Anatumia Mabilioni Kurudisha Nyuma Umri Wake

Hyrax

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2023
Posts
964
Reaction score
2,675
444e6511a80817b6.jpg

Mjasiriamali wa teknolojia Bryan Johnson anatumia mamilioni ya dola kwa mwaka kujaribu kurejesha nyuma umri wake halisi wa kibiolojia wa miaka 45.

Byan hufanyiwa vipimo vya mara kwa mara na matibabu na kundi la wataalamu linaojumuisha madaktari 30 na wanasayansi, BBC inaripoti.

Muonekano wa mwili wake hauendani na miaka aliyoishi duniani. Bryan pia anasema madaktari wake wametumia karibu miaka 22 kubadilisha umri wa ngozi yake.''Kibiolojia, nimekula chumvi kiasi cha haja. Sikio langu la kushoto ni la mtu wa miaka 64 na ukaguzi wa ubora wake unasema nina miaka 18. Mapigo ya moyo wangu ni wa mtu wa miaka 37 na uwezo wangu wa kupumua vyema ni wa kijana miaka 18," alisema Byan .

Bryan pia anasema madaktari wake wametumia karibu miaka 22 kubadilisha umri wa ngozi yake. Alieleza kuwa mashine inayofanya kazi ya kumpunguzia umri, hupiga picha kadhaa za muonekano wa uso wake na kutoa karibu ripoti 10 zinazonesha ukubwa wa pua yake na uso mzima kwa ujumla. Anasema mashine hiyo inasaidia kufuatilia mara kwa mara uwezo wake wa kusikia.

Bryan anasema juhudi hizo hazijapata ufanisi wa kuridhisha lakini anajitahidi kufikia lengo lake.''Ni watu wachache wamevutiwa na jambo hili hasa watafiti kwani ni mwanzo mpya wa kuendeleza pale nitakapofikia. Lakini pia kuna wale walionikosoa sana. Hata hivyo nawapenda.’’

Pimbi wa Ludewa
 
Uzee ni uzembe kama pesa ipo, kukosa shep yeñye muonekeno mzuri ni ujinga kama pesa iko kwa mwanamke
 
View attachment 2632167

Unatumia mamilioni ya pesa kucontrol usizeeke nje wakati cell zinaendelea kuchakaa ndani sawasawa na mpango wa Mungu.....
 
Unatumia mamailioni ya pesa kucontrol usizeeke nje wakati cell zinaendelea kuchakaa ndani sawaswa na mpango wa Mungu.....
kwa mabilioni hayo anayotumia nadhani wanacontrol mpaka hizo cells
 
Wakina Michael jackson walishajaribu hayo wakashindwa,huyo anajitoa tu muhanga,na cha kushangaza anaweza akaondoka mapema kabla hata ya miaka 60,kwani kiwango cha madawa wanachotumia kumaintain hiyo hali pia ni kikubwa sana,fatilia ujuwe M.Jackson mathalan kwa siku alikuwa anakunywa vidonge vingapi.Pitia hapa uone hili balaa The drugs found in Michael Jackson's body after he died .....
 
Back
Top Bottom