Anakatazwa kutoka ndani!!

Anakatazwa kutoka ndani!!

Heshima wakuu...
Kuna jamaa yangu ambaye tumekuwa pamoja nikiwa na maana michezo ya utotoni na shule ya msingi pia tumesoma darasa moja kule kijijini kwetu. Amekuwa kama ndugu maana ndiye alinipokea hapa mjini kabla sijaanza kujitegemea. Matatizo yalianza alipooa, baada ya miezi kama sita hivi nilipigwa marufuku na mkewe nisiwe na mazoea na huyu jamaa eti namtafutia wanawake, pindi tunapotoka pamoja hasa siku za wikendi. Kuepusha mgogoro nikaacha kwenda nyumbani kwa jamaa na kama kuna shida ya muhimu namuibukia ofisini kwake. Si mimi tu, bali marafiki wote wa karibu wa jamaa walipigwa mkwara kama mimi.
Ishu ni juzi huyu jamaa kaja kuniomba ushauri amfanye nini mkewe maana kero zimezidi, akichelewa kurudi kazini ni zogo, na akirudi haruhusiwi kutoka labda atoe sababu za msingi kwa nini anatoka na ikiwezekana wanatoka wote. Kifupi jamaa hana sauti mbele ya mkewe.
Nilimshauri jamaa hii ishu aifikishe kwa wazee akianza na mshenga, kabla ya kuchukua uamuzi. Mke wa jamaa ni mama wa nyumbani.
Nimeileta hapa ili tupate uzoefu kutoka kwa wataalamu wa mahusiano na mapenzi huenda tukapata uzoefu kwa waliowahi kupata mkasa kama huu.
Nawasilisha...
Mkuu kwa jinsi inavoonekana kati ya wanaume wapumbavu kabisa ni huyu rafiki yako... kampe ujumbe huo!!! Hata mumpe ushauri gani kama hatojitambua kuwa yeye ni mpumbavu hatotatua hilo tatizo lake!!!:smash:
 
Duh mi sihami chumbani kwangu hata arudi asubuhi shauri yake. hii ndoa ya kukomoana tu yaani mke baunca utadhani nini. sijui hata kama kwenye majambo analainika na ule wako usimfikishe kazini huendi[/QUOTE]
Ahaaa ahaaa ahaaa lol..wewe Gaga wewe
 
Jamaa yako ana tatizo gani Katavi? Hebu chunguzen, kuna shida hapo. Na kwa sasa m'mke atakuwa na kidume kinamgonga mahali. Ni vigumu sana kwa m'mke kumfungia mmewe tena anaempenda sebulen, this means you dont need need him any more. Cha kushangaza mke hana kazi analishwa na jamaa kisha anakuwa jeuri namna hiyo anaipata wapi? Katavi mshauri jamaa aondoke home awe na makazi hata ya muda walau apate ahuen. Vinginevyo anavyozidi kushupaza shingo yatmfika makubwa ambayo yanaweza kumfanya apoteze hata maisha, hatuombi yatokee. Kwa maisha ya sasa, mtu unatakiwa nyumbani pawe ni mahali pa amani na upamisi kila unapokuwa mbali, sasa yeye jamaa nyumbani kunakuwa kama gerezani bwana? Suluhisho aondoke amwachie kila kitu,. Kama ni nyumba na mali a-assume kuwa vimengua moto! Yote ya nini? Sasa kuna haja gani ya kuishi na mke asiyekujali na kukudhamini kama mme wake. Kwanza hampendi huyo jamaa hata kidogo. Na angekuwa na kipato huyo mama jamaa angeteseka sana zaidi ya hapo. Kama anamtendea hivyo leo akiwa hana kazi, je angekuwa ana kipato si angemfanya house boy wake na nguo zote angefua na kupika pia. Hatukatai kufanya hizi kazi cc wababa ila sio kila cku kwa shinikizo la mke! Once again mpe pole sana jamaa yetu na mkumbushe kuwa "Taking action without delaying is the secret of efficiency". Au

