Anaejua sakata la jamaa wa Kigamboni waliojiunganishia bomba la mafuta liliishia wapi atujuze

Anaejua sakata la jamaa wa Kigamboni waliojiunganishia bomba la mafuta liliishia wapi atujuze

Kuna mambo huwa yanapita bila kuhojiwa japo huwa yanazunguka kwenye vichwa vya watu.

Mojawapo ni jamaa waliounga bomba la mafuta la kigamboni hii issue ni ya uhujumu uchumi japo ni kama iliisha kirahsi rahsi kwa mtazamo wangu. Nitafurahi kama kuna anaejua hili nalo liliishaje.

Ama ukiona hili gumu tujuze tu matokeo ya wale jamaa wa hazina waliojichotea hela kama vile hazina haina mwenyewe nitashukuru.
Mkuu wa kaya wa wakati huo anajua.
 
Haya ndugu ✏️,Kalamu na tukupe homework tutafute mwendelezo wa jambo hili ili wote tusiwe wakilalamika na kusahau,ikikupendeza tuanzie na alipo ndugu Dc, ikipendeza na iliyokuwa kamati yake wakati huo.Japo watatupa dira ya uelekeo wa jambo lenyewe🤔
Wewe huoni tayari ninatimiza wajibu wangu hapa?
Fanya hiyo kazi wewe usiyekuwa na kazi yoyote. Acha uzembe.
 
Kalamu upo sawa lkn?
Nipo sawa kabisa wala sina shaka juu ya hili.
Wizi ulifanyika wakati wa Magufuli, tukio la kugundulika wizi huo ni wakati wa Samia na wala hakutoa neno lolote kuhusu jambo hilo, hadi leo.

Yaani lilifukiwa kwa maksudi kabisa lisizungumziwe, na kwa kweli ikawa hivyo.

Inaelekea hii ndiyo staili yake ya uongozi. Na ni hivi hivi ndivyo anavyoruhusu nchi kuhujumiwa.

Jambo la namna hii kufukiwa tu, na wala haijulikani kama kuna juhudi zozote za kusitisha wizi huo hadi sasa? Na wala wahusika kutojulikana kabisa?

Hii si kawaida hata kidogo.
 
Tuendelee kulalamika hadi tuzeeke.
Wajukuu zetu watakuja kuchukua hatua
Unajua?
Kulalamika ni sehemu ya kuchukua hatua.
Matukio makubwa na mageuzi hupitia hatua ya kulalamika.

Ni lipi lililo nafuu kidogo, kulalamika au kukaa kimya?
 
Kuna uwezekano mkubwa hii taasisi ya kutoa haki imeamua kufanya kila Jambo linalohusu utoaji wa haki kama Mali Yao MAAMUZI mengi ni kwa maslahi Yao binafsi. Hivi hizo Mahakama mnazielewa kweli? au ni kizazi hiki?
 
Nipo sawa kabisa wala sina shaka juu ya hili.
Wizi ulifanyika wakati wa Magufuli, tukio la kugundulika wizi huo ni wakati wa Samia na wala hakutoa neno lolote kuhusu jambo hilo, hadi leo.

Yaani lilifukiwa kwa maksudi kabisa lisizungumziwe, na kwa kweli ikawa hivyo.

Inaelekea hii ndiyo staili yake ya uongozi. Na ni hivi hivi ndivyo anavyoruhusu nchi kuhujumiwa.

Jambo la namna hii kufukiwa tu, na wala haijulikani kama kuna juhudi zozote za kusitisha wizi huo hadi sasa? Na wala wahusika kutojulikana kabisa?

Hii si kawaida hata kidogo.
Miaka nenda rudi kigamboni hiyo michongo ipo,na haiwezi kuisha

Ova
 
Miaka nenda rudi kigamboni hiyo michongo ipo,na haiwezi kuisha

Ova
Hapana. Haiwezekani kukubaliana dhana yako hii. Kuishi ni kupambana siku zote, 'for or against
Nyie mnaoona hivyo ndvyo bora kwenu, tuacheni nasi upande wa pili tukatae hayo mnayoyataka nyinyi.'
 
Mwenye pesa hafungwi ,Plea bargain iliwapenda zaidi wakamalizana na DIPIPII.
 
Tatizo hakuna Freedom of Information Act
Naona hili ni muhimu sana na ukihitaji kujua lolote lazima upate information zote

Kwa waafrika ni ngumu sana
 
Unamzungumzia Muro sio,

Alilipa Plea bargain akamalizana na serikali
Tena alilipishwa sh 100m! Ukweli ni kubwa yule aliyangulizwa mbele, lakini wahusika wakuu ni kampuni moja yenye vituo vya mafuta nchi nzima ikitumia rangi ya blue.
 
Back
Top Bottom