Analoshindwa Putin aliliweza Magufuli kwa kutumia zawadi ya tausi watatu kwa Museveni na Kenyatta

Analoshindwa Putin aliliweza Magufuli kwa kutumia zawadi ya tausi watatu kwa Museveni na Kenyatta

Kuna mtu yupo kiteto lkn anaona putin yupo pale kwa bahati mbaya
Putin hayupo pale kwa bahati mbaya tatizo lake ametawala mpaka kapitiliza. Mpaka kachokwa. Kumbuka mwaka 1999 alipoingia kremlin warusi wengi wanaoandamana kwa sasa walikuwa bado watoto wadogo na sasa wameshakuwa na uelewa wa nini wanachokitaka.

Ana tamaa ya madaraka akiona yeye tu ndio anayefaa kuongoza Russia, aliondoka madarakani akamuachia Medvedev ikulu ikiwa ni geresha tu akitaka kuidanganya dunia, halafu amerudi tena, Hana jipya na hana ubunifu wa kiuongozi.
 
Ukraine wanayo haki ya kuamua mstakabadhi waobila shinikizo la Putin. Hivi Vladimir Putin mzima huyu? Naona anataka kuwasha moto dunia haijawahi kushuhudia.
 
Ukraine wanayo haki ya kuamua mstakabadhi waobila shinikizo la Putin. Hivi Vladimir Putin mzima huyu? Naona anataka kuwasha moto dunia haijawahi kushuhudia.
Atapigwa asipoangalia. Rais wa Ukraine ni myahudi na kawaida yao wana umoja sana hawa jamaa, wanakuwa na network kamili siku zote ipo kazini.
 
Ila mwisho wa siku bado nia ya Ukraine kujiunga NATO ipo palepale.

Sasa Yeltsin alifanikiwa vipi kidiplomasia...!?
Miaka ya urais wake hukuwahi hata siku moja kusikia haya masuala ya Ukraine kuonewa wala kutaka kupigwa na Russia.

Chernomydin alikuwa waziri wa mambo ya nje mwenye kuijua kazi yake.
 
Video ya Vladmir Putin akihojiwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya magharibi inatembea mitandaoni. Putin anajitahidi sana kujenga hoja za kujibu maswali lakini kama kawaida yake anarudia makosa yale yale ya miaka yote. Putin aidha hana team nzuri ya Diplomasia au anaogopwa na wasaidizi wake ambao ni mawaziri wa Mambo ya nje wote aliowatumia tangu awe rais kwa mara ya kwanza mwaka 1999.

Putin anatumia nguvu kutaka Ukraine iwe karibu na Russia. Anataka kulazimisha wakati majibu atakayoyapata kutoka kwa Ukraine ni mepesi tu, sisi ni nchi huru wenye kuweza kufanya maamuzi yoyote muda wowote ule. Kwenye diplomasia kawaida nchi haitakiwi kulazimisha upendo au ridhaa ya mwingine. Ni mwendo wa ushawishi na nguvu ya kujenga hoja ndio inayotakiwa.

Hayati Boris Yeltsin ndio alikuwa kinara wa mahusiano ya kimataifa. Sauti yake akiongea ya mtu mlevi iliwachekesha viongozi mbalimbali wa wakati ule,. Ulevi wake wa pombe kali ulimpatia umaarufu haswa zile video zake zikimuonyesha akiwa na uso mwekundu akiwa kalewa chakali. Lilipokuja suala la diplomasia aliweza kuitawala Ukraine pasipo kulazimika kutumia majeshi.

Yeltsin alikuwa na mtu mmoja mahiri sana katika masuala ya diplomasia akiitwa Victor Stepanovich Chernomyrdin akiwa ni waziri wa mambo ya nje wa wakati ule. Asingeweza kusikika akiichimba mkwara Ukraine. Wala Russia isingeweza hata siku moja kulazimika kupiga mizinga kule Odessa. Silaha ya uhakika iliyoiweka Ukraine karibu na Russia ilikuwa ni nyepesi sana inaitwa 'nyama ya ulimi' waingereza wanaiita convincing powers, ukipenda unaweza ukaiita nguvu ya hoja. Unamteka mtu kwa hoja tu kwa kuyapangilia maneno mazuri mpaka anatulia na anakuwa upande wako kwa kila kitu.