Ushauri mzuri nimecheka pale uliposema ajifanya kama vimeungua moto vile
 
Duh mi sihami chumbani kwangu hata arudi asubuhi shauri yake. hii ndoa ya kukomoana tu yaani mke baunca utadhani nini. sijui hata kama kwenye majambo analainika na ule wako usimfikishe kazini huendi[/QUOTE]
Ahaaa ahaaa ahaaa lol..wewe Gaga wewe

Inashangaza mwenzetu anapata wapi courage ya kumfanyia hayo kukewe wakati kila kitu anafanyiwa na jamaa inaonekana anamuheshimu au ndio vimzizi?mtu kama huyu ndio maana unawaza kama kwenye hiyo bold yako
 
Amelishwa ile mambo ya kudhoofisha fikra wakuu? Kama ndivyo tumweke kwenye maombi limtoke.
 
Ahahahahaaaah!! Dena mimi nina miliki baiskeli........lol...

hahaha Acha bana! We JF premium member bana - Moja wa wafadhili wa forum (afu wewe si branch manager benki Morogoro!)........anyways naona wadau wametoushauri mwingi tu...hapa sasa ni kuchambua na kumplekea ule unafikiria utamfaa!
 
Katavi naomba unijuze, ndoa yao ina mda gani na wamejaliwa kupata watoto wangapi. After ths I'll gv you an idea. Urgent
 
Huyo mwanamke anasumbuliwa na wivu. Na kikubwa zaidi ni wivu wa mapenzi ambao ni matokeo ya kukosekana kwa vitu vikuu viwili katika nguzo za ndoa.
Ndoa ina nguzo kuu 6 nazo ni
  1. Kuheshimiana
  2. Kuaminiana
  3. Kushirikiana
  4. Kulindana
  5. Kusaidiana
  6. Kutambuana.
Nafikiri huyo mwanamke ameshindwa kumuamini mumewe au la hawakupata muda wa kutambuana.

Ili mume na mke waweze kuaminiana ni lazima kila mmoja atende vitendo vya vitakavyo onyesha kuwa, undani wake ni safi na vile vile, atende vitendo vya kukubali kuwa undani wa mwenziw, mtu ampendaye ni safi kabisa. Vitendo shurti viwe na yafuatayo.
  • Huyumbishwi katika maamuzi yako
  • Unatumia busara na hekima katika vitendo vyako.
  • Unauelewa mshtuko na mshangao wako
  • Huna swali chafu.
Kutambuana inafaa mume na mke watende matendo yenye kuonyesha kuwa wanatambuana kama vile
  • Kuheshimu maamuzi ya mwenzio.
  • Kuheshimu ndoa yako (usiwe na nyumba ndogo)
  • Kumuona mwenzio kama wewe mwenyewe.
  • Kujivunia hadhi ya mwenzio
Tafadhali washauri hawa wanadoa wazingatie mambo hayo nadhani yatanusuru hiyo ndoa.
 
Katavi naomba unijuze, ndoa yao ina mda gani na wamejaliwa kupata watoto wangapi. After ths I'll gv you an idea. Urgent

Better late than never alishajibu kuwa wanamtoto mmoja na ndoa ya kikristo (kama sijakosea)
 
hee kunyimana pumzi huku jamani, huyu frnd wako anashindwa nn kutoka job na kuendelea na mambo yake mengine mpaka aende home ndio mpaka apewe ruhusa? c atoke job aunganishe na mambo yake juu kwa juu....ndoa bwana ni kuoteana tu, wengine wanasumbuliwa na wake, wengine wanasumbuliwa na waume...kingine ni kwamba huyu dada anaona raha gani mwanaume mzima kushinda nae hapo home kama hakuna ulazima? jamani kuna kujichanganya pia.
Wewe nilimiss sana posti zako. Aisee mbona umepotea sana au ndio unasaka faranga. mwenzio Zion daughter naye ametukimbia siku hizi.
 
