Anakatazwa kutoka ndani!!

Anakatazwa kutoka ndani!!

Halafu ukizingatia na wazazi wa huyu binti waliishamwambia huyu jamaa kuwa binti yao ni jeuri pindi akileta za kuleta amshikishe adabu sasa sijui kwanini jamaa anakuwa muoga na mpole kiasi hicho mpaka mwanamke amempanda kichwani anywayz haya mambo ya ndani ya nyumba huwezi kujua ni kitu gani hasa kilichopo humo natamani sana huyo hausigeli angeongea maana atakuwa anajua mambo mengi sana yanayotendeka humo ndani

Mambo ya kiduku hayo yamemchanganya
 
Kuna wanaume wengine kwa wake zao kama majibwa koko hawafurukuti anaweza kudwa hivi hivi mbele za watu na akanywea.

Kuna siku nililikuwa nakunywa sebuleni na jamaa mmoja wa pale pale kitaa sasa jamaa story zimenoga mke wake akawa anamuhitaji nyumbani alikubwa amebanwa na hamu akatuma mtoto mara kwanza jamaa akasema nakuja baada ya dk.5 akarudi tena mtoto jamaa akasema nakuja zikapita dk.10 mama yule akaongozana na mtoto huku yeye akawa amejificha gizani akamwambia kamwite mtoto akaenda jamaa akasema mwambie nakuja yule mama akatoka huko gizani mpaka kwa jamaa akachukua bilauri ya kilaji akamwaga akamwambia nimekwambia nyumbani jamaa akawa mpole wkt pale pale alikuwa anapiga story jamaa ake anavyo nyanyaswa na mke wake basi jamaa huyoo akainuka kama kondoo. Mi nilicheka mpaka nikaharibu beer zangu kwa kucheua dah.

Fidel mambo mazito hayo, omba yasikukute, wanaume wengi ni tu wasiri sana!
 
Aku ukanifidq goti yangu maana jana ulivyoshabikia??? halafu kwa nini nimtafute DA na wakati wewe upo, au na wewe domo zito?

Ha ha ha Gaga bana bado unakumbuka goti yako kwa Fidel?? Usiogope unajua mie ndo sponser wake so kila kitu akitaka kufanya lazima aombe ruhusa kwangu
 
Heshima wakuu...
Kuna jamaa yangu ambaye tumekuwa pamoja nikiwa na maana michezo ya utotoni na shule ya msingi pia tumesoma darasa moja kule kijijini kwetu. Amekuwa kama ndugu maana ndiye alinipokea hapa mjini kabla sijaanza kujitegemea. Matatizo yalianza alipooa, baada ya miezi kama sita hivi nilipigwa marufuku na mkewe nisiwe na mazoea na huyu jamaa eti namtafutia wanawake, pindi tunapotoka pamoja hasa siku za wikendi. Kuepusha mgogoro nikaacha kwenda nyumbani kwa jamaa na kama kuna shida ya muhimu namuibukia ofisini kwake. Si mimi tu, bali marafiki wote wa karibu wa jamaa walipigwa mkwara kama mimi.
Ishu ni juzi huyu jamaa kaja kuniomba ushauri amfanye nini mkewe maana kero zimezidi, akichelewa kurudi kazini ni zogo, na akirudi haruhusiwi kutoka labda atoe sababu za msingi kwa nini anatoka na ikiwezekana wanatoka wote. Kifupi jamaa hana sauti mbele ya mkewe.
Nilimshauri jamaa hii ishu aifikishe kwa wazee akianza na mshenga, kabla ya kuchukua uamuzi. Mke wa jamaa ni mama wa nyumbani.
Nimeileta hapa ili tupate uzoefu kutoka kwa wataalamu wa mahusiano na mapenzi huenda tukapata uzoefu kwa waliowahi kupata mkasa kama huu.
Nawasilisha...

ndoa iliyofungwa na mungu na isiingiliwe,
nyinyi mwaitakia nini, hata kama mwanaume anapiga deki,anakatazwa kutoka,
wewe inakuhusu!
hayo mambo ni ya wana ndoa wenyewe, sasa wewe wa pembeni kinachokuwasha ni nini?
Ulitaka maisha ya wanandoa wote yafanane?imekuwa sare ya shule hiyo?
 