Tanzania imeweza kudumu na umaarufu wake kimataifa ikibebwa na uteuzi mahiri unaofanywa na marais wa mawaziri wa mambo ya nje. Kuanzia RIP Mkapa alivyomuamini Kikwete kama waziri wake wa mambo ya nje. Akaja Kikwete akamwamini Benard Membe kama waziri wake wa mambo ya nje. Akaja JPM akamwamini Profesa Kabudi. Na sasa SSH anavyomuamini na kumtumia Mama Mulamula.

Jinsi Putin anavyoishindwa hii tasnia nzima ya mahusiano ya kimataifa ananikumbusha ile mbinu ambayo RIP Magufuli aliitumia ya kuwavuta kwake marais wa Kenya na Uganda kwa kuwapa ndege aina ya tausi. Kwa mtazamo wa haraka haraka mtu anaweza asielewe maana ya wale ndege. Lakini leo unampa tausi Mzee Museveni halafu kesho anakupa mradi wa kupitisha bomba la mafuta lenye urefu wa maelfu ya kilomita litakalotoa ajira nyingi za moja kwa moja.

Leo unampa tausi Kenyatta halafu kesho likitokea tatizo la kidiplomasia anakuwa wa kwanza kusema sisi ni majirani tusiokuwa na shida yoyote katika uhusiano wetu. Hiyo ni nguvu ya kidiplomasia ambayo Tanzania siku zote tunajua kutengeneza misingi ya kuiweza lakini cha ajabu Russia na ukubwa wa taifa walionao wanaonekana kuishindwa. Putin angeweza kabisa kumvuta karibu Ukraine kama ambavyo Yeltsin aliweza lakini hana maarifa hayo. Anaishia kutungua ndege za Uholanzi zinazokatiza juu ya anga la Ukraine na kutengeneza uhasama na taifa la mbali kabisa kwa kutaka tu kumtawala jirani.

Hayati JPM ulale mahali pema peponi, umenikumbusha maana ya wale tausi. Kwa wakati ule sikuona ni ishara zipi zilizojificha katika kitendo kile, ila baada ya kutazama namna Russia wanavyoshindwa kulinda utawala wa mataifa ya jirani yake ndio naelewa ujumbe mpana wa zawadi ya tausi kwa majirani wetu wawili wa kaskazini.

Mkuu mbona miaka yote mumeshinndwa kutumia diplomasia Zanzibar yaani ni majeshi Na kuuwa watu kila ufikapo uchaguzi ?
 
Ukraine inamuumiza kichwa Putin kwa sababu zinapakana, ule ukaribu wa pua na mdomo halafu Russia anakosa mbinu wala ushawishi wa hoja wa kumvuta karibu. Ni masuala ya ulinzi zaidi.

Ni sawa sawa na Zanzibar inavyoshikiliwa na Tanganyika. Huwezi kuelewa wala kuona umuhimu wa visiwa vikiwa chini ya Muungano lakini vikishakuwa huru ni hatari kwa uhuru wa huku Bara.

Hatari yake ni nini ? Mbona Singapore ilijitoa kutoka Malaysia kumetokea nini cha hatari ? UK wamejitoa European Union hatari gani ? Kabla muungano kulitokea hatari gani ?
 
Putin hana maarifa ya diplomasia. Upo muungano mwingine unaoongozwa na Russia, humo kuna kina Kirgystan na Belorussia, mataifa ambayo kwa Russia hayana nguvu ya kupinga maamuzi yao.

Wanataka na Ukraine nao wawaheshimu na wawanyenyekee, kitu ambacho ni ngumu kutokea. Ukraine ni nchi yenye ushawishi inabidi itumike akili ya ziada kuweza kuwa na ushirikiano nayo.

Wewe huielewi Ukraina wale waliotawala Wakati wa Yeltsin walikuwa pro Russia hawa wanaotawala sasa hivi ni Wayahudi, Na niliwaambia hapa kuwa hawa watasababisha vita Na ndivyo ilivyotokea
 
Back
Top Bottom