Anayedaiwa kumuua ‘Trafiki’ kuhukumiwa Machi 2023

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Machi 17, 2023 kusoma hukumu ya kesi ya mauaji ya askari wa kikosi cha usalama barabarani, Sajenti Mensah inayomkabili Amani Philipo.

Tarehe hiyo ilipangwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Lumuli Mbuya anayesikiliza kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake.

Akihitimisha ushahidi wake huku akiandamwa na kilio na kwikwi, shahidi namba mbili, Samuel Thomas aliieleza mahakama jinsi alivyokuwa na mshitakiwa siku anayotuhumiwa kufanya tukio na yeye kujumuishwa katika kesi hiyo.

Akiongozwa na mawakili wa kujitegemea, Hassan Kiangio na Selemani Almasi shahidi huyo alidai kuwa Julai 22, 2016 siku ambayo Amani anatuhumiwa kutekeleza mauaji alikuwa naye toka asubuhi hadi saa 4:00 usiku.

Alisema yeye siku hiyo akiendesha gari la Spacio walitoka Tangi Bovu saa tatu na nusu usiku ambako walikunywa bia kidogo kisha yeye na Amani wakaondoka kwenye baa ambayo inamilikiwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Michael.

Alidai alimfikisha Amani kwake Mbezi Africana saa nne usiku na yeye kuelekea kwake Tegeta na kumsisitiza Amani waonane siku inayofuatia kwa ajili ya kutekeleza azma yao ya kuchoma nyama.

Samuel alidai siku iliyofuata Julai 23, 2016, saa nne asubuhi alipigiwa simu na Amani na kuulizwa kama yupo nyumbani na alipomjibu kuwa yupo akamwambi kuwa yeye yupo getini anaomba amfungulie.

Alidai alipokwenda kufungua geti alishangaa kuona aliyeingia hakuwa Amani bali askari aliyejitambulisha kwa jina la Ben Magufuli na kumuuliza mahala alikokuwa na Amani jana yake.

Alidai alimweleza safari yao iliyowafikisha Muhimbili hadi baa na kisha kumrejesha nyumbani saa nne usiku.

Alisema askari alimtaka aseme ukweli ili amsaidie Amani kwani ana matatizo, akamuuliza matatizo gani? Hakumjibu bali akatoka naye nje ya geti ambako alimkuta Amani akiwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Oswald Mang’ombe huku wamefungwa pingu.

“Nilimuuliza Amani nini kinaendelea? Amani akajibu hata mimi sijui kwani wamekuja kunikamata tu nyumbani,” alisema.

HABARI LEO
 
Hii habari mbona imeishia juu juu? Maelezo ya jinsi huyo askari alivyouwawa na muda aliouwawa hakuna? Hao waandishi nawashangaa kuona hii habari inajitosheleza!
 
Sijaelewa hapo Ben magufuli kaingiaje hapo au naye anahusika

Ova
 
Ben Magufuli ni Askari wa Oysterbay,alichaguliwa kuwa Bodyguard wa Magufuli alivyokuwa Waziri wa Ujenzi mwaka 2001 mpaka siku Magufuli anateuliwa kuwa Mgombea Urais wa CCM,hivyo amezoeleka kwa jina la Ben Magufuli lakini jina lake ni BERNATUS RUHAZA
Ni askari mwenye ukwasi wa maana
Pia....mpaka namulizaga kwann usiache upolisi tu
Magu alipopataka lile sekeseke jamaa ndy alimuokoaga

Ova
 
Hii habari mbona imeishia juu juu? Maelezo ya jinsi huyo askari alivyouwawa na muda aliouwawa hakuna? Hao waandishi nawashangaa kuona hii habari inajitosheleza!
Wao waandishi wamechukua cha mahakamani siku ya kesi
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Machi 17, 2023 kusoma hukumu ya kesi ya mauaji ya askari wa kikosi cha usalama barabarani, Sajenti Mensah inayomkabili Amani Philipo.

Tarehe hiyo ilipangwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Lumuli Mbuya anayesikiliza kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake.

Akihitimisha ushahidi wake huku akiandamwa na kilio na kwikwi, shahidi namba mbili, Samuel Thomas aliieleza mahakama jinsi alivyokuwa na mshitakiwa siku anayotuhumiwa kufanya tukio na yeye kujumuishwa katika kesi hiyo.

Akiongozwa na mawakili wa kujitegemea, Hassan Kiangio na Selemani Almasi shahidi huyo alidai kuwa Julai 22, 2016 siku ambayo Amani anatuhumiwa kutekeleza mauaji alikuwa naye toka asubuhi hadi saa 4:00 usiku.

Alisema yeye siku hiyo akiendesha gari la Spacio walitoka Tangi Bovu saa tatu na nusu usiku ambako walikunywa bia kidogo kisha yeye na Amani wakaondoka kwenye baa ambayo inamilikiwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Michael.

Alidai alimfikisha Amani kwake Mbezi Africana saa nne usiku na yeye kuelekea kwake Tegeta na kumsisitiza Amani waonane siku inayofuatia kwa ajili ya kutekeleza azma yao ya kuchoma nyama.

Samuel alidai siku iliyofuata Julai 23, 2016, saa nne asubuhi alipigiwa simu na Amani na kuulizwa kama yupo nyumbani na alipomjibu kuwa yupo akamwambi kuwa yeye yupo getini anaomba amfungulie.

Alidai alipokwenda kufungua geti alishangaa kuona aliyeingia hakuwa Amani bali askari aliyejitambulisha kwa jina la Ben Magufuli na kumuuliza mahala alikokuwa na Amani jana yake.

Alidai alimweleza safari yao iliyowafikisha Muhimbili hadi baa na kisha kumrejesha nyumbani saa nne usiku.

Alisema askari alimtaka aseme ukweli ili amsaidie Amani kwani ana matatizo, akamuuliza matatizo gani? Hakumjibu bali akatoka naye nje ya geti ambako alimkuta Amani akiwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Oswald Mang’ombe huku wamefungwa pingu.

“Nilimuuliza Amani nini kinaendelea? Amani akajibu hata mimi sijui kwani wamekuja kunikamata tu nyumbani,” alisema.

HABARI LEO
Kwanza ninaungana na familia ya marehemu trafiki polisi kuomboleza msiba wa ndugu yao kipenzi. Hasara ya kumpoteza mtu huwa haina replacement. Tunamuomba Mungu ampumzishe askari wetu.

Jambo la pili. Kwa maelezo ya shahidi ni wazi kuwa jeshi la polisi wamejiweka juu ya sheria ambapo wanamkamata na kumshtaki mtu yeyote hata kama hakuna ushahidi unaojitosheleza.

Kinachosababisha hili ni kutoheshimiwa kwa Katiba na Sheria za nchi kunakofanywa na viongozi wetu wanaowateua makamanda wa polisi.

Mungu atussidie
 
Nikukumbuka ile kesi ya Mbowe, ni hakika bin shairi kabisa Polisi hawafuati misingi ya utendaji wao wa kazi. Ndio maana mahakamani Kibatala alikuwa anatumia PGO kuwasambaratisha....

Unamkamataje mtu unayemtuhumu kwa mauaji kirahisi namna hiyo?
 
Back
Top Bottom