Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

Chief Dai mahari yako ..tena wakulipe Yote,otherwise wafunguliekesi ya utapeli...Nyapu zinazijielewa zipo kinao....Huyo ni mdangaji tu..Ungeoa kimeo
 
Acha ufala, ndoa ni ya mwanamke. Akikukataa usilazimishe, piga chini.
 
Kashaingia anga za wajanja huyu.Nakushauri dai mahari yako tafuta mwengine uoe.

Ila nakuhakikishia baadae anahitaji Sana ndoa hata ikibidi atataka umuoe mke wapili.

Usijichanganye ukamrudia tena.
 
Nenda kwao angalau warudishe pesa ya uchakavu, mshukuru Mungu kukuepushia msala
 
Shukuru Mungu hujamuoa bado ,ungekuwa umemuoa halafu anakuletea mambo meusi sijui ingekuwaje.
Nje ya mada,
Najiuliza swali hivi inawezekanaje watu mnaishi vizuri Tu hata zaidi ya miaka kadhaa lakini mnashindwa kufunga ndoa ni uchawi ama ni nini sababu mtu si ni yuletule WA siku zote au!!!?
 

Amekutana na mshededee mpya… umemchanganya ameona kwanini alichelewa na anaona kamwe hawezi kumuuacha.. shukuru hilo zimwi limetibuka kabla hujaoaa ungeoaa mke wa mtu.
 
Wewe dogo wenzako tulipofikia hatua ya kutoa mahali tulikuwa na stock ya kutosha iliyokuwa na maana akizingua x y anatake place, huna stock huyo ni mama yako? Mim naomboleza staki kuchokozwa
 
Hii ni kweli..unaishi Na MTU vizuri Ile unakaribia kuoa, mwanamke anasema hataki tena..inaumiza..ilishanitokea, Sasa sijui ni uchawi au
 
Acha ujinga chukua kadai chako hiyo pesa unywe mvinyo..huyo sio mke wa kuoa,amekuepusha na mengi mshukuru mungu
 
Man up broh, kaa kimya kubali matokeo na hata hiyo mahali usiende kudai, kuachwa ni kuachwa tu.
 
Mtu anataka muachane. Na bado hamjaoana sasa unataka uzungumze na mama yake ili iweje? Umuoe mama yake? Waambie wakurudishie mali mwache mwanamke akatafute changamoto nyingine.
 
Ni kheri kuumia sasa kuliko kuumia ukiwa kwenye ndoa, huna hata haya ya kuuliza mara mbili, tunza message hiyo, wape ndugu zake waage urudi kwako! Temana nae hilo jini litakutesa ukiling'ang'ania! Utakuja kunishukuru baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…