Anataka kuja kwangu wakati sina hata godoro nalala chini, kwake nilikwenda nikakuta ana maisha mazuri

Anataka kuja kwangu wakati sina hata godoro nalala chini, kwake nilikwenda nikakuta ana maisha mazuri

Acha aje muda utaongea yeye anafuata promising future kwako jikite huko muonyeshe kwamba wewe mpambanaji hapo unajipanga tu....sio level yako
 
Mimi ni kijana wenu mtanzania halisi ila kwa sasa nipo huku Malindi,Kenya kujitafuta.

Sasa, kinachonileta kwenu ni hivi: Kuna mwanamke (maana ni mwanamke ako na 35 years) tulikutana kwa app inaitwa "tagged" sasa tukaongeaa mengi kama wiki kadhaa nyuma ila ikawa ngumu kuonana, unajua kazi tena.

Sasa leo nimepata time nzuri nikaenda kwake kwa mara ya kwanza tukaonana live. Sasa, kiukweli kajipanga ako vizuri kimaisha; yaani mimi labda naingia mara hata 10 hivi.

Tukaongea, mimi nikaamua kusepa. Sasa kasema kesho anakuja kwangu na mimi hata godoro ni kale kadogoo, nalala chini, sijajipata poa.

Sasa, jee kesho ajeee au nimpotezeee atakuja kunidharau? Nishaurini wazee wa JF

Ni mtihani kwako wa kutambua iwapo unataka kuwekeza kwenye uhusiano au vitu.

Ushauri; wekeza katika uhusiano wako; kesho kutwa utashangaa.
 
Mwambie ata geto sio lako ni la kuazima,, kuepushia aibu ya icho kigodoro,, mwambie wewe ni kama yesu tu huna pakulala,,, unalalaga lindo,, nenda kaazima iphone 15, uwe nayo siku anakuja ili ajue sio kwamba umeshindwa kumiliki geto labda hupendi tu
 
😃😃😃 hii ni chai iliyochanganywa na alikasusu walah.
Kivipi mkuu? Kuna wanawake wamechezewa,na wanatamani mtu wa kusupport,mkweli,si wa kuazima geto. Kikubwa asiwe amejimwambafai. Na kama kumruhusu,kwanza amwambie uhalisia wa maisha yake. Kwani kususwa kisa huna kitu,si kawaida tuuuu!!
 
Back
Top Bottom