Huyo mwanamke anasumbuliwa na wivu. Na kikubwa zaidi ni wivu wa mapenzi ambao ni matokeo ya kukosekana kwa vitu vikuu viwili katika nguzo za ndoa.
Ndoa ina nguzo kuu 6 nazo ni

  1. Kuheshimiana
  2. Kuaminiana
  3. Kushirikiana
  4. Kulindana
  5. Kusaidiana
  6. Kutambuana.
Nafikiri huyo mwanamke ameshindwa kumuamini mumewe au la hawakupata muda wa kutambuana.

Ili mume na mke waweze kuaminiana ni lazima kila mmoja atende vitendo vya vitakavyo onyesha kuwa, undani wake ni safi na vile vile, atende vitendo vya kukubali kuwa undani wa mwenziw, mtu ampendaye ni safi kabisa. Vitendo shurti viwe na yafuatayo.

  • Huyumbishwi katika maamuzi yako
  • Unatumia busara na hekima katika vitendo vyako.
  • Unauelewa mshtuko na mshangao wako
  • Huna swali chafu.
Kutambuana inafaa mume na mke watende matendo yenye kuonyesha kuwa wanatambuana kama vile

  • Kuheshimu maamuzi ya mwenzio.
  • Kuheshimu ndoa yako (usiwe na nyumba ndogo)
  • Kumuona mwenzio kama wewe mwenyewe.
  • Kujivunia hadhi ya mwenzio
Tafadhali washauri hawa wanadoa wazingatie mambo hayo nadhani yatanusuru hiyo ndoa.
Pamoja na kukubaliana na yote hajo juu kwa maoni yangu naona nguzo kuu ya ndoa ni kujamiiana. Uzoefu unaonyesha kwamba kwenye ndoa mke/mme anaweza kuboronga mambo mengi lakini inapofikia kunyimana unyumba hapo uzalendo huwa unashindikana.Ni hilo tu nilitaka kusema.
 
Heshima wakuu...
Kuna jamaa yangu ambaye tumekuwa pamoja nikiwa na maana michezo ya utotoni na shule ya msingi pia tumesoma darasa moja kule kijijini kwetu. Amekuwa kama ndugu maana ndiye alinipokea hapa mjini kabla sijaanza kujitegemea. Matatizo yalianza alipooa, baada ya miezi kama sita hivi nilipigwa marufuku na mkewe nisiwe na mazoea na huyu jamaa eti namtafutia wanawake, pindi tunapotoka pamoja hasa siku za wikendi. Kuepusha mgogoro nikaacha kwenda nyumbani kwa jamaa na kama kuna shida ya muhimu namuibukia ofisini kwake. Si mimi tu, bali marafiki wote wa karibu wa jamaa walipigwa mkwara kama mimi.
Ishu ni juzi huyu jamaa kaja kuniomba ushauri amfanye nini mkewe maana kero zimezidi, akichelewa kurudi kazini ni zogo, na akirudi haruhusiwi kutoka labda atoe sababu za msingi kwa nini anatoka na ikiwezekana wanatoka wote. Kifupi jamaa hana sauti mbele ya mkewe.
Nilimshauri jamaa hii ishu aifikishe kwa wazee akianza na mshenga, kabla ya kuchukua uamuzi. Mke wa jamaa ni mama wa nyumbani.
Nimeileta hapa ili tupate uzoefu kutoka kwa wataalamu wa mahusiano na mapenzi huenda tukapata uzoefu kwa waliowahi kupata mkasa kama huu.
Nawasilisha...
Mchunguzeni huyo mwanamke, lazima atakuwa anatembea nje ya ndoa...! Hivyo anajihami na kujijengea hali ya kuwa insecure ....! Hivyo ndivyo nionavyo mimi mkuu....!
 
Mimi naomba nitoe angalizo tu. Reading between the lines napata picha ya domestic violence.Sitashangaa kama huyu bwana huwa anapigwa na mkewe na hataki marafiki wajue na inawezekana pia ndo maana mke anajenga ukuta kati ya mmewe na marafiki/majirani. Ikiwa ni hivyo ni hatari sana maana usiombee kipigo cha mke kwa mme.Binafsi maishani mwangu nimeshuhudia matukio mengi tena sana ya domestic violence wake wakipiga waume zao na wengine hata kukaribia kuwaua.Na ukiangalia pattern ya couples hizo ni exactly kama alivyoeleza Katavi,mme kukatazwa kutoka ndani,mme kuzuiwa marafiki,mme kuzuiwa ndugu zake nyumbani na mwishowe mnashtukia mme kalazwa hospitali.I am fearing for the safety of this guy.Katavi, kama walivyosema wadau hapo juu mtumie house girl kuchunguza na kama anakung'utwa basi waeleze wazazi wa mwanaume ili hata likitokea la kutokea wawe forewarned.
 
