Anayedaiwa kumuua ‘Trafiki’ kuhukumiwa Machi 2023

Anayedaiwa kumuua ‘Trafiki’ kuhukumiwa Machi 2023

Nikukumbuka ile kesi ya Mbowe, ni hakika bin shairi kabisa Polisi hawafuati misingi ya utendaji wao wa kazi. Ndio maana mahakamani Kibatala alikuwa anatumia PGO kuwasambaratisha....

Unamkamataje mtu unayemtuhumu kwa mauaji kirahisi namna hiyo?
NIngekuwa Jaji ningeagiza polisi kufungua jalada la uchunguzi dhidi ya hao askari waliomkamata na kumfungulia kesi Amani

Ukiona polisi wanakusukumia mzigo, ujue kuna wahaka
 
Kila ninapomuona polisi nahisi kama nimeiona taswira ya shetani.

Wana mambo mengi ya hovyo kuliko viapo vyao
Siku moja polisi ambaye ni jirani na rafiki yangu aliponilengesha kwa polisi mwenzie bila kujua aliyenilengesha kwake ni classmate wangu O level ndipo siku nilipofunga rasmi urafiki na haya majama....

Nilipata tatizo la traffic case.... nataka nishughulikie mambo ya insurance... Nikammfuata jamaa. Akanambia ngoja nikuunganishe kwa mtu atakayekusaidia kwa haraka zaidi... Kumbe kashamwambia "huyo ni jirani yangu nimeshindwa kumkamua... najua ana vihela, mkamue lakini hakikisha napata elfu 50 yangu".... ***** wallah... Yani haya ananiambia classmate wangu ambaye ndo nimepelekwa kwake anisaidie... Na unaweza kukuta huyu classmate wangu pia kaniuza

Pumbaf na robo
 
Kiukweli huyo dogo Amani kesi imemuangukia kila mtu ameshangaa. Amesota jela muda mrefu sana hadi huruma lakini ndio hivyo hadi mahakama itende haki.
 
Ukisoma hii taarifa utajua tunashida kubwa mno kwenye mifumo yetu, mtu anasota jela karibia miaka 6 kwa jambo ambalo seems halikuchunguzwa vyema!! Kama mahakama ikiona hana hatia hiyo miaka karibia 6 ya msoto atafidiwa vipi?

Haya mambo yasikie yasikukute aisee!!
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Machi 17, 2023 kusoma hukumu ya kesi ya mauaji ya askari wa kikosi cha usalama barabarani, Sajenti Mensah inayomkabili Amani Philipo.

Tarehe hiyo ilipangwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Lumuli Mbuya anayesikiliza kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wake.

Akihitimisha ushahidi wake huku akiandamwa na kilio na kwikwi, shahidi namba mbili, Samuel Thomas aliieleza mahakama jinsi alivyokuwa na mshitakiwa siku anayotuhumiwa kufanya tukio na yeye kujumuishwa katika kesi hiyo.

Akiongozwa na mawakili wa kujitegemea, Hassan Kiangio na Selemani Almasi shahidi huyo alidai kuwa Julai 22, 2016 siku ambayo Amani anatuhumiwa kutekeleza mauaji alikuwa naye toka asubuhi hadi saa 4:00 usiku.

Alisema yeye siku hiyo akiendesha gari la Spacio walitoka Tangi Bovu saa tatu na nusu usiku ambako walikunywa bia kidogo kisha yeye na Amani wakaondoka kwenye baa ambayo inamilikiwa na mtu aliyemtaja kwa jina la Michael.

Alidai alimfikisha Amani kwake Mbezi Africana saa nne usiku na yeye kuelekea kwake Tegeta na kumsisitiza Amani waonane siku inayofuatia kwa ajili ya kutekeleza azma yao ya kuchoma nyama.

Samuel alidai siku iliyofuata Julai 23, 2016, saa nne asubuhi alipigiwa simu na Amani na kuulizwa kama yupo nyumbani na alipomjibu kuwa yupo akamwambi kuwa yeye yupo getini anaomba amfungulie.

Alidai alipokwenda kufungua geti alishangaa kuona aliyeingia hakuwa Amani bali askari aliyejitambulisha kwa jina la Ben Magufuli na kumuuliza mahala alikokuwa na Amani jana yake.

Alidai alimweleza safari yao iliyowafikisha Muhimbili hadi baa na kisha kumrejesha nyumbani saa nne usiku.

Alisema askari alimtaka aseme ukweli ili amsaidie Amani kwani ana matatizo, akamuuliza matatizo gani? Hakumjibu bali akatoka naye nje ya geti ambako alimkuta Amani akiwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Oswald Mang’ombe huku wamefungwa pingu.

“Nilimuuliza Amani nini kinaendelea? Amani akajibu hata mimi sijui kwani wamekuja kunikamata tu nyumbani,” alisema.

