ANATAFUTWA: Michael Juma anatafutwa na mwanae. Alikuwa askari magereza, mkazi wa Masasi na Mtwara mjini

ANATAFUTWA: Michael Juma anatafutwa na mwanae. Alikuwa askari magereza, mkazi wa Masasi na Mtwara mjini

Alizaliwa musoma miaka ya 1979-1980.Baba yake anaitwa Juma Michael.Mzee Juma alikuwa askari magereza-Musoma miaka ya 1980 na mkazi wa mtwara.Mama yake Anna alikuwa ni mnyiramba wa singida.Kama kuna mtu anamjua au yeye mwenyewe yupo naomba tuwasiliane anaweza kusaidia kupatikana kwa taarifa za mzazi wake mzee Juma,ambaye anatafutwa na kijana wake.

Mmejaribu pia kupitia pitia katika Fukwe za Ziwa Victoria au katika ' Boneti ' ya lile Gari Toyota Cruiser la juzi kule wanakolima sana Bange / Bangi Tarime mkamkosa?
 
Kama mada inavyojieleza hapo juu, huyu ndugu alikuwa askari magereza katika gereza la Musoma miaka ya 1980 na aliondoka Musoma mwaka 1983.Kwa maelezo tuloyapata aliacha kazi na kuanzisha karakana ya ufundi.

Anatafutwa na kijana wake alimzaa na mama mmoja anaitwa Monika mwenyeji wa Musoma Vijijini,alizaliwa miaka ya 1981.Kwa mujibu wa mama Monika,mzee Michael Juma alikuwa na mke mnyilamba wa Singida ambapo kwa kipindi hicho walikuwa na mtoto wa kike jina lake Anna na huyu mama walikuwa wanamwita mama Anna.

Pia mzee Michael Juma alikuwa anasema wazazi wake walikuwa wanaishi Masasi na badae walihamia Mtwara Mjini kwa muda,bahati mbaya jina la babu yake mzeze Michael hatukuweza kulipata.

Kama huyu mzee bado yupo hai au kama kuna mtu anamjua au kama huyu binti yake(Anna) yupo naomba sana kwani JF inaiunganisha Tanzania ,naomba tuwasiliane kwa namba 0789443404/0762364740.

Hii itasaidia huyu jamaa aweze kuwapata ndugu zake,kikubwa anataka tu amwone mzee wake na pia aweze kumsaidia mzee wake.

ASANTENI
 
Itakuwa Anapiga Stori Na Mzee Majuto Huko Aliko! Maana Maisha Haya Yenyewe Mafupi Mkuu, Si Unajua Tena.
Hata Dadaye Jiwe Kafia Pale Bugando, Juzi Tu.
 
Pole sana watu wa kale walikuwa na kinyongo sijui nina ndugu wawili waliondoka nyumbani na kutokomea pasipo julikana.

Mmoja wao alikuwa ni Askari mstaafu.
 
Nashukru sana wana bodi kuna member amenipigia ana details juu yake alikuwa rafiki ya baba yake na kuna tetesi yuko mbozi,anaumwa,nikishakamilisha kila kitu nitakuja kuwajuza.Asanteni.
Kila la heri aisee na tunaomba mrejesho.
 
Nashukru sana wana bodi kuna member amenipigia ana details juu yake alikuwa rafiki ya baba yake na kuna tetesi yuko mbozi,anaumwa,nikishakamilisha kila kitu nitakuja kuwajuza.Asanteni.
Karibu sana " hii ndio JF ....hakiharibikagi kitu hapa
 
Back
Top Bottom