Katavi naomba unijuze, ndoa yao ina mda gani na wamejaliwa kupata watoto wangapi. After ths I'll gv you an idea. Urgent
Ndoa huu mwaka wa tatu, wana mtoto mmoja ana mwaka mmoja na nusu.
 
Pole yake anahitaji maombi ya kufunga hili limbwata limtoke hii ni threa yangu ya kwanza kusoma ila imenitia uchungu hawa ndio wanafanya wanaume waogope kuoa, mimi kama mwanamke simfagilii kabisa huyo mama
 
Heshima wakuu...
Kuna jamaa yangu ambaye tumekuwa pamoja nikiwa na maana michezo ya utotoni na shule ya msingi pia tumesoma darasa moja kule kijijini kwetu. Amekuwa kama ndugu maana ndiye alinipokea hapa mjini kabla sijaanza kujitegemea. Matatizo yalianza alipooa, baada ya miezi kama sita hivi nilipigwa marufuku na mkewe nisiwe na mazoea na huyu jamaa eti namtafutia wanawake, pindi tunapotoka pamoja hasa siku za wikendi. Kuepusha mgogoro nikaacha kwenda nyumbani kwa jamaa na kama kuna shida ya muhimu namuibukia ofisini kwake. Si mimi tu, bali marafiki wote wa karibu wa jamaa walipigwa mkwara kama mimi.
Ishu ni juzi huyu jamaa kaja kuniomba ushauri amfanye nini mkewe maana kero zimezidi, akichelewa kurudi kazini ni zogo, na akirudi haruhusiwi kutoka labda atoe sababu za msingi kwa nini anatoka na ikiwezekana wanatoka wote. Kifupi jamaa hana sauti mbele ya mkewe.
Nilimshauri jamaa hii ishu aifikishe kwa wazee akianza na mshenga, kabla ya kuchukua uamuzi. Mke wa jamaa ni mama wa nyumbani.
Nimeileta hapa ili tupate uzoefu kutoka kwa wataalamu wa mahusiano na mapenzi huenda tukapata uzoefu kwa waliowahi kupata mkasa kama huu.
Nawasilisha...

Du! yan mama wa nyumbani ndo anamwendesha jamaa kiasi hicho! au jamaa kasha lambishwa limbwata! Unajua wanawake ni wajanja sana akitingisha kibiriti halafu kikasambaratika badala ya kitikisika basi umekwisha! wanawake wanamweshimu mtu mwenye maamuzi na msimamo, kama anaambiwa rafiki zake wasije home anakubali basi akaona mengine yote yanawezekana, cku nyingine atarukishwa kichura mbele ya watoto majirani zake! Saasa huyu jamaa kitu cha mwanzo atoe sheria za home
1. Atakua anarudi muda autakao home bila ya kufokewa,na afunguliwe mlango
2. Amtume dukan usiku halafu amfungie nje na yeye aonje tamu ya kufungiwa nje
3. Rafiki zangu wote watakuja hapo home bila kupewa bugda na mkewe
4. hata cku moja ikiwezekana amwonzeshe angalu kofi la uhakika moja tu ila ahakikishe ameanguka
5. kama hana mtoto basi yeye ale hotelini kwa wiki moja au zaidi bila ya kutoa matumizi ya home
6. hao washenga wa nini, yeye ni mwanaume na amalize matatizo yake mwenyewe kama kichwa cha nyumba! Huyu dogo vipi huyu, yaani unanikasirisha mimi wewe na huruma zako za kibazazi, utafikiri umeolewa mke bwana, be a man pls!
 
Back
Top Bottom