Huyo mwanamke anasumbuliwa na wivu. Na kikubwa zaidi ni wivu wa mapenzi ambao ni matokeo ya kukosekana kwa vitu vikuu viwili katika
nguzo za ndoa.
Ndoa ina nguzo kuu 6 nazo ni
- Kuheshimiana
- Kuaminiana
- Kushirikiana
- Kulindana
- Kusaidiana
- Kutambuana.
Nafikiri huyo mwanamke ameshindwa kumuamini mumewe au la hawakupata muda wa kutambuana.
Ili mume na mke waweze kuaminiana ni lazima kila mmoja atende vitendo vya vitakavyo onyesha kuwa, undani wake ni safi na vile vile, atende vitendo vya kukubali kuwa undani wa mwenziw, mtu ampendaye ni safi kabisa. Vitendo shurti viwe na yafuatayo.
- Huyumbishwi katika maamuzi yako
- Unatumia busara na hekima katika vitendo vyako.
- Unauelewa mshtuko na mshangao wako
- Huna swali chafu.
Kutambuana inafaa mume na mke watende matendo yenye kuonyesha kuwa wanatambuana kama vile
- Kuheshimu maamuzi ya mwenzio.
- Kuheshimu ndoa yako (usiwe na nyumba ndogo)
- Kumuona mwenzio kama wewe mwenyewe.
- Kujivunia hadhi ya mwenzio
Tafadhali washauri hawa wanadoa wazingatie mambo hayo nadhani yatanusuru hiyo ndoa.