Anayedaiwa kumuua mkewe ajirusha na kuligonga treni, afariki dunia

Anayedaiwa kumuua mkewe ajirusha na kuligonga treni, afariki dunia

Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya watu kujiua na wengine kuua, wenza wao sababu nyingi zikihusishwa na wivu wa mapenzi na imani za kishirikina.
Miaka hii kufuga ng'ombe kwaajili ya glass moja ya maziwa ni mateso wakati waweza kunywa maziwa restaurent au kwa mama lishe
 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina na Omary amefariki baada ya kujirusha kwenye treni eneo la Ubungo Maziwa baada ya kudaiwa kumua mke wake Mwanahamisi Mjeshi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zinaekeza kuwa tukio hilo la mwanamke kuuwawa zimetokea leo Jumatano Juni 28,203 saa moja asubuhi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amethibitisha kutokea kwa tukio hilo,
“Taarifa hizo ni za kweli na yeye amejirusha kwenye treni, lakini tunaendelea kufuatilia kwa karibu, taarifa zaidi nitazitoa lakini tukio hilo lipo,” alisema Muliro.

Akisimulia tukio hilo mmoja wa mashuhuda aliileza Mwananchi Digital kuwa wakati treni hiyo ikitokea Ubungo kuelekea Gerezani, ikiwa maeneo ya Maziwa gafla alijitokeza akiwa na viatu mkononi kisha kujirusha.

“Tukio limetokea saa 12 kasoro wakati treni ikitoka Ubungo kuelekea Gerezani, alijitokeza mwanaume akiwa anakimbia huku akiwa ameshika viatu mkononi na kujirusha kwenye treni,” ameeleza shuhuda huyo.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya watu kujiua na wengine kuua, wenza wao sababu nyingi zikihusishwa na wivu wa mapenzi na imani za kishirikina.

Februari mwaka huu Fausta Tesha (26), mkazi wa Mero Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro ameuawa kwa kukatwa na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha mwanaye wa wiki mbili kujeruhiwa kwa kisu na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) hata hivyo alifariki baadaye.
Mwanahamisi mjeshi, zingatia hapo kwenye mjeshi .

Wapumzike wanapostahili.
 
Matatizo ya Akili yapo katika jamii
Kuna mtu aliulizwa kama amewahi kuvuta hewa ya oxygen maishani mwake, akaruka kimanga akawataka wote waliowahi kuvuta hewa hiyo waende wakatubu na kumrudia Mungu haraka
 
Wanawake mnaoteseka wote njooni kwangu niwape upendo wa dhati..,
Nataka wale walioshindikana na kuteswa

Kama hamtaki, baki na bichwa lako kama chungu huko uliko uuwawe, Rubish kabisa
 
Kuna mtu aliulizwa kama amewahi kuvuta hewa ya oxygen, akaruka kimanga akawataka wote waliowahi kuvuta hewa hiyo waende wakatubu na kumrudia Mungu haraka
Hao ni wataka trend
 
Back
Top Bottom