Halafu ukizingatia na wazazi wa huyu binti waliishamwambia huyu jamaa kuwa binti yao ni jeuri pindi akileta za kuleta amshikishe adabu sasa sijui kwanini jamaa anakuwa muoga na mpole kiasi hicho mpaka mwanamke amempanda kichwani anywayz haya mambo ya ndani ya nyumba huwezi kujua ni kitu gani hasa kilichopo humo natamani sana huyo hausigeli angeongea maana atakuwa anajua mambo mengi sana yanayotendeka humo ndani
Licha ya jamaa kulazwa sebuleni pia siku nyingine wakikorofishana mke anaenda kulala chumba cha house girl!!
 
ndoa iliyofungwa na mungu na isiingiliwe,
nyinyi mwaitakia nini, hata kama mwanaume anapiga deki,anakatazwa kutoka,
wewe inakuhusu!
hayo mambo ni ya wana ndoa wenyewe, sasa wewe wa pembeni kinachokuwasha ni nini?
Ulitaka maisha ya wanandoa wote yafanane?imekuwa sare ya shule hiyo?
Hatuingilii, jamaa mwenyewe kaomba ushauri baada ya kuona mambo yanamshinda!
 
ndoa iliyofungwa na mungu na isiingiliwe,
nyinyi mwaitakia nini, hata kama mwanaume anapiga deki,anakatazwa kutoka,
wewe inakuhusu!
hayo mambo ni ya wana ndoa wenyewe, sasa wewe wa pembeni kinachokuwasha ni nini?
Ulitaka maisha ya wanandoa wote yafanane?imekuwa sare ya shule hiyo?

Hee??? Umetokea wapi wewe?? Au inawezekana ndo wewe huyo jamaa maana ulivyosema kwa ..................kama imekuuma vile
 
ndoa iliyofungwa na mungu na isiingiliwe,
nyinyi mwaitakia nini, hata kama mwanaume anapiga deki,anakatazwa kutoka,
wewe inakuhusu!
hayo mambo ni ya wana ndoa wenyewe, sasa wewe wa pembeni kinachokuwasha ni nini?
Ulitaka maisha ya wanandoa wote yafanane?imekuwa sare ya shule hiyo?

Pole kaka bacha
 
Licha ya jamaa kulazwa sebuleni pia siku nyingine wakikorofishana mke anaenda kulala chumba cha house girl!!
Aisee Katavi huyu mwanamke anahitaji kuwekwa sawa na tena kuwekwa sawa haswa maana inakoelekea jamaa atakuwa anambiwa ikifika saa 12 jioni uwe umeishafika nyumbani.
 
Ha ha ha Gaga bana bado unakumbuka goti yako kwa Fidel?? Usiogope unajua mie ndo sponser wake so kila kitu akitaka kufanya lazima aombe ruhusa kwangu

Hivo eee yaani mpaka tupitie kwako ndio akatufidq?? haya ngoja nirudi loliondo DA naenda kazia na dozi ya babu maana ile kila tatizo hata kama boss wako hakupendi ukirudi tu unakuta anakukenulia meno
 
Hivo eee yaani mpaka tupitie kwako ndio akatufidq?? haya ngoja nirudi loliondo DA naenda kazia na dozi ya babu maana ile kila tatizo hata kama boss wako hakupendi ukirudi tu unakuta anakukenulia meno

Haya nitakuja kukupokea my dear
 
Jamaa yako ana tatizo gani Katavi? Hebu chunguzen, kuna shida hapo. Na kwa sasa m'mke atakuwa na kidume kinamgonga mahali. Ni vigumu sana kwa m'mke kumfungia mmewe tena anaempenda sebulen, this means you dont need need him any more. Cha kushangaza mke hana kazi analishwa na jamaa kisha anakuwa jeuri namna hiyo anaipata wapi? Katavi mshauri jamaa aondoke home awe na makazi hata ya muda walau apate ahuen. Vinginevyo anavyozidi kushupaza shingo yatmfika makubwa ambayo yanaweza kumfanya apoteze hata maisha, hatuombi yatokee. Kwa maisha ya sasa, mtu unatakiwa nyumbani pawe ni mahali pa amani na upamisi kila unapokuwa mbali, sasa yeye jamaa nyumbani kunakuwa kama gerezani bwana? Suluhisho aondoke amwachie kila kitu,. Kama ni nyumba na mali a-assume kuwa vimengua moto! Yote ya nini? Sasa kuna haja gani ya kuishi na mke asiyekujali na kukudhamini kama mme wake. Kwanza hampendi huyo jamaa hata kidogo. Na angekuwa na kipato huyo mama jamaa angeteseka sana zaidi ya hapo. Kama anamtendea hivyo leo akiwa hana kazi, je angekuwa ana kipato si angemfanya house boy wake na nguo zote angefua na kupika pia. Hatukatai kufanya hizi kazi cc wababa ila sio kila cku kwa shinikizo la mke! Once again mpe pole sana jamaa yetu na mkumbushe kuwa "Taking action without delaying is the secret of efficiency". Au
 
Licha ya jamaa kulazwa sebuleni pia siku nyingine wakikorofishana mke anaenda kulala chumba cha house girl!!

Duh mi sihami chumbani kwangu hata arudi asubuhi shauri yake. hii ndoa ya kukomoana tu yaani mke baunca utadhani nini. sijui hata kama kwenye majambo analainika na ule wako usimfikishe kazini huendi
 
Back
Top Bottom