Kuna mambo huwa yanapita bila kuhojiwa japo huwa yanazunguka kwenye vichwa vya watu.
Mojawapo ni jamaa waliounga bomba la mafuta la kigamboni .hii issue ni ya uhujumu uchumi japo ni kama iliisha kirahsi rahsi kwa mtazamo wangu. Nitafurahi kama kuna anaejua hili nalo liliishaje.
Ama ukiona hili gumu tujuze tu matokeo ya wale jamaa wa hazina waliojichotea hela kama vile hazina haina mwenyewe nitashukuru.
"Mama aliupiga mwingi" toka mwanzo na sasa tunaona unavyoendelea kuwa "mwingi"
Nami ningependa kujua yule binti DC aliishia wapi?
Huenda tukijua alipo sasa tunaweza kuanza kujenga hoja juu ya hii mada.
Mkuu 'Escrowseall', nikushukuru kwa kumbukumbu zako hizi. Mimi nilianza kulishangaa hili jambo lilivyochukuliwa toka mwanzo, na kama kawaida ya waTanzania, hakuna alieshtuka, na sasa wala hakuna anayekumbuka kama swala hilo liliwahi kutokea na kunyamaziwa kabisa.
Na pengine hadi leo mradi huo unafanya kazi kama kawaida, maanake hatukuona mabomba yaking'olewa!
Pengine huu ulikuwa ni mradi wa mama mwenyewe, maana alivyolichukua inashangaza sana.
Na haya mahela tunayowapigia kelele akina Mwigulu, si nawe ulisikia "STUPID"?
Hizi ndiyo njia mpya za kushughulikia haya maswala ya uhujumu. Sema neno moja ukionyesha hasira, halafu nyamaza, acha waTanzania wasahau. Ikifika 2025, hakuna atakayekumbuka chochote, hadithi ni za kupamba tu, kama tunavyoona sasa mabango kila sehemu za miji.
Nchi ya ajabu sana hii.