Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
ANAKUPENDA WEWE AU ANAPENDA UONGO WAKO? SWALI MUHIMU KUJIULIZA 😊
Yawezekana yupo kwako kwa kuvutiwa na majigambo yako uliyojivika na kuonekana mtu mwingine ila siku ukirudi uhalisia unakuwa sio yule anayemuhitaji 😔
Katika kutafuta kukubalika kuna watu hudanganya ili tu wawe kwenye hadhi ya kukubaliwa na watu fulani na mara nyingi hufanikiwa ila hayawi mafanikio ya muda mrefu.
Lengo lako ni lipi? Mafanikio ya muda mfupi au mrefu? Ukidanganya uhusika jua ipo siku utakuwa yule halisi na mambo yatakuwa mabaya ila ukiwa halisi utakataliwa na wasiostahili na kukubaliwa kwa wale walioridhika wenyewe bila shuruti.
Sio vizuri kujiweka wazi kwa asilimia kubwa ila pia sio vizuri kudanganya kwa asilimia kubwa kwa masaibu madhara yake ndio hayo unakubaliwa ukijulikana wewe ni mkurugenzi sasa siku ukianza kuombwa mahitaji ya hadhi ya mkurugenzi unaanza kulalamika kumbe wewe ndio ulijitambulisha hivyo .
#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako