Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

Pole sana mkuu, achana na huyo mwanamke ni ngumu lakini huna budi kufanya hivyo.
Hata huko mkoa X,T alikopita ni wazi kuwa ana mwanaume na amekusaliti. Kwa namna unavyomjali na kumpenda hustahili kufanyiwa hivi hata kidogo, muache aende.
 
Mungu ana mpango na wewe ndugu yangu. Hebu achana nae mara moja wala usilazimishe.

Hata huyo mama yake anajua kila kitu, ni ngumu sana kwa mama kutozungumza na binti yake vizuri. Hapo anakuvungia tu.

Mapenzi hayalazimishwi mkuu
 
mtego umejifyatua wenyewe kabla ya kukunasa...kimbia nduki nene

NB:mahari arudishe ANDAZI HUYO
 
Ushachapiwa mkuu. Kubaliana na msimamo wake la sivyo utateseka sana
 
Ukweli humweka mtu huru , huyo dada binafsi nampongeza ! Hebu fikiria mtu mnaingia kwenye ndoa hana hisia na wewe ! Hiyo ndoa wewe mwenyewe mkuu ingekuliza ila kwa sasa utapata changamoto kidogo ya mazoea !! Fungua akili chukua chuma mpya hapo wanaohitaji ndoa ni wengi asizibe nafasi .
 
kwa kweli
Mwanamke wa aina hii kamwe awezi olewa kamwe ni kama kajiroga kabisa kabisa…..! Hivi anafikiri huyo mwanaume anayempa kiburi akijua alichomfanyia mwenzie nae si atakuwa mguu sawa na anajua hakuna mwanamke hapa?
Huyo lazima arudi kwa magoti na hakuna msamaha unapaswa kutolewa ni kumuacha ateseke hadi roho imtoke….
 
Kula chuma Hiko,,ngumu kumeza lakini ndio dawa hiyo,hukupigao ndio hukufunzao,, shukuru Mungu songa mbele,next time usitangaze kuoa kwa ndoa na harusi wahuni tunakamata unatia mimba anasogea mnaishi mnakuja kufunga ndoa mna watoto wanne keshazeeka hana pa kukimbilia,,,aaah aaah kataa ndoa za mapema
 
Hahahahahahhaa
Kwanza una lisiti(ili ikuwie rahisi kudai chako),japo hata hivyo nauli,chipsi kuku na nini bado utakula hasara tu.
Ndo maana wazungu huishi kivyao na kujijua wenyewe.
Mi nauli nikupe ya nini? Umepanga safari bila nauli? Mara utasikia nina njaa ntumie hela nikale. Kabla ya kufahamiana ulikuwa huli? Mara ohh, nitumie elfu mbili nikanunue vocha. Wewe ukimwambia nichukulie maji tu,utasikia sina chochote.
Kama kuoa, shirikisha wazazi kijijini au wapi wakutaftie wa kuendana na wewe. Na mkubali alivyo.
Sasa wengine wanajiona wana hela,wanataka wale wanaotembea nusu uchi, wanasahau kwamba ni mali za umma. Ona sasa
 
Daaaaahh
Sasa mwanamke akisema it's over huyo si ndio mzuri kumnyoosha.
Ushauri: Mwandikie sms ya kukubali ombi lake la kuachana rasmi.
Then mblock kila mahali usipate kuona tena sms yake yoyote, hata picha yake usiione popote.
Funga ndoa simple ndani ya miezi 2 tu kuanzia leo , wanawake wako mamilioni duniani.
Baada ya miaka miwili tu atachanganyikiwa na maisha yake kuvurugiga.
Mimi ndoa yangu ina miaka 7 ila wife nishampa msimamo wangu kuwa sioni kazi kufanya uamuzi wowote na muda wowote hivyo aishi kwa kutulia tujenge family.
 
Back
Top Bottom