Mama yeyote mjamzito anapohudhuria clinic katika kadi ya clinic kuna aina mbalimbali za vipimo unavyotakiwa kufanyiwa kama vile BP, Kisukari, UTI, VDL, HIV.<br />
<br />
Sasa katika hivyo vipimo hakuna suala la hiari kwa sababu limelenga katika uzazi salama. Mfano, ni lazima ijulikane kama umeambukizwa magonjwa yoyote ya zinaa STDs (Kaswende, gonorrhea, warps, n.k) ili kama uko +ve kwa hayo magonjwa utibiwe ili usije mwambukiza mtoto au usije jifungua mtoto mwenye ulemavu wa macho n.k. Kwa HIV ni lazima kwa sababu kwanza inaweka kumbukumbu ili wakati wa kujifungua ijulikanae kama wewe ni +ve utaratibu maalumu utaandaliwa kwa ajili yako. Lakini vilevile, kwa kuwa uzazi wa sasa hivi unakuwa na matatizo na wakati mwingine kujifungua kwa operation, tahadhari kwa madaktari lazima ichukuliwe katika hali yoyote ile kulingana na hali ya kiafya ya mjamzito.
Kwa hiyo hakuna suala la hiari kwa mjamzito. Kama hutaki kupima basi usibebe mimba. Ninasema hivyo kwa uzoefu kwa kuwa nimekuwa nikihudhuria nikimsindikiza "mywife" wangu, so i know everything. Na kimsingi kuna faida zaidi kwa mjamzito kujua hali yake ya HIV kuliko kutokujua. Hii pia ni kwa upande wa madaktari, wakunga na wauguzi wanaowahudumia hao akima mama wajawazito.
Hakuna sheria iliyotungwa na bunge ya kulazimisha hili suala, ila ni mwongozo wa wizara ya afya wa namna ya kuwahudumia wajawazito kuhakikisha uzazi salama kwa mama na mtoto anayezaliwa.