Anang'ang'ania kuwafahamu wazazi wangu.

Anang'ang'ania kuwafahamu wazazi wangu.

Mwamatandala

Member
Joined
Jul 17, 2009
Posts
44
Reaction score
3
Waungwana jamvini habari?
mimi nina mpenzi wangu tupo kwenye mahusiano takribani mwaka mmoja sasa.na nimemuahidi kwamba nitamuoa.
tatizo lake kila siku anataka ni kamtambulishe kwa ndugu zangu.mie nimemwambia asubiri nimalize masomo kwanza lakini hanielewi.naomba ushauri wenu,je ananipenda kwa dhati au lengo lake ni kuolewa tu?
 
inaonekana ulipömtongoza uliingia na gia za ndoa:rain:
 
Ana age gani? Inawezekana anazeeka anataka ndoa wewe unampotezea muda!
 
kama kweli ni mpenzi wako wa dhati why usimuonyeshe nduguzo,kumfahamisha kwa ndugu sio kumtambulisha rasmi ila ni kuweka ukaribu zaidi wenye manufaa kwa pande zote na kuongeza ushirikiano wenu katika mambo mbalimbali
Sasa hiyo fichaficha yako isijefika siku nduguyo akakutana nae akamtongoza bila kujua ni shemeji....
 
Na wewe unaogopa nini kumtambulisha kwa ndugu zako, au ina maana yeye ni for school use only. Basi mwambie ukweli
 
mahaba ya siku hizi bwana yamejaa mashaka tupu....mtu akigusia kitu kidogo tu mwenzie tayari mawasi wasi....:spider:
 
umalize masomo yepi ya secondary au chuo? kama ni secondary ni kweli unaweza kuogomba kuwa wazazi watakuona kuwa unachezea hela zao kwaajili ya wasichana lakini kama ni chuoni nafikiri hakuna kizuizi maana chuoni kuna watu wazima. otherwise unaintention zingine ndo maana unakataa kumpeleka kwa nduguzo
 
unaonyesha wewe hujiamini ktk hayo mahusiano pole sana................. weka wazi funga ndoa
 
Nashkuru wadau kwa ushauri wenu mahsusi.hatimaye nimefunguka na naweza kufanya maamuzi sahihi.mbarikiwe sana.
 
umalize masomo yepi ya secondary au chuo? kama ni secondary ni kweli unaweza kuogomba kuwa wazazi watakuona kuwa unachezea hela zao kwaajili ya wasichana lakini kama ni chuoni nafikiri hakuna kizuizi maana chuoni kuna watu wazima. otherwise unaintention zingine ndo maana unakataa kumpeleka kwa nduguzo
nipo chuo.ila nataka nilipe umuhimu wake suala hili.ndio maana nilitaka kulitekeleza baada ya masomo.
 
kama kweli ni mpenzi wako wa dhati why usimuonyeshe nduguzo,kumfahamisha kwa ndugu sio kumtambulisha rasmi ila ni kuweka ukaribu zaidi wenye manufaa kwa pande zote na kuongeza ushirikiano wenu katika mambo mbalimbali
Sasa hiyo fichaficha yako isijefika siku nduguyo akakutana nae akamtongoza bila kujua ni shemeji....

Kabisa mkuu kama kweli una nia ya kumuoa kuna ubaya gani kumtambulisha kwa Wazazi?
 
mpeleke tu kwa wazazi....ile si ndoa...ni hatua tu itakayompa amani na imani kwako.......!!!
 
mkuu wewe mtambulishe kwa wazazi na ndugu wengine ila kwenye ndoa mwambie asubiri mpaka umalize shule.
 
Back
Top Bottom