Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

whiteskunk

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
3,904
Reaction score
9,342
Tulidumu karibu miaka 10, nia yangu ilikiwa ni kumuoa ila baada ya kukamilisha mipango niliyojiwekea, ilipobaki miezi michache tuoane akanikalisha chini akaniambia kuwa hawezi kuendelea kuwa na mimi.

Ikabidi niheshimu mawazo yake japo roho iliniuma mpaka kufikia hatua nikawa napata maumivu kwenye moyo.

Nakumbuka kuna siku nilikuwa namfuatilia kwenye facebook nikitamani kujua aliyenipiku ananini kunizidi, nikakuta kamposti jamaa fulani mfupi kapiga picha mbele ya rav 4, roho iliniuma sana na ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukosa usingizi mpaka asubuhi, na kiherehere cha kumfuatia kikaishia palepale.

Baada ya kupita miaka mitano, Mwaka jana siku moja napeleka mzigo wa mteja mara simu ikaita kuchek namba ya airtel, kupokea anasema mimi I, nikamuambia mimi siongeagi na wake za watu akasema hajaolewa.

Akasema amenimiss anatamani kuniona tukapanga tukakutana, nilikuwa na hamu ya kuona maisha anayoishi,
Tukaenda anapoishi ni chumba kimoja kidogo kina kitanda tu na jiko la mkaa, amepauka amekonda. Akawa anampa mtoto kipande cha tikiti maji.

Hana kazi anategemea elfu 50 ya malezi ya mtoto anayopata kila mwezi kutoka kwa baba wa mtoto. Yenyewe aliipata kwa mbinde kupitia ustawi wa jamii.

Akanielezea kuwa yule mwanaume alikuwa ameoa ana watoto wa 3 na amezalisha wanawake kibao.

Akaniomba numpe nafasi awe mke bora mi nikawa namcheki tu alivyopauka.

Hivi kweli nipambanie maisha mpaka hapa nilipo alafu nioe mwanamke mwenye mtoto tena aliyenidhau.

Hakikisheni mkiacha mtu mnaenda kwa aliye bora zaidi. Ni hesabu rahisi tu.
 
Baada ya kupita miaka mitano, Mwaka jana siku moja napeleka mzigo wa mteja mara simu ikaita kuchek namba ya airtel, kupokea anasema mimi I, nikamuambia mimi siongeagi na wake za watu akasema hajaolewa.
Kwa hiyo jumla ni miaka 15? Acheni kuwazeesha watoto wa watu. Subiri haya mnayofanya watafanyiwa watoto wenu wa kike mtaona jinsi roho inauma. Karma
 
Swala sio kwenda Kwa aliyebora chief,hapo ni swala la karma kuingia kwenye system mkuu.hata kama ulikuwa juu mawinguni itahakikisha inakushusha chini sakafuni ugaregare huko.

*tujifunze kuachana Kwa wema
 
Hakuna mwanamke anaweza kukuvumilia ujipange kumuoa kwa miaka 10 usimlaumu bure.

Shida tunawalaumu kina mama bila kuwaza upande wa pili. Wewe unaweza ona ndoa sio ishu kuuuuubwa ila kwa kina mama huwa ni kitu sensitive sana. Umekaa nae miaka 10 huo sio uchumba tena ni kitu kingine. Kwani lazima umuoe kwa harusi kubwa, ungefunga nae ndoa nakuhakikishia huyo mama angekuvumilia kwa tabu na raha zako.

Ukishakuwa na mwanamke ambae age inasogea ndoa huwa ni sensitive sana. Kama unampenda muoe kisha muendelee kutafuta maisha pamoja.
 
Uyo sasa ni veteran kashamaliza vita zake anataka kutulia na wewe. Sio kwamba anakupenda hapana anaamini wewe ni bwege kwake atakupanga utapangika ili mwisho wa siku mtoto wake akue vizuri kwa gharama za hela yako.

Je, utamuoa au hutomuoa hilo sasa ni juu yako mkuu?
 
Duh...!! Zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Mi naona kama moyoni kwako bado ana nafasi mchukue umuoe.. hakikisha unamuhudumia mtoto kama wako, zile elfu 50 zisitishwe na aache mazoea na mzazi mwenzie.

Unaweza kuchukua mke mpya akawa na majanga pia matatizo yakaanza na upyaa.

Mmmh! Lakini mwenye mtoto tayari huwaga mtihani..
 
Mpe pole Sana Huyo single mom!

Aliathiriwa na jamii hasa mtizamo na DESTURI zetu za kijinga!

Kwamba;

Mliishi KWA Miaka kumi na BADO hiyo sio NDOA Hadi tafrija na CHETI Ndio iwe NDOA!kwani jamii iliwachukuliaje wakati mnaishi!!?

Huo ni ukoloni mamboleo wa kizungu!!

Angejiona kama mke Halali wa ndoa bila CHETI na tafrija angekuwa na good life nawewe!!

Hii dhana inaendelea kututafuna Sana and so Deep!
 
Mliishi KWA Miaka kumi na BADO hiyo sio NDOA Hadi tafrija na CHETI Ndio iwe NDOA!kwani jamii iliwachukuliaje wakati mnaishi!!?
Hata mimi nadhani walitakiwa wawe walishaanza maisha ya uhakika bila kujali Baraka za Padre wala Askofu.

Hizi mambo za pete na ndelemo ndelemo zinawakost wanawake.
 
Hapa umeridhika ila Ungekutana naye anajiweza gari kali, nyumba nzuri na mume wake hadithi ingekuwa tofauti na huenda kawivu kangekuvaa, ungetaka kula kimasihara kwa kujaribu kupasha kiporo ili amsaliti mumewe. Hivyo ndivyo tulivyo binadamu. Mtu akikuacha unatamani yamkute hayo yaliyomkuta x wako na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom