Anakutafuta wakati wa shida, muweke pembeni


Upendo sio ishu ya mzazi au Mtoto. Upendo ni Amri. Hakuna cha mzazi au Nani. Mila na desturi yoyote inayovunja Kanuni ya upendo, Haki, ukweli na Akili hiyo Mila ni potofu na kikawaida zinapitwaga na Wakati.

Kijana anaweza kumtafuta mzazi lakini mzazi akawa anam-disapoint mtoto Kwa kumzingua na kumkejeli. Unafikiri Kwa uelewa wako Mtoto Hana Haki ya kuchukia.

Mtoto amekupigia simu ili akusalimie wewe unaleta mambo ya Pesa, na kuanza kumlaumu. Na Siku ukimpigia simu yeye(mtoto) hujawahi kumpigia simu ili tuu muongee , wewe kila mara ni lawama na shida. Hiyo sio Sahihi. Ni ubinafsi na ushenzi.

Hizo Mila na desturi za Afrika unazozisema nyingi zilikuwa za Zama za Giza ambazo zimepitwa na Wakati.
 
Binafsi napenda kutafutwa wakati wa shida , ninakua ninajivuna kuwa mimi ni mtatua matatzo , nilizaliwa kutatua matatizo sasa unitafute wakati una raha ili nikusaidie nini?

Kwa hiyo unapenda wenzako wakiwa na shida?
Au ndio nyie wa atakuja tuu kisa mnajua ni lazima shida impate?
 
kusalimiana mara kwa mara bila ishu ya maana nayo ni sehemu ya umbea
 
Binafsi napenda kutafutwa wakati wa shida , ninakua ninajivuna kuwa mimi ni mtatua matatzo , nilizaliwa kutatua matatizo sasa unitafute wakati una raha ili nikusaidie nini?
Hahaha
 

Kuna Ile Watu wanakupa wajibu wa kuwatembelea na kuwatafuta. Wao hawana Mpango na wewe. Alafu utasikia siku hizi hutusalimii Wakati mara zote wewwe ndiye unayewatafutaga.

Wanaitwa wazee WA kukutafutia ubaya
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Yaani unitafute wakati wa raha uniambie raha zako au niaje??

Tutafutane kukiwa na jambo la msingi, hatuna mazoea zaidi kiivo, status zimetusaidia sana. Naview zako unaview zangu. Kama zitanihusu nitareply kama hazinihusu napita kushoto hata miezi.

Hamna la kuongea mnapigiana simu ili nini kama sio kuanza kuulizana fulani yuko wapi na huyu yuko wapi.

Kausha ukiwa na shida nicheki, nikiwa nayo kama wewe ndio msaada nitakucheki tu.
Sasa nikukupq hi itakusaidia nini? Una uhaba wa watu wa kukujulia hali?

Nashukuru watu wangu wa karibu hawana desturi yq simu za hovyo hovyo. Labda kama upo kwenye majanga kila mda utapigiwa kujuliwa hali ila sio uko normal kwenye harakati zako tu uanze kutegemea simu za salamu.
 
Mkuu natembea na usemi wako umaskini ni laana , sasa kama wana laana wazidi kuteseka tu , mm ni mwanafunzi wako mtiifuπŸ™πŸ™
Kwa hiyo unapenda wenzako wakiwa na shida?
Au ndio nyie wa atakuja tuu kisa mnajua ni lazima shida impate?
 

Kwa hiyo Mafanikio sio Jambo la msingi?

Kwenye upendo hakuna Lugha isemayo, simu ya hovyohovyo.
Kila kitu kitajengwa na dhamiri njema.

Mtu anataka kuwasiliana na wewe Kwa sababu ya upendo wewe unasema simu ya hovyohovyo?
Hapo ishu ni kuwa kama unakazi au Majukumu ndugu, jamaa na marafiki watajua.

Kila Jambo lifanyike Kwa kiasi na dhamiri njema.

Hicho unachokisema ndio chanzo kikuu cha Depression katika Ulimwengu huu. Ambapo ni ukosefu WA Upendo.
 
Mkuu natembea na usemi wako umaskini ni laana , sasa kama wana laana wazidi kuteseka tu , mm ni mwanafunzi wako mtiifuπŸ™πŸ™

Ni kweli umaskini ni laana.
Lakini Mungu akikufanikisha kwenye Maisha jukumu la mwisho ni kuwa Masihi, mkombozi wa Ndugu, Rafiki na jamii yako hasa wale wenye uhitaji. Yaani watakaoomba msaada wako. Au utakaoona wanahitaji msaada wako.

Kukomboa Wengine ndio iwe kusudio la mwisho Baada ya Mungu kukufungulia Njia. Wewe ni Masihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…