Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

Hello wanajamvi
Mimi ni kijana wa miaka 30, ninaishi mkoa x kikazi.. nimekuwa na mahusiano na mwanamke kwa muda wa miaka 5 tumekuwa tukiishi pamoja, mwaka jana nilikwenda kwao na kutoa mahari.

Mwezi uliopita niliomba likizo moja ya vitu tulivyotarajia kuvifanya kipindi hicho cha likizo ni pamoja na kurudi nyumbani mkoa Y kwa ajili ya kusalimia wazazi na kuweka mipango ya ndoa.
Baada ya kulifikisha swala hili kwa mpenzi wangu yeye aliniomba kuwa aende mara moja kwao mkoa Z kumsalimia bibi yake then baada kama ya siku kama 3 atarudi kuungana na mimi.

Nilimpa ushirikiano wote katika safari yake hiyo pamoja na kufanya shopping, na kumlipia nauli, na kuwa na mipango mingi ya kufanya baada ya yeye kurudi na kuungana na mimi.

Cha kushangaza baada tu ya kufika kwao tu nikaanza kunotice hata pattern ya mawasiliano yamebadilika, hanijulii hali, nikimpigia simu anadai yupo busy. Nikimuuliza atarudi lini hanipi majibu ya uhakika.

Baada ya siku kama nne akanipigia simu kuwa anataka kurudi ila atapitia mkoa T kwa rafiki yake ninayemfahamu before kuja kuungana na mimi na kuniomba nimtumie nauli nikafanya hivyo.

Siku ninayotarajia kuwa atakuwa safarini anakuja kuungana na mimi akanitumia sms kuwa anaumwa sana, baadaye akaniambia kuwa amekosa magari ya kuja huku nilipo, ukimpigia simu hapokei lakini wakati wa jioni nikampata kwenye simu katika kumuuliza kuwa anaendeleaje ana mpango gani na hiyo safari akaniambia kuwa kuna ujumbe amenitumia kwenye simu.. kucheki ule ujumbe alikuwa ameandika kuwa anaona ni wakati umefika wa kumaliza mahusiano yetu.

Hivi sasa hapa nyumbani walikuwa wanamsubiria kwa ajili ya kudiscuss naye kuhusu swala la ndoa na tayari nimekwishalipa mahari kwao.

Hapa nipo kwenye dilema sijui la kufanya nimezungumza na mama yake na yeye anashangaa anajaribu kuwasiliana naye ila hapokei simu zake.

Huyu mpenzi wangu sijawahi kuwa na ugomvi wowote mkubwa tumekuwa tukiishi vizuri tu.
uliyempenda ana mwingine naye mwingine kapendwa na mwingine, mkuu move on huyo demu siyo wako ukiforce utakuja kupigwa na kitu kizito sana,
 
WANAUME WENZANGU MSIWE MNADHARAU DALILI MBAYA ZA AWALI UKILAZIMISHA UTAJUTA.

MWANAMKE HUWA ANASEMA UKWELI BILA KUJIJUA.

AKIWA NA MWAMBA MWINGINE HUWA ANAANZA KONA KONA...ELEWA HUYO DEMU ANAKAZWA NA MUHUNI MWINGINE ACHANA NAYE, PEWA MAHARI AU SAMEHE.

WANAUME SOKO LETU LIKO JUU SANA
 
Mkuu pole sana! Kuna watu ni wakatiri sana aiseee…Mkuu achana nae kabisa kata mawasiliano naye na usikubali kabisa kusuluhishwa na mtu yeyote kabisa kamwe usikubali huyo mwanamke hakupendi na hakutaki kabisa!
Ila wanawake muda mwingine unaweza usiwaelewe kabisa unaweza kuta anadanganywa na kajamaa wala hakato muoa kabisa na akana mpango kabisa!

Kitakachofata hapo ni wewe kusumbuliwa na huyo binti na watu ili msuluhishwe..kamwe usikubali kuwa na suluhu na mtu aliyekukataaa kwenye hiyo hatua …..usikubali suluhu hiyo kamwe kamwe…tafuta mwanamke mwingine oa huyo achana nae kabisa wala usikubali kukaa kikao nae….
Uchumba huwa hausuluhishwi hata kidogo
 
Back
Top Bottom