Mapenzi ni ya wawili, nyinyi (wewe na yeye) ndo mnajua u-deep wa uhusiano wenu. Wapo waliopita kwenye magumu kuliko wewe lakini ndoa zao zipo hai na active mpaka leo. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kujiuliza kabla haujafanya declaration yoyote;
1. Alikuwa hataki mfunge NDOA kwa sababu mama yake alikuwa anamkataza. Je, mkirudiana NDOA bado itakuwepo au ndo mtaishi kwa kuchezeana?? Mama yake ataridhia ndoa yenu??? Je, wewe utaolewa na wangapi (na yeye, na mama yake au wote)?? Je, ataendelea kumsikiliza mama yake katika mambo yenu yote ya ndani???
2. Wahenga husema, "kufanya kosa sio kosa, bali kurudia kosa" lakini wamesahau kusema kuwa "anayeomba msamaha ndie aliyekosa na ndiye atakayesamehewa". Kutuma dada zake si vibaya, lakini je una uhakika kuwa hao dada zake walitumwa na huyo mchumba wako?? Hata kama ni kweli walitumwa kuomba msamaha, bado yeye kama mkosaji ilibidi;
(i) Kukiri kosa
(ii) Kujutia kosa
(iii) Kuazimia kutorudia tena kosa. Yeye kama graduate wa chuo ni lazima atakuwa na akili timamu na uwezo wa kutunza kumbukumbu kwamba asirudie tena.
3. Alikuwa anakuzungusha kufunga ndoa na wewe. Baadae akakuambia kuwa amempa mimba mwanamke mwingine kwa hiyo hatafunga ndoa na wewe, mimba ikaharibika. Baada ya hapo akakurudia tena kwa kuomba msamaha, NASHAURI YAFUATAYO;
(i). Kaa nae, ongea nae kwa kirefu nini hasa malengo yake kuhusu wewe.
(ii) Inaonekana anataka mtoto, je kama upo tayari kubeba mimba yake, je atafunga ndoa nawe??? Na nini kianze, NDOA kisha mtoto au mtoto kisha NDOA???? Kwa ushauri wa kidini, "NDOA kwanza kisha mtoto" kwa life experience,"MTOTO kisha NDOA"
(iii) Miaka 5 ya uhusiano si michache, utakuwa unajua nguvu juu ya ufanyaji wake wa mapenzi ipoje [in terms of time(day) interval]. Je atapokuhitaji na wewe upo mbali yeye atafanyaje???
(iv). Umbali wa kijiografia kati ya maisha yake na ya mama yake ni lazima uwe mbali. ASIKUDANGANYE MTU, DUNIA YA SASA HIVI NDOA AU MAHUSIANO MENGI 'MACHANGA' VIKWAZO NI MAMA MKWE NA MAWIFI. Lakini Mkishaishi walau kwa miaka 10 na kuendelea wote hufyata mkia na kuja upande wako.
MWISHO mi sikushauri uachane nae maana kila mwanaume (mimi mwenyewe nikiwemo) ana madhaifu yake, na pia sikushauri uendelee nae kwa sababu sijui kwa undani mapenzi yenu. HIZO NI DONDOO ZA KUKUSAIDIA LAKINI UAMUZI UNAO WEWE MWENYEWE (SI WAZAZI WALA NDUGU ZAKO, SI WAZAZI WALA NDUGU ZAKE).
UHONDO WA NGOMA UNAUJUA WEWE, KAZI KWAKO................