Binafsi nadhani mleta mada ndiye anaweza kuwa anachanganyikiwa. Kwa maisha yalivyo magumu hivi, mtu ambaye hana ajira, ana zunguka vijiweni kutafuta riziki unamuona kachanganyikiwa? Kama ukoo wenu mgekuwa na Hospitali mkamuajiri kisha akakataa, ningemuona mwehu. Nyie hamna ajira, ila ni watoa ushauri tu, Kaomba MD program hajapata, labda hana qualifications za kutosha, na Je akipata MD program mnaweza kumsomesha au anapesa ya kijisomesha au itakuwaje tena?
Huyu ni kijana anajitafuta, msibeze mawazo yake, mimi namuelewa sana. Kwa ufupi hizo course za mionzi, Radiology Techician zinalipa kwenye mazingira yetu, na malipo yake zaidi ni Rushwa. Watu wengi uhitaji huduma hizo, na hawazipati kirahisi, hivyo kuongeza mianya ya rushwa kwenye maeno zinapotolewa huduma hizo.Hivyo kuwafanya ma Radiology Technicins kupiga pesa nyingi nje ya mishahara yao. Kinachotafutwa ni pesa, career ni ubishoo tu siku hizi.
Akifanikiwa kusoma na akapata kazi, huyo mnaweza msimsikie kabisa., kwa vijipesa vya kuishi hizo course zina lipa sana hospitalini mwacheni akasome, kama hamna njia ya kumsaidia kufanya MD.