sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Asikwambie mtu nlikuwa nadhani kufukuza mtu kazi kitu simpo, nshawahi kushuhudia jamaa yangu aliifata bodaboda yake stendi akamnyanganya funguo kijana anaeiendesha mbele ya umati mkubwa nidhani rahisi, Pia nliwahi kushuhudia mjomba wangu alimfukuza kijana aliekuwa akimsaidia kuuza duka, alimfukuwa wazi wazi bila kujali kijana ataenda wapi, nikadhani rahisi.
Nikiri tu maishani sijawahi kumfukuza mtu kwasababu hii ndio biasharara yangu mpya nliyofungua baada ya kushawishika niwe na vimiradi ukiachana na kazi yangu katika shirika la serikalini,
Nimefungua kamradi ka oili za magari zile oili za sevisi na vifaa muhimu vya sevisi n.k
Kila wiki ni lazima nihesabu mzigo na kulinganisha na idadi ya mizigo iliyouzwa na hapo najua idadi inayotakiwa iwepo dukani.
Sasa wiki 3 zilizopita nlikuta utofauti wa mizigo ambayo ilikuwa haipatikani stoo ya kiasi cha elf 58 nikakaa na huyu muuzaji nikamwelewesha kwamba aandike kila kitu anachouza na akiona hela ya mauzo imezidi basi ni kwamba alisahau kuandika asifikiri ni muujiza akaenda kuipigia bata
wiki iliyopita nikaona material price variance (utofauti wa mizigo kwa gharama) ikiwa ni laki na 70, kwa kweli nlichukia sana na kwa vile mshahara wake ni laki 2 nikakata laki 1 nae asikie maumivu hio 70 nikampa onyo akirudia nakata yote.
Leo sasa nmehesabu mzigo nakuta variance imefika tena laki na 20
Nilipatwa na hasira nikawa naongea sauti ya juu kidogo bila kujijua dada akaanza kutoa machozi, nlipanga kumfukuza ila sikudhani itakuwa rahisi kiasi hiki.
Naombeni uzoefu wakuu, nlitaka nisingizie biashara ni yamjomba ili nimkodishe aje kumfukuza ila yup mbali sana