HABARI LEO

Tatizo uwezo wa kupeleleza kwa askari wetu ni mdogo sana….wanachojua wao ni kuwapiga nyayoni na kuwalazimisha wakili makosa yao….ile kesi ya ugaidi ya mbowe ilitufungua mengi….police inatakiwa wajikite kwenye kufundisha wapelelezi wao,waboreshe vitengo vya uchunguzi wa kisasa ili wawe na uwezo wa ku connect dot.

Nimeona lile tukio la yule mama kuua watoto na yeye kujinyonya,haraka haraka wanasema kajinyonga,wamefanya uchunguzi kubaini ni kweli kajinyonga!?
 
Pesa na kazi ni Tofauti ni Mimi Mwenyewe Ben Magufuli askari Mtiifu katika Taifa langu
Hongera, chimbo lako la Las kalinyo
Nmelikubali watu wanaburudika 24/7
Juma3 mpk juma2

Ova
 
juzi kati uko morogoro wilaya ya kilombero panaitwa mang'ula, kuna dereva pikipiki amemgonga Traffic officer barabaran ktk eneo lake la kazi adi kaua. uyo boda saiz yupo hospitalini na pingu zake na uyo askari ameshazikwa ardhini ameiacha gari yake aina ya spacio pemben imepaki.
 
huyu ben kipindi cha makonda yupo mkuu wa mkoa alikoswa koswa ila wenzake wa pale ostabey sijui walitoka.
Huyu si ndio mmiliki wa BM SALOON ya Kinondoni. Jamaa anaukwasi wa kutisha sana na sijui kama maafisa wa wa maadili wameshamchunguza huyu. Polisi hasa idara ya upelelezi ni matajiri sana tena sana wana utajiri wa kutisha, ila huyu BM mwisho wake kamwe hauwezi kuwa mwema. Polisi wengi wanaobambikia watu kesi wanamaliza maisha yao kwa mateso makubwa sana. Wabunge wetu lazima watakiwe kuwepo na chombo cha kujilizisha na hizi kesi kabla ya kumpeleka mtuhumiwa mahakamani kwa kumhoji askari anayehusika na kesi hiyo kwa kula kiapo. Tuachane a huyu DPP.
 
na hoteli pale mwenge.mshahara wa polisi sijui kama anatumia maana ukimuona unaweza kujua kibopa fulani.

ostabey polisi pale kuna uvundo ila tunyamaze
 
na hoteli pale mwenge.mshahara wa polisi sijui kama anatumia maana ukimuona unaweza kujua kibopa fulani.

ostabey polisi pale kuna uvundo ila tunyamaze
Kavipata wapi vyote hivi?! Kwa wenzetu walioendelea na wanaoheshimu utu na heshima, huyu BM kamwe asingekuwepo kazini lakini ndio hivyo nchi imeoza sana hii mtu unatakiwa kukaa kwa tahadhari kubwa sana. Mahakama, polisi na majaji wetu wanaendeshwa na rushwa tu.
 
Siku moja polisi ambaye ni jirani na rafiki yangu aliponilengesha kwa polisi mwenzie bila kujua aliyenilengesha kwake ni classmate wangu O level ndipo siku nilipofunga rasmi urafiki na haya majama....

Nilipata tatizo la traffic case.... nataka nishughulikie mambo ya insurance... Nikammfuata jamaa. Akanambia ngoja nikuunganishe kwa mtu atakayekusaidia kwa haraka zaidi... Kumbe kashamwambia "huyo ni jirani yangu nimeshindwa kumkamua... najua ana vihela, mkamue lakini hakikisha napata elfu 50 yangu".... ***** wallah... Yani haya ananiambia classmate wangu ambaye ndo nimepelekwa kwake anisaidie... Na unaweza kukuta huyu classmate wangu pia kaniuza

Pumbaf na robo
Hata mimi iliwahi kunikuta hii! Hawa viumbe rafiki/jirani/ndugu yao wa damu ni pesa tu!

Ni watu wanapenda sana kusaidiwa, ila wewe ukiwa na shida; wanakusukumizia kwa mtu usiye fahamiana naye, ili wakutoe upepo.
 
juzi kati uko morogoro wilaya ya kilombero panaitwa mang'ula, kuna dereva pikipiki amemgonga Traffic officer barabaran ktk eneo lake la kazi adi kaua. uyo boda saiz yupo hospitalini na pingu zake na uyo askari ameshazikwa ardhini ameiacha gari yake aina ya spacio pemben imepaki.
Mang'ula ya wapi hiyo! Nimeishi kwa miaka sana hapo. Nakumbuka sana maeneo ya Mang'ula A, B, Corner, Posta, Mwaya, Mgudeni, Katulukila,
 
Back
Top Bottom