Anayedaiwa kumuua mkewe kwa kunyimwa unyumba, akamatwa

Anayedaiwa kumuua mkewe kwa kunyimwa unyumba, akamatwa

Nuraty J

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
1,729
Reaction score
3,831
WEDNESDAY AUGUST 18 2021

jeshoi la polisipic

Moshi. Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kennedy Malekea (21), mkazi wa kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwatuhuma za kumuua mkewe Fausta Silayo (22) kwa kumchoma visu vya tumboni na mgongoni kwa madai ya kunyimwa unyumba.

Marehemu Fausta alikuwa na mtoto mchanga wa mwezi mmoja alichomwa visu hivyo Julai 23 na kusababisha kifo chake Julai 24 alipokuwa akipelekwa hospitali ya Huruma kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa Kennedy huyo baada ya kutoweka kwa siku 25 na kukimbilia nchi jirani ya Kenya baada ya kutenda tukio hilo.

"Ni kweli amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea," amesema Kamanda Maigwa.

Marehemu Fausta alizikwa katika kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwa wazazi wake, Julai 31 mwaka huu ambapo ameacha watoto wawili mmoja ana umri wa mwezi mmoja na mwingine wa mwaka mmoja

Chanzo: Mwananchi
 
Mzazi mwenzie hata siku 40 hajamaliza. Inamaana kama alijifungua kwa upasuaji ahkua amepona vizuri. Na hata kama alikua amejifungua kawaida bado damu ya uzazi ingalipo! Unamani vipi kufanaya mapenzi na mwanamke akiwa kwenye hali hiyo? Hizo nyingine sio nyege bali ni kujiendekeza.
 
Duh miaka 21 ameoa mke wa miaka 22?

Pengine aliozeshwa na wazazi na hayo ndio madhara yake,ukute hyo dogo hyo ndio mwanamke wake wa kwanza..
 
Moshi.

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kennedy Malekea (21), mwanaume wa kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwa tuhuma za kumuua mke wake Fausta Silayo (22) kwa kumchoma visu vya tumboni na mgongoni kwa madai ya kunyimwa unyumba.

Marehemu Fausta alikuwa na mtoto mchanga wa mwezi mmoja alichomwa visu hivyo Julai 23 na kuuawa kwake Julai 24 akiwa hospitali ya Huruma kwa matibabu.

Kamanda wa polisi Mkoa wa kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo baada ya kutoweka kwa siku 25 na kukimbilia nchi jirani ya Kenya baada ya kutenda tukio hilo.

"Ni kweli amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea," alisema Kamanda Maigwa.

Marehemu Fausta alizikwa katika kijiji cha Msinga wilayani Rombo kwa wazazi wake, Julai 31 mwaka huu ambapo anaacha watoto wawili akiwa na umri wa mwezi mmoja na mwingine wa mwaka mmoja
 
Mtoto wa kwanza ana mwaka mmoja wa pili mwezi mmoja ina maana mimba ya pili ilipatikana mtoto wa kwanza akiwa na miez mi2 inawezekana kama marehem angemkubalia ilikuwa mimba ya 3, mtihani kwakweli .
 
Duu Mme 21yrs mke 22yrs watoto wawili mkubwa ana mwaka 1 na wapili mwezi 1, daa familia hii jamani mbona hatari, poleni sana wafiwa
 
Mwanaume unatakiwa uoe angalau una miaka 25 hapo akili ya utu uzima inakuwepo.
Miaka 20 ni miaka ya balehe, kijana muda wote anawaza ngono tu.
Duu Mme 21yrs mke 22yrs watoto wawili mkubwa ana mwaka 1 na wapili mwezi 1, daa familia hii jamani mbona hatari, poleni sana wafiwa
 
Aachiwe haraka, mume gani ana miaka 21? Huyo mwanamke alikuwa anambaka kijana wa watu.
 
Back
Top Bottom