Anaejua sakata la jamaa wa Kigamboni waliojiunganishia bomba la mafuta liliishia wapi atujuze

Anaejua sakata la jamaa wa Kigamboni waliojiunganishia bomba la mafuta liliishia wapi atujuze

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
4,618
Reaction score
4,605
Kuna mambo huwa yanapita bila kuhojiwa japo huwa yanazunguka kwenye vichwa vya watu.

Mojawapo ni jamaa waliounga bomba la mafuta la kigamboni hii issue ni ya uhujumu uchumi japo ni kama iliisha kirahsi rahsi kwa mtazamo wangu. Nitafurahi kama kuna anaejua hili nalo liliishaje.

Ama ukiona hili gumu tujuze tu matokeo ya wale jamaa wa hazina waliojichotea hela kama vile hazina haina mwenyewe nitashukuru.
 
Kuna mambo huwa yanapita bila kuhojiwa japo huwa yanazunguka kwenye vichwa vya watu.

Mojawapo ni jamaa waliounga bomba la mafuta la kigamboni .hii issue ni ya uhujumu uchumi japo ni kama iliisha kirahsi rahsi kwa mtazamo wangu. Nitafurahi kama kuna anaejua hili nalo liliishaje.

Ama ukiona hili gumu tujuze tu matokeo ya wale jamaa wa hazina waliojichotea hela kama vile hazina haina mwenyewe nitashukuru.
"Mama aliupiga mwingi" toka mwanzo na sasa tunaona unavyoendelea kuwa "mwingi"

Nami ningependa kujua yule binti DC aliishia wapi?

Huenda tukijua alipo sasa tunaweza kuanza kujenga hoja juu ya hii mada.

Mkuu 'Escrowseall', nikushukuru kwa kumbukumbu zako hizi. Mimi nilianza kulishangaa hili jambo lilivyochukuliwa toka mwanzo, na kama kawaida ya waTanzania, hakuna alieshtuka, na sasa wala hakuna anayekumbuka kama swala hilo liliwahi kutokea na kunyamaziwa kabisa.

Na pengine hadi leo mradi huo unafanya kazi kama kawaida, maanake hatukuona mabomba yaking'olewa!

Pengine huu ulikuwa ni mradi wa mama mwenyewe, maana alivyolichukua inashangaza sana.

Na haya mahela tunayowapigia kelele akina Mwigulu, si nawe ulisikia "STUPID"?

Hizi ndiyo njia mpya za kushughulikia haya maswala ya uhujumu. Sema neno moja ukionyesha hasira, halafu nyamaza, acha waTanzania wasahau. Ikifika 2025, hakuna atakayekumbuka chochote, hadithi ni za kupamba tu, kama tunavyoona sasa mabango kila sehemu za miji.

Nchi ya ajabu sana hii.
 
Bongo issue zote ni hela tu... just few months baada ya kusikia hiyo jamaa alimalizana na serikal na "bus zikabadil majina" oh sorry akauza kampuni
Na wanaojiita waandishi wa habari wala hawana kumbukumbu yoyote.

Wenye magazeti yao na wao habari kama hizi haziuzi kama wanavyoneemeka na wanayoyapata toka serikalini na kwa hao wahujumu wenyewe.

Ni sahihi kabisa na wao kuwajumuisha kwenye kundi hilo la uhujumu.
 
Mama kaingiaje wakati ilikuwa kipindi cha Magufuli?
Usilete ubishi hapa usiokuwa na maana yoyote.

Ndiyo, wizi ulifanyika awamu ya tano, ukagundulika awamu ya sita ambayo ndiyo ilitakiwa ichukue hatua.
 
Kapuku Na Sakara Ndiyo Watakaopata Tabu Sana Sana Tanzania
 
Kuna mambo huwa yanapita bila kuhojiwa japo huwa yanazunguka kwenye vichwa vya watu.

Mojawapo ni jamaa waliounga bomba la mafuta la kigamboni hii issue ni ya uhujumu uchumi japo ni kama iliisha kirahsi rahsi kwa mtazamo wangu. Nitafurahi kama kuna anaejua hili nalo liliishaje.

Ama ukiona hili gumu tujuze tu matokeo ya wale jamaa wa hazina waliojichotea hela kama vile hazina haina mwenyewe nitashukuru.
Inaonekana unataka kujua kama watanzania bado wanafuatilia kesi yako?haya hongera baba umeshinda!
 
Usilete ubishi hapa usiokuwa na maana yoyote.

Ndiyo, wizi ulifanyika awamu ya tano, ukagundulika awamu ya sita ambayo ndiyo ilitakiwa ichukue hatua.
ndugu kama jambo hulijui niheri kutulia kuliko kujifanya mjuaji halafu ukajiweka wazi hili jambo liliishia kipindi cha mwenda
 
Back
Top Bottom