaada.

Baada ya Lissu kukaa ndani ya gereza, Mh. Heche, Makamu Mwenyekiti nae akashangalia usemi wa wahenga wa "kufa kufaana". Heche sasa amekuwa maarufu ndani na nje ya nchi kwa kisingizio cha kutaka kumtoa Lissu kwa kutumia mititi ya ndani na nje ya nchi. Hii mititi ndiyo biashara yake kuu kwakuwa ili mititi hii iwepo ndani na nje yanchi inahitaji fedha nyingi za kuendesha mikutano, usafiri, malazi, chakula na matumizi yake na familia. Anaomba hela kwa kila mtu ili kufanikisha kumtoa Lissu kwa mititi. Hata hivyo mititi hii haileti matokeo ya haraka ya kumtoa Lissu; na off course, haiwezi kufua dafu. Fedha hizo hazina mahesabu ya uhakika maana zinaenda mfukoni kwa wajanja moja kwa moja.

Waliomsukumiza Lissu kwenye janga; yaani wale wanaCCM (kijani) na wanadini sasa hivi wamemgeuka Heche, wanataka atoke ili njia ya maridhiano itumike kumtoa Lissu nje; njia yake yakutumia mititi anathibitiwa na Katambi, na EU, Jumuiya ya madola, ICC na wengine huko nje wanaonekana hawana cha maana wanafanya ili Lissu atoke. Sasa hivi wanataka kumtoa Heche kafara kupitia wanachadema wenyewe ili njia za kawaida za ndani ya nchi za maridhiano zitumike kumtoa Lissu nje awe huru. Sasa hivi tuhuma za Heche kala pesa zimepambamoto kila kona ya chadema, bahati mbaya tu wanakosea kuisingizia serikali ya CCM ya samia kuwa ndiyo inayowapa pesa waseme kuhusu Heche.

Naomba taifa kwa kutumia Mama Samia, Rais wa Tanzania na DPP wakae kitako watete wamtoe LIssu nje kwa njia zetu, utashi wetu watanzania chini ya katiba yetu, sheria zetu na uhuru wetu kuionyesha dunia kuwa tanzania haifundishwi namna ya kulinda nchi yetu, kuwahudumia watu wetu na kudumisha amani na utulivu sio tu kwa watu wetu bali hata kwa wanyama wetu wa kufungwa na wa porini.

Lissu kuwa ndani hatupati faida yoyote, lakini kama akikosea tena tutamkamata tena kama raia mwingine kwa kosa lake hilo jipya.

Mungu ibariki Tanzania

Pia soma: Heche hataki Lissu atoke, anachekelea umaarufu wa kufa kufaana
Kwani mbowe ilikuwaje?
Alitokea gerezani Moja kwa Moja ikulu
Wewe.umekaa hapo unapika majungu ya kipumbav kama mwehu
 
Back
Top Bottom