Anatafutwa Mume mtu mzima 36 - 42

Njemba walihitilafiana na kila mtu akachukua ustaarabu wake, ila njemba alishaoa pande zingine kabisa

Yule njemba aliyezaa naye kwa sasa mbona hayupo naye? Ama wameitilafiana kimaisha? Funguka mleta uzi,kwani maswali ni kwako na kama ni wewe mwenyewe usisite kujuza hili!
 
King'asti, nimeshawaambia watu humu mimi niko engaged, na huu uzi ni on behalf of my friend. Sasa hao watakaogeuza kibao imekula kwao

Tatizo la hawa gt, hawakawii kukutaka wewe wakamkataa mlengwa! Kuwa muangalifu.
 
Kuna ujanja umezuka hapa JF. Kila mtu utamsikia...rafiki yangu anataka vile, rafiki yangu anashida hii............KUMBE MUANDIKAJI NDO MWENYE MAHITAJI... Huyo rafiki yako naye ana vigezo kama anavyovitaka huyo mwanaume awe navyo?
 
Kama unaona thread haikuhusu, unaweza kupita tu mkuu sio lazima utie neno

Kuna ujanja umezuka hapa JF. Kila mtu utamsikia...rafiki yangu anataka vile, rafiki yangu anashida hii............KUMBE MUANDIKAJI NDO MWENYE MAHITAJI... Huyo rafiki yako naye ana vigezo kama anavyovitaka huyo mwanaume awe navyo?
 
Anatakiwa aweke picha yake kwanza kabla ya maelezo.
 
kha!!! aibu...mbona watotot wenye bado vikinda kabisa....huyo anayo kazi kupata kidume
 
Baba Enock, wanaume wapo tatizo ni kwamba wengi wao hawajatulia, sio waaminifu n.k

Kweli umenena ila wakati mwingine hata selection ya wanawake inasababisha kuchagua wanaume wasiowaaminifu maana kuna wengine wakishaangalia mwonekano wa mtu tayari mambo mengine haangalii mwisho wa siku kile alichokuwa anadhani atakipata anakitegemea anakuta tofauti au hawaendani. (huku street unakuta mwanadada anasema yule jamaa ni handsome na anajipenda sema tu sijamzoea kumbe akishaingia kwenye kumi na nane zake inabidi aende zaidi kumchunguza) Maana mwanaume anaweza akawa kicheche kwa mwanamke huyu akawa serious kwa mwanamke mwingine but inategemea kama mdada analijigonga mwenyewe
 
Reactions: ram
Nimeipenda sifa namba 7! Da kwa jina langu tu situmi PM nishatengwa
 
Wapendwa wanajamii, kwanza pokeeni shukrani za dhati kutoka kwa my friend mwenye nia ya kweli ya kupata mume, lakini pia shukrani za pekee ziwaendee wanaume wote walioonesha interest ya kutaka kuwa nae, shukrani hizi ni kutoka kwa mtafuta mume, anawashukuru sana sana.

Anachoomba sasa amesitisha kupokea maombi,anahitaji muda wa kuwasiliana na hawa ambao wamejitokeza kwani maombi ni mengi, kama hatapatikana basi atarudi tena kuendelea kupokea maombi mangine na kama atapatikana pia atakuja kupitia hapahapa kuleta shukrani zake.

Nawasilisha!
 

Mamito ram mwambie shosti wako ajitahidi next time ajitokeze yeye mwenyewe, aidha amempata ama hajampata wa kufanana nae!
 
Last edited by a moderator:
Unajua mwita kila mtu ana interst zake, yeye hana kabisa interest na mambo ya mitandao ya kijamii, hopeful iko ck atajiunga tu. Nadhani akipata mume ndo atajua umuhimu wa JF


Mamito ram mwambie shosti wako ajitahidi next time ajitokeze yeye mwenyewe, aidha amempata ama hajampata wa kufanana nae!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…