kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Inafahamika kuwa 4Rs zilimnyanyua juu juu juu zaidi kimataifa Rais Samia kwenye nyanja ya demokrasia. Hii inaweza kuwa chanzo cha hasira kwa wale wote waliokuwa wakisema hataweza.
Bwawa limekwisha, SGR anabeba watu, madaraja yanamalizika kujengwa, barabara za mabasi ya haraka vumbi linatimka kila kona Dar es Salaam, kodi ya kistaarabu inakusanywa, mikopo na misaada inamiminika kila uchao, nchi haina njaa, ndege zinaruka na kutua, bandari inachapa lapa, mabasi yanasafiri hata usiku, hospitali tunaziona, umeme unawaka nchi nzima, wanafunzi wanakwenda shule bila kelele za kucheleweshwa mikopo. Atakaepinga asigombee 2025 atasema nini, atadai nini, ataleta hoja gani? Atasema ni mdini? atasema ni mla rushwa? Atasema miradi hakumaliza? atasema ni mwanamke? au atasema ni Mzanzibar?
Critical thinkers watajua kuwa Hakuna serikali inayoteka raia wake hadharani, kuwaua na kuwatupa sehemu za wazi ili watu waone na kuwapandisha hasira. Hakuna kiongozi wa serikali ambae anaweza kusema hadharani kuwa serikali iliingia madarakani kwa kuiba kura na kuengua wapinzani hata kama hayo yalifanyika kweli. Hizi zinawezakuwa hujuma kwa serikali hii ili "aonekane" hafai kimataifa na ndani ya nchi kuelekea 2025, yaani wanamsagia kunguni usoni ili anuke.
Sisi tuliosomea Cuba tutahitaji uchunguzi wa kina kwenye mambo ya nchi badala ya kukimbilia kunyooshea serikali kidole moja kwa moja.